Rafiki yangu mpendwa,

Changamoto kubwa sana kwenye biashara imekuwa ni kupata watu sahihi wa kuwaajiri kwenye biashara hiyo, ambao wataiwezesha biashara hiyo kukua.

Upatikanaji wa wafanyakazi sahihi umekuwa mgumu sana. Watu wengi wanataka kazi, lakini hawapo tayari kujituma wakishapata kazi hiyo.

Pia watu wengi siyo waaminifu, wanapopewa kazi huwa wanatafuta njia ya kujinufaisha wao wenyewe kwanza kama kuiba.

Kutokana na changamoto hizi za kuajiri, wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wanakata tamaa na kuona hawawezi kukuza zaidi biashara zao.

Kwani pale wanapojaribu kuajiri na kukutana na changamoto hizo za kuajiri, wanaona ni bora waendelee kufanya biashara zao wenyewe kwa kiwango kidogo kuliko kuzikuza na kusumbuana na watu.

Lakini hiyo siyo hatua sahihi ya kufikia, hupaswi kuacha kukuza biashara yako kwa sababu ukiajiri watu wanakusumbua.

Bali unapaswa kujua kwamba njia unazotumia kuajiri siyo sahihi, ndiyo maana watu unaowapata wanakusumbua.

Zipo njia sahihi za kuajiri ambazo zitakuwezesha kuwapata watu sahihi wa kufanya kazi kwenye biashara yako. Na hata baada ya kuwapata watu hao, zipo njia sahihi za kuwafanya wawe na ufanisi, uzalishaji na tija kwenye biashara hiyo.

Njia bora ya kuongeza ufanisi, uzalishaji na tija ya wale unaowaajiri kwenye biashara yako.

Rafiki, ipo njia moja bora sana ambayo ukiweza kuitumia vizuri utaweza sana kuongeza ufanisi, uzalishaji na tija ya wale ambao umewaajiri kwenye biashara yako.

Kwa kutumia njia hii, wale unaowaajiri hawatakuwa mzigo kwenye biashara yako, badala yake watakua rasilimali muhimu kwenye ukuaji wa biashara hiyo.

Njia hii inawafanya wajitume sana na wazalishe matokeo bora sana kwa biashara yako.

Njia hiyo ni kuwa na MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU.

Position-Agreement

Mara nyingi watu wanapoajiri, huwa wanawapa wafanyakazi wao mkataba wa kazi. Mkataba huo unakuwa unaeleza nafasi ya kazi, majukumu ya kazi, malipo na taratibu nyingine muhimu. Mkataba huo unaeleza wazi kwamba mtu anapokwenda kinyume na mkataba huo basi anakuwa ameuvunja na kujifukuzisha kazi mwenyewe.

Sasa unahitaji kuwa na mkataba wa pili, ambao ni tofauti kidogo na mkataba wa kazi.

Mkataba huu unaorodhesha majukumu ambayo mtu anapaswa kuyatekeleza kwenye kitendo chake cha kazi, unaeleza matokeo ambayo anategemewa kuyazalisha kwenye kazi anazofanya na viwango ambavyo mtu anapaswa kuvikifia katika kutekeleza majukumu yake.

Mtu anasoma na kuelewa vitu hivyo vitatu muhimu vilivyopo kwenye mkataba wa utekelezaji wa majukumu, kisha anaweka sahihi kukubaliana na mkataba huo. Sasa mkataba huu unaeleza wazi kabisa kwamba kama mtu atakwenda kinyume na mkataba huo, basi anakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe. Inakuwa hakuna haja ya kujadiliana nini kimetokea, kama mtu hatatimiza kile alichoahidi kupitia mkataba, hana haja ya kuendelea kuwa kwenye biashara hiyo.

Kwa kuwa na mkataba wa aina hii, unawasukuma sana watu kuweka juhudi na kuzalisha matokeo ambayo yanatarajiwa. Wanahakikisha viwango ambavyo wanategemewa kufikia wanavifikia. Hili linaongeza uzalishaji, ufanisi na tija.

Faida nyingine ua mkataba wa aina hii ni unakusaidia kuchuja na kujua kama mtu uliyempata ni sahihi au la. Kama mtu siyo sahihi utajua haraka sana kwa jinsi atakavyopokea mkataba huo na hata ufanisi wake kwa kumpima kupitia mkataba huo.

Jinsi ya kutengeneza mkataba wa utekelezaji wa majukumu.

Swali muhimu ambalo utakuwa unajiuliza ni jinsi gani unaweza kutengeneza mkataba wa utekelezaji wa majukumu kwenye biashara yako.

Na kabla hujafikiria mkataba huo, unapaswa kwanza kufikiria kitu muhimu zaidi kwenye biashara yako, ambacho ni MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA HIYO.

Ni kupitia mfumo wa kuendesha biashara ndiyo utatengeneza nafasi za kufanyia kazi kwenye biashara hiyo, na kwenye kila nafasi utatengeneza majukumu ya kutekeleza, matokeo yanayotegemewa na viwango vya ufanyaji wa kazi kwenye kitengo husika.

Ukishakuwa na mfumo unaogusa maeneo yote muhimu, hapo sasa unaweza kutengeneza mkataba wa utekelezaji wa majukumu na kuwapa wafanyakazi wako.

Hivyo swali lako la kwanza linapaswa kuwa unawezaje kutengeneza MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YAKO?

Na hapa ndipo ninapokukaribisha kwenye SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto hii kubwa ambayo wafanyabiashara wengi wanapitia, ya kukosa wasaidizi bora kwenye biashara zao na hivyo kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

NJIA MBILI ZA KUSHIRIKI KWA WASIO WANACHAMA WA KISIMA CHA MAARIFA.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, kuna njia mbili unazoweza kutumia kushiriki semina hii.

Njia ya kwanza ni kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu kwa ajili ya semina hii. Kama huwezi kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA au kama hutaki kuendelea kujifunza kila siku, unaweza kupata masoko ya semina hii kwa kujiunga na kundi maalumu la semina hii. Kundi hili litakuwa hai wakati wa mafunzo ya semina na baada ya semina kuisha litafungwa. Ili kujiunga kwenye kundi hili maalumu, unapaswa kulipa ada ya kushiriki semina pekee, ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) na hapo utaweza kuyapata masomo haya mazuri na kuiwezesha biashara yako kufanikiwa sana.

Chagua sasa rafiki yangu utashiriki semina hii kwa njia ipi kati ya hizo mbili, kwa kuwa mwanachama au kujiunga na kundi maalumu. Wito wangu kwako ni usikubali kutokushiriki semina hii, ni kosa ambalo hutajisamehe kwenye maisha yako.

Kwa wale ambao wamechagua kushiriki kwa kundi maalumu, bonyeza kiungo ninachoweka hapa ili kujiunga na kundi maalumu la semina. Kiungo ni hiki; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t kama tayari umeshakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hilo maalumu. Hilo ni kundi kwa wale wanaotaka kushiriki semina pekee na siyo wanachama.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA au KUNDI MAALUMU ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kama siyo mwanachama basi bonyeza kiuongo hiki ujiunge na kundi maalumu la semina hii; https://chat.whatsapp.com/LRtdAqkeDD0BgJXzzoPR6t

Na kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge