“The advice we give others is the advice that we ourselves need.”
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USHAURI UNAOWAPA WENGINE, NI USHAURI UNAOUHITAJI WEWE…
Huwa ni rahisi sana kuwashauri wengine kwenye mambo mbalimbali kwenye maisha yao.
Lakini kwa hakika, ushauri wowote unaoutoa kwa wengine, ni ushauri ambao wewe mwenyewe unauhitaji sana.
Chochote ambacho unafikiri wengine wanapaswa kufanya, ndiyo ambacho wewe mwenyewe unapaswa kufanya.
Hata katika ukosoaji au ulalamikaji,
Chochote amnacho unakosoa kwa wengine, au kulalamikia kwa wengine ndiyo ambacho wewe mwenyewe unapaswa kukifanyia kazi kwenye maisha yako.
Huwa ni rahisi kwetu kurusha matatizo yetu kwa wengine, lakini kama tutakaa chini na kuyatatua matatizo hayo, tutakuwa bora sisi wenyewe.
Kila unapotoa ushauri kwa mtu mwingine, jiulize kama wewe mwenyewe unatekeleza hicho unachoshauri, na kama siyo anza kukitekeleza kwenye maisha yako.
Kama kuna kitu unalalamikia au kukosoa kwa wengine, anza kujiangalia kwanza wewe mwenyewe kama huna au hufanyi vitu vya aina hiyo, utajikuta wewe mwenyewe upo mshari wa mbele kufanya vile unavyokosoa na kulalamikia kwa wengine.
Kama utaweka juhudi kwenye kuishi ushauri unaotoa kwa wengine, na kukazana kuyaboresha maisha yako kuliko kukosoa na kulalamikia wengine, utaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Chochote unachotoa kwa wengine, hebu anza kukifanyia kazi kwako wewe mwenyewe kwanza, na maisha yako yatakuwa tofauti.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanyia kazi ushauri unaoutoa kwa wengine, na kufanyia marekebisho kwako yale unayokosoa kwa wengine.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha
Ni kweli usemayo kocha, uwe na siku njema .
LikeLike
Karibu sana
LikeLike