Rafiki yangu mpendwa, kila mtu anapenda kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yake, kila mtu anapenda utajiri. Lakini ni wachache sana wanaofuata kanuni na misingi sahihi ya kupata fedha. Wengi huwa wanafikiri fedha zinaweza kujitokeza tu, wanaweza kulala masikini na kuamka matajiri.

Na ndiyo maana unaona michezo ya kubahatisha na kamari zinazidi kushika chati na kupata umaarufu kila siku. Imefika mahali watu wanaamini kupata fedha ni kitu cha bahati. Misingi imesahaulika kabisa na watu wanakimbizana na bahati.

Sasa kwa kuwa nakupenda sana rafiki yangu, na sitaki ukimbizane na bahati ambazo hazitakuwezesha kufikia uhuru wa kifedha, leo nimekuandalia makala nzuri yenye kanuni rahisi sana ambayo kama utaifuata kila siku itakuwezesha kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yako.

Kanuni hiyo ni hii;

MALENGO YENYE NGUVU + TABIA NZURI + IMANI CHANYA + LUGHA CHANYA = UHURU WA KIFEDHA.

kanuni kuu ya utajiri

Kanuni hii ina vipengele vinne tu ambavyo kila mtu anaweza kuvifuata na akaweza kufikia uhuru wa kifedha. Kwa kifupi nakwenda kukuelezea kuhusu kila kipengele.

MALENGO YENYE NGUVU.

Malengo ndiyo eneo la kwanza kwenye kufikia uhuru wa kifedha, lazima uwe na kitu unacholenga, lazima uwe na kitu unachofanyia kazi.

Anza kwa lengo la kiasi gani cha fedha unachotaka kufikia, na lengo liwe halisi na linalopimika. Usiseme tu nataka fedha nyingi, bali weka kabisa kiasi cha fedha unachotaka kupata. Pia weka muda wa kupata kiasi hicho na kuwa na njia za kujipima.

Malengo yenye nguvu ndiyo yatakayokusukuma ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha kwa muda uliojiwekea.

TABIA NZURI.

Tabia zako ndizo zinazokujenga au kukubomoa. Na kwa upande wa fedha, zipo tabia ambazo zinajenga utajiri (TABIA ZA KITAJIRI) na zipo tabia ambazo zinajenga umasikini.

Ili kufikia uhuru wa kifedha na utajiri, unapaswa kujijengea tabia za kitajiri na kuziishi kila siku.

Nimekuandalia semina ya kujifunza tabia 10 za kitajiri ambazo ukiziishi kila siku utafikia uhuru wa kifedha na utajiri. Maelezo zaidi kuhusu semina hii yapo hapo chini.

IMANI CHANYA.

Kiwango cha fedha unachokuwa nacho kwenye maisha yako ni matokeo ya imani uliyonayo. Kwa kifupi huwezi kupata fedha zaidi ya kile kiasi ambacho unafikiri unaweza kupata au unastahili kupata.

Kama una imani hasi juu ya fedha, kwamba fedha ni mbaya au fedha ni nguvu basi huo ndiyo utakaokuwa uhalisia wako.

Ili kufikia uhuru wa kifedha, unapaswa kuwa na imani chanya juu yako na juu ya fedha. Jua kwamba fedha ni nzuri na unao uwezo wa kupata fedha kwa namna unavyotaka wewe. Pia amini kwamba fedha siyo ngumu, bali ni matokeo ya mabadilishano ya thamani, kwamba unapotoa thamani zaidi unapata fedha zaidi.

LUGHA CHANYA.

Lugha unayotumia pia ina athari kubwa kwenye maisha yako. Na kwa upande wa fedha, unapaswa kuwa makini sana na lugha unazotumia, hasa zile ambazo zimezoeleka kwenye jamii.

Mfano watu wengi wamekuwa na lugha hasi kuhusu fedha kwenye jamii, lugha kama vyuma vimekaza, fedha imepotea, nyakati ni ngumu na uchumi ni mbaya, zinaweza kuwa zinatumika sana kwenye jamii. Lakini wewe usitumie lugha hizi.

Mara zote tumia lugha chanya linapokuja swala la fedha, hata kama mambo ni magumu kiasi gani, usikiri ugumu. Badala yake ona fursa zinazopatikana kwenye kila ugumu. Kwa mfano hata kama fedha ni ngumu kiasi gani, bado watu wanakula, bado wanavaa, bado wanaendesha magari, bado wanajenga na kadhalika. Hivyo ukijiweka upande chanya, utaona njia bora za kuwahudumia watu na kutengeneza kipato.

Rafiki, hivyo ndiyo vipengele vinne vya kanuni rahisi ya kukuwezesha kufikia uhuru wa kifedha. Ishi vipengele hivi kwenye kila siku ya maisha yako na hakuna kitakachoweza kukuzuia kufikia uhuru wa kifedha.

Nimekuahidi kuhusu semina ya TABIA ZA KITAJIRI, na maelezo zaidi kuhusu semina hapo hapo chini;

KARIBU KWENYE SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha na kukukumbusha kuhusu semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Kwenye semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI, utajifunza tabia kumi za kuishi kwenye kila siku ya maisha yako ambazo zitakuwezesha kufikia utajiri na mafanikio makubwa.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote.

Semina hii itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019 zitakuwa siku kumi za kupata nondo kumi za moto ambazo nitaweka msingi muhimu sana wa mafanikio makubwa na utajiri kwenye maisha yako.

Kuna njia mbili za kuweza kushiriki semina hii;

Njia ya kwanza ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama tayari wewe ni mwanachama moja kwa moja unapata nafasi ya kushiriki semina hii. Na kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga sasa kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=) na kupata nafasi ya kushiriki semina pamoja na kuendelea kupata mafunzo mengine kwa kipindi cha mwaka mzima.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu la semina hii, hili ni kundi kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kwa sasa hawawezi kulipa ada na kujiunga. Hawa watapata nafasi ya kushiriki semina hii kwa kulipia tsh elfu 20 pekee (20,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kupata mafunzo haya ya semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Ili kufanya malipo ya kushiriki semina, iwe ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au kujiunga na kundi maalumu, lipa ada yako kwa namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap namba 0717396253.

Kama kuna zawadi moja unayoweza kujipa kwa mwaka 2019 ambayo miaka mingi ijayo utajishukuru sana, basi ni wewe kushiriki semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI.

Pia unaweza kumlipia mtu wa karibu kwako akaweza kujifunza na kuyabadili kabisa maisha yake kwa mwaka 2019. Mlipie tsh elfu 20 ili aweze kuingia kwenye kundi maalumu la semina hii na ajifunze.

Kamilisha malipo yako leo ili uweze kupata nafasi hii ya kipekee sana ya kupata maarifa sahihi ya kujijengea tabia sahihi zitakazokufikisha kwenye utajiri na mafanikio makubwa.

Rafiki yangu, nakusisitiza tena, usipange kukosa semina hii, nimekupa kila njia ambayo itakuwa rahisi kwako kushiriki semina hii, ni wewe tu kuitumia.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge