“Make sure you’re not made ‘Emperor,’ avoid that imperial stain. It can happen to you, so keep yourself simple, good, pure, saintly, plain, a friend of justice, god-fearing, gracious, affectionate, and strong for your proper work. Fight to remain the person that philosophy wished to make you. Revere the gods, and look after each other. Life is short—the fruit of this life is a good character and acts for the common good.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.30
Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu,
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAFANIKIO YASIKUBADILISHE…
Watu wengi wanapokuwa hawajafanikiwa, wanakuwa na tabia nzuri sana. Wanakuwa wanyenyekevu, wanajituma sana na wapo tayari kujifunza kila wakati. Ni tabia hizo ndizo zinazowafanya wafanikiwe sana.
Lakini pale mtu anapofanikiwa, anajiona ameshajua kila kitu, na hapo tabia zinabadilika. Wanakuwa na kiburi na dharau, hawaweki tena juhudi kubwa na wanaona hakuna kipya cha kujifunza, wameshajua kila kitu.
Kubadilika huku kwa tabia ndiyo kunatengeneza anguko la wengi wanaofanikiwa.
Rafiki, kile unachofanya kabla hujafanikiwa na kikakupeleka kwenye mafanikio, ndiyo unapaswa kuendelea kukifanya hata baada ya kufanikiwa, tena kukifanya kwa ubora wa hali ya juu zaidi.
Mafanikio yasikudanganye kwamba wewe umeshaweza sana na hakuna cha kukuangusha.
Mafanikio yasikudanganye kwamba umeshajua kila kitu hivyo hakuna kipya cha kujifunza.
Endelea kuweka juhudi kama vile ndiyo unaanza, endelea kujifunza kama vilw hujui chochote, na hili litakufanya uzidi kufanikiwa zaidi.
Lakini kama mafanikio kidogo yatakufanya ubadilike, hutaweza kupata mafanikio makubwa zaidi.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendelea kuweka juhudi kubwa na kujifunza kama vile ndiyo unaianza safari yako ya mafanikio.
#UsileweMafanikio, #KilaSikuNiMwanzo, #UsileteMazoea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha