Rafiki yangu mpendwa,
Furaha kubwa sana ninayoipata kila siku mpya ni kadiri watu wengi zaidi wanavyojitoa kwa ajili ya mafanikio zaidi.
Miaka mitano iliyopita, wakati naanza huduma hii ya uandishi wa hamasa na mafanikio, watu wengi walikuwa hawaelewi na hata wengi walisema Watanzania bado hawana mwamko huo, wanapenda kusoma vitu vya udaku,, umbeya na siasa.
Lakini mimi nilijiambia kitu kimoja, siandiki kwa ajili ya kila mtu, naandika kwa ajili ya wachache, na kama mimi nina kiu ya mafanikio makubwa, basi Tanzania nzima hawatakosekana watu wengine angalau elfu moja ambao wana kiu kubwa ya mafanikio.
Na hivyo lengo langu kuu likawa kuwafikia watu elfu moja pekee, ambao wana kiu kubwa ya mafanikio, ambao wapo tayari kujitoa zaidi, ambao hawatafuti njia za mkato za kufanikiwa.
Kwa kuweka juhudi na kutokukata tamaa, Kupitia AMKA MTANZANIA nimeweza kuwafikia Watanzania zaidi ya elfu 10, hawa ni wale ambao kwa kuchagua kwao wenyewe, walinipa mawasiliano yao (email na namba ya simu) ili niwe nawatumia masomo zaidi. Japo wengi hawakuwa wafuatiliaji wa muda mrefu, lakini kwa sasa, angalau watu zaidi ya elfu moja, wanasubiri kujifunza kitu kutoka kwangu kila siku.
Kitu kingine ambacho kinaendelea kutokea tofauti na wengi walivyozoea huko nyuma, ni utayari ambao watu wapo tayari kujitoa ili kuweza kupata mafanikio. Zamani ilizoeleka kwamba ushauri unapatikana bure tu, makundi ya wasap unajiunga bure tu, makala mtandaoni unasoma bure tu. Lakini mimi nilianzisha huduma ya juu zaidi ya kulipia kwenye maeneo hayo yote yaliyozoeleka kuwa ya bure, na watu wapo tayari kulipia.

Hii inaonesha ni kwa kiasi gani watu wana kiu kubwa ya mafanikio, na ndiyo maana kila siku nimekuwa nakazana kushirikisha maarifa bora zaidi ili kila mmoja wetu aweze kuchukua hatua zaidi. Lengo langu kuu ni kila anayekutana na mimi, kupitia kazi zangu basi asibaki pale alipo. Hata kama hatachukua hatua, basi angalau abebe mzigo wake, aache kulalamika na kulaumu wengine na ajipe majukumu ya maisha yake.
Rafiki, nimeanza na maelezo hayo kwa kifupi ya huduma ninayofanya, lakini nilitaka kukushirikisha kitu ambacho nimekiona kwa marafiki zangu ambao ni wasomaji na wafuatiliaji wa kazi zangu.
Siku chache zilizopita nilitoa nafasi 10 za watu kufanya kazi na mimi moja kwa moja katika kukuza biashara zao kwa kipindi cha mwaka mzima. Ni wazo ambalo nimekuwa nalo kwa muda mrefu na nimekuwa nalifanya kwa hatua za mtu mmoja mmoja lakini siyo kwa kikundi, kwa sababu kwa kikundi inahitaji kazi zaidi.
Basi nikaweka mpango kwamba baada ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, nitatoa nafasi 10 za watu tutakaofanya kazi pamoja kwa kipindi cha mwaka mzima. Kilichonishangaza, japo sikusema watu wawahi nafasi hizo, maana nilisema maelekezo zaidi nitayatoa siku ya semina, watu wengi sana walikuwa tayari kupata nafasi hizi.
Yaani kabla hata ya siku kuisha, nafasi kumi nilizotoa zilikuwa zimeshajaa kwa watu ambao walinipigia simu na kunitumia ujumbe kwamba wanahitaji sana kupata nafasi hiyo.
Hii inaonesha ni jinsi gani watu wana kiu kubwa ya mafanikio, hii inaonesha jinsi ambavyo watu wameshaona kikwazo kikubwa kwao ni kipi na kuwa tayari kukivuka kwa namna yoyote ile.
Huu ni moja ya ujumbe niliopokea kutoka kwa msomaji mwenzetu;
Habari za asubuhi Kocha,,
Naomba kuwa mmoja Wa watu10 ambao nitakuwa kwenye programu ya mwaka mzima Huu na si mwaka mzima tu ila Kwa maisha yangu, maana Nina program ya 2018-2028 yaani miaka 10 ya kufanya kazi Kwa umakini na ufanisi pia kufikia Uhuru Wa kifedha Kwa ujumla hivyo naomba niwe Wa kwanza katika hao watu 10 na niyajitahidi niondoke dar tarehe 5 badala ya tarehe 4/11/2018 Kwa ajili ya maelekezo ya hiyo program
Wako, F. B.
Rafiki, nimekuandikia hili kukutaarifu mambo mawili makubwa sana, ambayo sitaki kabisa uyakose, kwa sababu nimejitoa sana kuhakikisha wewe unafanikiwa mno, kwa sababu najua bila wewe kufanikiwa, mimi siwezi kufanikiwa.
Jambo la kwanza ni je umeshajitoa kwa asilimia 100 kwa ajili ya mafanikio yako? Je umeshajiandaa kupambana na chochote kinachoweza kukuzia usifanikiwe? Na je ungependa kufanya kazi na timu ndogo ya wale ambao wanaelekea kule unakoelekea? Kama majibu ni ndiyo, basi hakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, maelezo zaidi yako hapo chini.
Jambo la pili ninaongeza nafasi mbili katika nafasi zile 10 nilizotoa awali. Hivyo badala ya nafasi 10, sasa zitakuwa nafasi 12 za timu ya watu tutakaofanya kazi kwa pamoja kuweza kukuza zaidi biashara zetu na hata kufanikiwa zaidi kwa mwaka 2018/2019. Hivyo nina imani hutakosa nafasi hii, kama kweli umejitoa na kama upo tayari kufanikiwa. Nitaweza kufanya kazi na watu 12 tu, kwa sababu ninaamini kwenye kundi dogo la watu waliojitoa hasa, hakuna kinachoshindikana. Hivyo usikose nafasi hii.
Rafiki, kupata nafasi hizi, pamoja na maelekezo mengine kuhusu programu hii, nitatoa siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni tarehe 03/11/2018.
KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.
Rafiki, tarehe 03/11/2018 ndiyo siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina hii itafanyika kwenye moja ya hoteli zilizopo jijini dar es salaam.
Itakuwa ni semina ya siku nzima, kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni. Yatakuwa ni masaa 12 ya kujifunza, kujuana na wengine, kuhamasika na kuweka mkakati wa kwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
Ada ya kushiriki semina hii ni tshs 100,000/= (laki moja) ada ambayo itajumuisha huduma zote za siku ya semina, kuanzia chai, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandikia na kalamu.
Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kulipa ada yako kabla ya tarehe 31/10/2018, ambayo ndiyo tarehe ya mwisho ya kulipia ada.
Pia nafasi za kushiriki semina hii ni 100 pekee, na zilizobaki ni chache sana. hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii, lipa ada yako mapema ili tuweze kuwa pamoja kwenye semina hii.
Nakusubiri kwa hamu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, kwa sababu yapo mengi mazuri nimekuandalia kwa mafanikio yako kwa mwaka 2018/2019.
Namba za kufanya malipo ili kushiriki semina hii ni MPESA- 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY – 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukituma fedha tuma na ujumbe wa kueleza umefanya malipo ya semina, ukiambatana na jina lako na namba yako ya simu kwa ajili ya kupewa taarifa zaidi za semina.
Rafiki yangu mpendwa, nimalize kwa kusema kwamba, nina imani kubwa utakuwa mmoja wa wale wachache 12 tutakaofanya kazi pamoja kwa miezi 12 ijayo. Hivyo utakamilisha malipo ya ada na kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018. Fanya hivyo na kwa umoja wetu, na nguvu ya wachache waliojitoa, ikusaidie kufanikiwa zaidi.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL