Mpendwa rafiki yangu,
Changamotozo katika maisha hazitakoma, bali zitaendelea kuwepo kila siku ya maisha yako. Maisha yasingekuwa na changamoto yangekuwa hayana maana kuishi ila maisha yanakuwa yana nidhamu kwa sababu ya changamoto.
Hatuwezi kuwa bora bila changamoto, tunakuwa imara pale tunakabiliana na changamoto ndiyo maana mpaka ukimwona mtu ametangazwa mshindi wa kitu fulani basi ujue huyo kuna changamoto ameweza kuzivuka ndiyo maana anapongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuzishinda changamoto.
Kila mtu kuna eneo ambalo anaweza kusaidia mtu mwingine hivyo hakuna mtu ambaye hawezi kwa kila kitu. usijione huwezi kwa sababu ya changamoto fulani bali jione unaweza kwa uwezo wa asili ulionao ndani yako, kumbe basi, maisha ni changamoto zisizoisha na chukulia maisha ni kama vile tumbo ukila sasa unaweza kusema hutokuja kula tena lakini baada ya muda utahisi njaa tena hivyo ulazimika kula ndivyo ilivyo kwa changamoto hata ukitatua sasa itakuja tena nyingine kwa namna ya tofauti.
Tumezaliwa kupambana na kushinda na siyo kukimbia yale magumu. Ukuu wowote duniani unapatikana katika magumu ambayo watu wengi wanayakimbia lakini wachache wenye ujasiri wanaamua kukaa chini na kuyatekeleza.
Uzuri mkubwa wa changamoto ni kwamba hakuna changamoto inayodumu milele. Changamoto zote tunazokutana nazo zipo tu kwa muda lakini hakuna changamito itakayodumu milele yote hapa duniani. Zinakuja kwa muda zinatupa funzo fulani halafu zinaondoka lakini zitakuja tena kwa mtindo mwingine.
Hebu tu jitafakari hapo mwanzo ulipokuwa mdogo ulikuwa huwezi kuongea vizuri kuna misamiati ilikuwa ni changamoto kwako kutamka lakini kwa sasa hiyo changamoto haipo tena na kama kuongea unaongea vizuri tu bila hata kufikiria yaani fluent.
Hatua ya kuchukua leo, usichukulie matatizo kama kitu hasi kwa bali yapokee na jifunze kitu. kaa chini na andika ulichojifunza halafu chukua hatua mara moja.
Hivyo basi, habari njema ni kwamba uko hai kwa sababu umekuwa ni jasiri wa kupambana na changamoto za dunia. Hivyo sherekea ushindi huo huku ukipambana kuweka juhudi za kuwa bora zaidi.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti hii hapa www.mtaalamu.net/kessydeo .
Asante sana na karibu sana!