Rafiki yangu mpendwa,

Watu wengi wanaoingia kwenye biashara ndogo huwa wanaruka hatua moja muhimu sana ambayo huja kuwagharimu mbeleni.

Watu hawa huwa wanakuwa na wazo zuri la biashara, wanapambana kupata mtaji ili kuingia kwenye biashara hiyo.

Wanakuwa na hamasa kubwa ya kuingia kwenye biashara hiyo na wanategemea kupata uhuru mkubwa wa maisha yao kutoka kwenye biashara wanayokwenda kuanzisha.

Kwa hamasa hii kubwa, watu hao wanaingia kwenye biashara, wanaanza biashara wao wenyewe, kwa wao kuwa ndiyo kila kitu kwenye biashara zao.

Kwa hamasa kubwa wanayokuwa nayo wanajituma kweli na hilo linawafanya watoe matokeo mazuri sana kwenye biashara zao. Wateja wao wanaridhika kwa huduma hizo nzuri na kurudi tena pamoja na kuleta wengine.

Hata kipato nacho kinakuwa kizuri kuliko ambavyo mtu alikuwa anapata kabla hajaingia kwenye biashara hiyo.

Ni pale biashara inapoendelea kukua, ndipo mtu anakuja kugundua kosa kubwa alilolifanya mwanzoni.

business trap

Biashara inapozidi kukua mtu anagundua kwamba asipokuwepo yeye biashara haiwezi kwenda. Na hata anapojaribu kuajiri watu, wengi hawawezi kufanya kama anavyofanya yeye.

Hapa ndipo biashara ndogo zinazoanzishwa na wengi hufikia ukomo, hazikui zaidi na nyingi hufa.

Lakini ipo njia nyingine ya kutumia kuingia kwenye biashara ambayo itakuondolea ukomo wa ukuaji na kukupa uhuru zaidi kwenye maisha yako.

Kwa kutumia njia hiyo, kadiri biashara yako inavyokuwa kubwa, ndivyo uhuru wako unakuwa mkubwa pia.

Njia hiyo mbadala ya kuanza biashara ni kutengeneza mfumo wa kuendesha biashara hiyo kabla haijaanza.

Hapa unakaa chini na kutengeneza picha kamili ya jinsi biashara hiyo itakavyoendeshwa na itakavyokuwa.

Unaanza kwa kugawa maeneo muhimu ya biashara hiyo, kisha chini ya kila eneo kuu unaweka vitengo na chini ya hivyo vitengo unaweka majukumu ya kutekelezwa na aliye kwenye kitengo hicho.

Kwa kuwa na mfumo wa aina hii, hata kama upo mwenyewe kwenye biashara, utaweza kuiendesha vizuri. Na unapozidi kukua kibiashara, ukiajiri mtu unamkabidhi kitengo chake na kuwa na njia bora ya kumpima. Hii inapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto za kuajiri kwenye biashara.

Najua swali kubwa unalojiuliza sasa ni utawezaje kutengeneza mfumo kwenye biashara yako.

Na hapa ndipo mimi kocha wako ninapoingia kwenye maisha yako na biashara yako pia.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto hii kubwa ambayo wafanyabiashara wengi wanapitia, ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

NJIA MBILI ZA KUSHIRIKI KWA WASIO WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, kuna njia mbili unazoweza kutumia kushiriki semina hii.

Njia ya kwanza ni kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu kwa ajili ya semina hii. Kama huwezi kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA au kama hutaki kuendelea kujifunza kila siku, unaweza kupata masoko ya semina hii kwa kujiunga na kundi maalumu la semina hii. Kundi hili litakuwa hai wakati wa mafunzo ya semina na baada ya semina kuisha litafungwa. Ili kujiunga kwenye kundi hili maalumu, unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina pekee, ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) na hapo utaweza kuyapata masomo haya mazuri na kuiwezesha biashara yako kufanikiwa sana.

Chagua sasa rafiki yangu utashiriki semina hii kwa njia ipi kati ya hizo mbili, kwa kuwa mwanachama au kujiunga na kundi maalumu. Wito wangu kwako ni usikubali kutokushiriki semina hii, ni kosa ambalo hutajisamehe kwenye maisha yako.

Kwa wale ambao wamechagua kushiriki kwa kundi maalumu, bonyeza kiungo ninachoweka hapa ili kujiunga na kundi maalumu la semina. Kiungo ni hiki; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t kama tayari umeshakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hilo maalumu. Hilo ni kundi kwa wale wanaotaka kushiriki semina pekee na siyo wanachama.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA au KUNDI MAALUMU ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kama siyo mwanachama basi bonyeza kiuongo hiki ujiunge na kundi maalumu la semina hii; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t

Na kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge