Rafiki yangu mpendwa,

Aliyekuwa raisi wa 16 wa taifa la Marekani, Abraham Lincolin amewahi kunukuliwa akisema; “That some should be rich shows that others may become rich, and hence is just encouragement to industry and enterprise.”

Akimaanisha kwamba wachache wanapaswa kuwa matajiri ili wengine wajifunze kwamba inawezekana na wao kuwa matajiri pia. Na hili linaleta faraja kwenye kazi na hata biashara.

Huu ni msingi muhimu sana ambao kama kila mtu akiweza kuutumia kwenye maisha yake ataweza kupata mafanikio makubwa sana.

Kwamba mafanikio ni kitu ambacho kinaweza kuigwa, kama umewahi kumwona mtu tajiri, basi kwa hakika na wewe unaweza kuwa tajiri.

Ni kupitia kauli hii ya Lincolin pamoja na wanamafanikio wengine tunakwenda kujifunza kwenye semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

dc2a0-fedha2bmkopo

Kupitia semina hii, tunakwenda kujifunza tabia kumi ambazo matajiri wote wanazo na zimewawezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.

Hii ina maana kwamba, kama mtu atazielewa tabia hizo, na kuziweka kwenye maisha yake ya kila siku, basi utajiri kwake itakuwa siyo swala la kujiuliza kama ataupata au la, bali litakuwa swala la kusubiri lini kuupata, maana kuupata ni hakika.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha na kukukumbusha kuhusu semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI.

Semina ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote.

Semina hii itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019 zitakuwa siku kumi za kupata nondo kumi za moto ambazo nitaweka msingi muhimu sana wa mafanikio makubwa na utajiri kwenye maisha yako.

Kuna njia mbili za kuweza kushiriki semina hii;

Njia ya kwanza ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama tayari wewe ni mwanachama moja kwa moja unapata nafasi ya kushiriki semina hii. Na kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga sasa kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=) na kupata nafasi ya kushiriki semina pamoja na kuendelea kupata mafunzo mengine kwa kipindi cha mwaka mzima.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu la semina hii, hili ni kundi kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kwa sasa hawawezi kulipa ada na kujiunga. Hawa watapata nafasi ya kushiriki semina hii kwa kulipia tsh elfu 20 pekee (20,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kupata mafunzo haya ya semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Ili kufanya malipo ya kushiriki semina, iwe ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au kujiunga na kundi maalumu, lipa ada yako kwa namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap namba 0717396253.

Kama kuna zawadi moja unayoweza kujipa kwa mwaka 2019 ambayo miaka mingi ijayo utajishukuru sana, basi ni wewe kushiriki semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI.

Kamilisha malipo yako leo ili uweze kupata nafasi hii ya kipekee sana ya kupata maarifa sahihi ya kujijengea tabia sahihi zitakazokufikisha kwenye utajiri na mafanikio makubwa.

Rafiki yangu, nakusisitiza tena, usipange kukosa semina hii, nimekupa kila njia ambayo itakuwa rahisi kwako kushiriki semina hii, ni wewe tu kuitumia.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge