Rafiki yangu mpendwa,

Kadiri ninavyopata nafasi ya kuwahudumia watu wengi, ndivyo ninazidi kuona makosa na matatizo yanayojirudia rudia kwa wengi.

Nimekuwa naona baadhi ya makosa machache ambayo watu wengi wanayafanya na yanawagharimu sana kwenye maisha yao.

Watu wengi wanafanya mambo ambayo yanakuwa kikwazo kwao kufanikiwa, lakini wao wenyewe wanakuwa hawajui kama wanajizuria kufanikiwa.

Hivyo utawakuta watu wanakazana sana, lakini hakuna hatua wanayopiga licha ya kuweka juhudi kubwa.

cropped-mimi-ni-mshindi

Hapa nakwenda kukushirikisha sifa saba za watu wengi wanaojizuia kufanikiwa, na baada ya hapo nitakupa suluhisho unalopaswa kufanyia kazi kama una sifa yoyote katika hizo saba.

SIFA YA KWANZA; Hujui kwa hakika nini unataka na maisha yako.

Kama bado hujajua nini hasa unataka na maisha yako, kaka hujui kusudi la wewe kuwa hapa duniani, unajizuia wewe mwenyewe kufanikiwa.

Kwa sababu kama hujui unakokwenda, hutaweza kujua hata kama umefika au hujafika. Pia utapoteza muda wako mwingi kujaribu vitu ambavyo siyo sahihi kwako na hilo litazidi kukupotezea muda wako.

SIFA YA PILI; Vipato vyako havikutani.

Kama upo kwenye ajira au biashara kwa muda, na vipato vyako havikutani, basi unajiweka kwenye wakati mgumu kufanikiwa. Kwa sababu kama kipato kimoja kinaisha kabla ya kipato kingine kufika, hutaweza kuchukua hatua sahihi unazopaswa kuchukua ili kufanikiwa.

SIFA YA TATU; Umewahi kuchukua mikopo lakini hujui umefanyia nini.

Kama umewahi kuchukua mkopo, na wakati unachukua mkopo huo ulikuwa na mpango fulani, ukachukua mkopo huo na ukautumia mpaka ukaisha, lakini hujui mkopo huo umeishaje, basi unajiwekea kikwazo kwenye mafanikio yako.

Watu wengi wamekuwa wanakimbilia kuchukua mikopo ambayo siyo sahihi kwao, wanaitumia vibaya, na mwisho wanabaki na mzigo wa kulipa mkopo na wasione kikubwa walichofanya na mkopo waliotumia.

SIFA YA NNE; Umeshindwa kwenye biashara na kususa.

Kama umewahi kuanzisha biashara yoyote ile, ikashindwa kwa sababu zozote unazojiambia, lakini baada ya biashara hiyo kushindwa, umejiambia hutafanya tena biashara. Yaani kwa kifupi umesusa, hutaki tena kusikia chochote kuhusu biashara, maana unaona wewe huna mkono wa biashara.

Ukweli ni kwamba kuna makosa uliyoyafanya wewe mwenyewe ndiyo maana biashara hiyo ilikufa. Hata kama unajishawishi ni wasaidizi wako waliua biashara, wanasema samaki huwa anaanza kuoza kichwani, hivyo matatizo yalianzia kwako kisha yakaenda kwa wengine.

SOMA; Sababu Moja Kubwa Kwa Nini Biashara Inakuwa Ngumu Kwako Na Jinsi Ya Kuivuka Sababu Hiyo.

SIFA YA TATO; Umeshafanya biashara zaidi ya tatu ndani ya mwaka mmoja.

Kama ndani ya mwaka mmoja, umeshafanya biashara zaidi ya tatu, na zote zinashindwa, upo kwenye upande wa kupishana na mafanikio. Hii ni kwa sababu unakuwa kwenye hali ya kujaribu jaribu na hujajitoa hasa kufanikiwa kwenye biashara.

Kurukia rukia kila aina ya biashara unayosikia inalipa, bila hata ya kuichunguza kwa kina, ni dalili kwamba mafanikio yatakuwa magumu sana kwako.

SIFA YA SITA; Kipato chako hakiongezeki.

Upo kwenye ajira au biashara kwa muda mrefu lakini kipato chako ni kile kile, hakiongezeki. Hii ni dalili kwamba hakuna thamani kubwa unayotoa, na kama hutoi thamani, unajiandaa wewe mwenyewe kushindwa.

Ongezeko la kipato chako ni kiashiria kwamba thamani unayoitoa nayo inaongezeka.

SIFA YA SABA; Kupoteza fedha kizembe.

Kama umewahi kukopa fedha, au kuchukua fedha zako na kumkabidhi mtu mwingine, ili azifanyie biashara na wewe upate tu faida, bila ya makubaliano ya kisheria, upo kwenye upande usio wa mafanikio.

Wapo watu ambao wamekuwa wanaamini sana maneno ya wengine, hasa ya wale watu ambao ni wa karibu kwao. Wanapewa mpango wenye hamasa na kuchukua fedha zao kuwakabidhi watu hao, wakiamini hawawezi kuwatapeli. Ni kweli wanaweza wasiwatapeli, lakini wanakutana na changamoto ambazo hata wao wenyewe hawawezi kuzitatua, hivyo mpango unashindwa.

Rafiki yangu, kama una sifa yoyote kati ya hizo saba, kuna kitu kimoja ambacho unakikosa. Pamoja na juhudi kubwa ambazo unaendelea kuweka kwenye maisha yako, unakosa mwongozo sahihi wa wewe kufanya maamuzi yako.

Kama una sifa yoyote kati ya hizo saba, utakuwa unafanya maamuzi yako kwa hisia au kwa mazoea. Utakuwa unaangalia wengine wanafanya nini na wewe unafanya. Sasa itakuwa vigumu sana kwako kuweza kufanikiwa kama huna msingi unaouishi na kuusimamia.

HATUA MUHIMU KWAKO KUCHUKUA.

Rafiki yangu, kama una sifa yoyote kati ya hizi sana, kuna hatua muhimu sana unayopaswa kuichukua. Hatua hiyo ni KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu muhimu sana ya mafunzo ambayo ninaitoa. Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kuwa kwenye kundi maalumu la wasap la mafunzo. Pia unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo yaliyopo kwenye blog ya KISIMA CHA MAARIFA.

Muhimu zaidi, kwenye KISIMA CHA MAARIFA utapata mafunzo haya, ambayo yatakuwezesha ubadili sana maisha yako.

MOJA; MSINGI WA MAISHA YA MAFANIKIO. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunaendesha maisha yetu kwa msingi mkuu wa mafanikio ambao ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, kwa kujiunga na KISIMA, utaelewa kwa undani msingi huu na jinsi ya kuuishi ili kufanikiwa.

MBILI; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kuna masomo ya semina ya elimu ya msingi ya fedha. Kwenye masomo haya utajifunza kila unachopaswa kujua kuhusu fedha. Kuanzia kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kuweka akiba, kuwekeza, kulinda fedha zako na hata kuacha wosia kwenye fedha zako. Ukipata elimu hii ya msingi ya fedha, sehemu kubwa ya matatizo yako ya kifedha yatatoweka kabisa.

TATU; SEMINA YA UKUAJI WA BISHARA YAKO. Zipo njia 50 unazoweza kuanza kutumia sasa hivi kwenye biashara yako na ikaweza kukua sana, bila ya kujali unaanzia wapi. Njia hizi zipo kwenye masomo ya semina ya ukuaji wa biashara. Kama upo kwenye biashara au unatarajia kuingia kwenye biashara, unapaswa kusoma masomo haya.

Rafiki yangu, masomo hayo na mengine mengi, utayapata kwa gharama ya ada ya mwaka mmoja, ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Hii ina maana kwamba ukishalipa ada hiyo, utapata mafunzo hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Karibu leo ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA uondokane changamoto nyingi zinazokuzuia wewe usifanikiwe.

Kujiunga tuma ada kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe kwa wasap namba 0717396253 wenye majina yako kamili, namba ya simu na email na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA, na utaunganishwa na KISIMA CHA MAARIFA.

Rafiki, usiendelee kujitesa na kujizuia kufanikiwa, karibu kwenye nyumba ya maarifa na hamasa ya mafanikio, karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Chukua hatua hii muhimu sana kwako leo ili uweze kuishi maisha yenye maana kwako na yenye mafanikio makubwa.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)

Kupata huduma nyingine za ukocha tembelea www.amkamtanzania.com/kocha

Kupata vitabu vizuri vya kusoma tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu

Usomaji