“Think of those who, not by fault of inconsistency but by lack of effort, are too unstable to live as they wish, but only live as they have begun.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 2.6b
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNAISHI KAMA UNAVYOTAKA AU KAMA ULIVYOANZA?
Watu wengi wamekuwa wanaendesha maisha yao kwa mazoea.
Wanaishi leo siyo kwa sababu ndivyo walivyooanga na kutaka kuishi, bali kwa sababu ndivyo walivyoishi jana.
Wanafanya kazi siyo kwa sababu wanataka kufanya kazi hiyo, bali kwa sababu ndiyo kitu pekee kinachowaingizia kipato.
Mtu ukishafika kwenye hatua hii, ya kuendesha maisha kwa mazoea badala ya mabadiliko, unakuwa umechagua kuyapoteza maisha yako.
Wangi hawapendi mabadiliko, lakini bila mabadiliko huwezi kupiga hatua na kufanikiwa.
Hivyo ni muhimu sana ukawa mtu wa kujihoji na kijitathmini.
Kila unachofanya kwenye maisha yako jiulize kama UMECHAGUA kufanya au umefanya kwa sababu ndivyo umekuwa unafanya.
Ulianzia wapi na ulianzaje haina maana kubwa sana kama unafanya nini kwa sasa.
Ulifanya nini jana haina maana kubwa leo kama utarudia kile kile cha jana.
Chagua kuishi maisha ya kuchagua kila unachofanya na siyo maisha ya mazoea.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kile ulichochagua kufanya na siyo kufanya kile ulichozoea kufanya.
#MaishaNiKuchagua, #MchaguziMkuuNiWewe #ChaguaKwaUsahihi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1