Habari rafiki yangu mpendwa?

Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa za semina muhimu tunayokwenda kuwa nayo mwezi julai 2019 ambayo ni semina ya kutengeneza MFUMO WA BIASHARA utakaokupa uhuru mkubwa kwenye biashara yako.

Awali nilitoa njia mbili za kushiriki semina hii, ya kwanza ikiwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ya pili ikiwa ya kundi maalumu la semina hii pekee.

Lakini baadaye niliondoa njia ya kundi maalumu na imebaki njia ya KISIMA CHA MAARIFA pekee.

Watu wengi wameniandikia wakieleza kuhusu mabadiliko hayo yatakavyowaathiri, na hapa nimeandaa makala ya ufafanuzi zaidi na hatua za kuchukua kwa wale ambao hawawezi kulipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa.

Tuanze na maoni ya msomaji mwenzetu aliyeniandikia kuhusu jambo hili;

Habari? Asante kwa email yako hii kuhusu mabadiliko kwenye ushiriki wa semina ya kutengeneza mfumo wa biashara.

Mawazo ya mwanzo ya njia mbili za kushiriki kwenye semina hii ambayo ni kupitia kuwa mwanachama wa kisima cha maarifa (ada Tshs 100,000/=) na kundi maalum (ada Tshs 20,000/=) yalikuwa ni mazuri na uliona mwitikio wake ulikuwa mkubwa.

Sio wengi wenye uwezo wa kulipa hiyo 100,000 ya kujiunga na kisima cha maarifa (kutokana na hali ya kiuchumi) lakini wana uwezo kwa hivi sasa kulipa ile Tshs 20,000 na wanatamani kushiriki semina hiyo (mie mmojawao) ambayo ingewasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye maisha/biashara zao. Kuondolewa hii option ya pili kutawaathiri wengi.

Kwa kuwa naamini lengo lako ni kusaidia watu waweze kutoka kimaisha na watu hao wengi wao hali zao kimaisha hivi sasa ni za kawaida, uangalie upya na urudishe tena ile option ya pili ya kushiriki semina hiyo ya mfumo wa biashara kwa watu kulipia Tshs 20,000 na kuunganishwa na kundi maalum.

Nakutakia kazi njema, kila la heri.

Stephen Mwakasunga.

Kama alivyotuandikia rafiki yetu Stephen hapo, pamoja na wengine wengi walioniandikia, uamuzi wa kuondoa njia ya ushiriki kupitia kundi maalumu umewaathiri watu wengi sana. Hilo lipo wazi kabisa.

productVSservice

KWA NINI NIMEONDOA NJIA YA USHIRIKI WA KUNDI MAALUMU.

Rafiki, kama nilivyoeleza kwenye makala ya mabadiliko ya ushiriki wa semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, nimeondoa njia ya ushiriki wa kundi maalumu kwa sababu nahitaji kuweka juhudi zangu zote kwenye kundi moja na wale wanaoshiriki waweze kuondoka na maarifa sahihi ya kwenda kufanyia kazi.

Iko hivi rafiki, ninapokuwa naandaa semina hizi ambazo nafundisha, mtu wa kwanza kujifunza ni mimi mwenyewe. Yaani mafunzo ambayo nawashirikisha, naanza kuyatumia mimi mwenyewe ili kuwa bora zaidi kwa kila ninachofanya.

Na moja ya vitu nilivyojifunza kuhusu kutengeneza mfumo wa biashara ni kuacha kuhangaika na bidhaa au huduma nyingi kwenye biashara yako, na kuchagua bidhaa au huduma chache ambazo utazifanya kwa ufanisi mkubwa na kuweza kujitofautisha na wengine wote wanaofanya kama unavyofanya wewe.

Baada ya kujitafakari kwa kina, nikagundua hilo ni kosa ambalo nimekuwa nafanya, najihusisha na huduma nyingi sana kiasi kwamba nguvu zangu zinagawanyika kwenye mambo mengi.

Hivyo baada ya kujifunza nimekwenda kuchukua hatua kubwa moja, ya kupunguza huduma ninazotoa na kuwa mbili pekee, UKOCHA na UANDISHI. Hizi ndiyo huduma kuu mbili ambazo nimeona zina msaada kwa wengi, hasa wale ambao nimewakochi kupitia makundi maalumu kama GAME CHANGERS na LEVEL UP. Na pia uandishi ndiyo njia pekee ambayo watu wananijua na kuhitaji huduma zaidi ninazotoa.

Lakini pia kwenye kujifunza kuhusu kuendesha biashara kwa mfumo, nimekutana na dhana kwamba hata kama biashara unayofanya ni ya huduma, unapaswa kuiendesha kama biashara ya bidhaa. Yaani huwezi kutengeneza mfumo bora wa kuendesha biashara kama utaichukulia kama huduma, unapaswa kuigeuza kuwa bidhaa ambayo watu wanainunua kama ilivyo.

Na hapo ndipo nimefanya KISIMA CHA MAARIFA kuwa bidhaa kuu ninayoiuza kwa wale ambao wanahitaji kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao. Na mtu akishaingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ndiyo sasa anaweza kupata huduma nyingine ambazo ni tatu, GAME CHANGERS, LEVEL UP na kushiriki SEMINA.

Bidhaa nyingine ninayotoa ni channel ya TANO ZA JUMA ambapo kila juma mtu anapata uchambuzi wa kina wa vitabu na vitabu vyenyewe.

Na bidhaa ya tatu ni vitabu vya kuchapwa, ambapo kila mwaka nitachapa vitabu viwili.

Vitu hivyo pekee ndiyo nitakavyojihusisha navyo kwa sasa, kundi litakuwa moja pekee la KISIMA CHA MAARIFA na ili kupata huduma za ukocha itabidi kwanza uwe umeshajiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Lakini pia kupitia KISIMA CHA MAARIFA mtu unapata nafasi ya kujiunga na KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambapo watu mnaokaa mkoa mmoja mnakuwa mnakutana kwa pamoja na kushirikiana katika kupiga hatua zaidi.

Huduma nyingine zote ambazo nimekuwa natoa ninazisitisha rasmi ili niweze kuweka nguvu zangu zote kwenye huduma hizo chache na wanaishiriki wanufaike kweli.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA BIASHARA KAMA HUWEZI KULIPA ADA YA KISIMA CHA MAARIFA.

Rafiki, ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa ni tsh laki moja (100,000/=). Hii ni ada kubwa, hilo halina ubishi. Na siyo kila mtu anaweza kumudu ada hii.

Lakini ninaamini kitu kimoja, huu ni kama uwekezaji ambao utaweza kukulipa sana. Kama mtu upo kwenye biashara tayari, hata kama ni ndogo kiasi gani, kuwekeza ndani yako mwenyewe ni hitaji la kwanza ambalo unapaswa ulifanyie kazi.

Kama mtu unapanga kuingia kwenye biashara, kabla hujapeleka mtaji wako kwenye biashara yoyote, itakuwa vyema zaidi kama utaanza kuwekeza ndani yako kwanza.

Hivyo kwa vyovyote vile, kazana ulipe ada ya KISIMA CHA MAARIFA, siyo tu utajifunza semina, lakini kwa mwaka mzima utapata mafunzo na mwongozo sahihi wa mafanikio.

Lakini pia KISIMA CHA MAAARIFA kwa sasa ni bidhaa na siyo huduma. Najua wengi wanaona ugumu wa kulipa ada kwa sababu wanaona ni huduma, ndiyo maana wengine wamekuwa wanaomba walipe kidogo kidogo badala ya kulipa mara moja yote.

Naomba nikuulize swali moja rafiki, kama unasoma hapa najua unatumia simu janja (smartphone) au kompyuta. Najua simu janja unayotumia bei yake siyo chini ya laki moja. Swali ni je ulipoenda dukani kununua simu janja ulimwambia muuzaji akupe halafu utakuwa unamlipa kidogo kidogo? Jibu ni hapana, ulilipia na ukapewa simu janja yako. Ulikuwa tayari kulipia kwa sababu hiyo ni bidhaa.

Kadhalika ndiyo KISIMA CHA MAARIFA kilivyo, ukijiunga leo, utapata mafunzo mengi ya semina zote za nyuma, ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, TABIA ZA KITAJIRI, UKUAJI WA BIASHARA na masomo mengine mengi. Hivyo hii ni bidhaa kama ilivyo simu, lipia mara moja na uipate.

Lakini pamoja na hayo yote tuseme haiwezekani kabisa wewe kulipia ada kwa sasa, na unataka kushiriki semina.

Hapa ushauri wangu kwako rafiki yangu ni huu, kuwa na subira, masomo haya yataendelea kuwepo na hiki ni kitu nimechagua kukifanya kwa maisha yangu yote.

Hivyo kwa sasa fanyia kazi masomo mengi na mazuri yanayopatikana bure kabisa kwenye AMKA MTANZANIA, kisha ukipata matokeo mazuri, njoo ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Semina zote ninazoendesha kwa njia ya mtandao huwa nazihifadhi kwenye blogu ya KISIMA CHA MAARIFA hivyo hata kama utajiunga mwaka kesho, utayapata mafunzo haya na yatakusaidia sana.

Hivyo nikupe uhakika rafiki, niko na wewe hapa, kama utashindwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa, fanya hilo kuwa lengo lako kuu, weka juhudi kwenye shughuli zako, ongeza kipato chako na jiunge. Maarifa yote utayapata, hakuna utakachokosa.

Nikutakie kila la kheri rafiki yangu, na nikukaribishe sana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, uwekezaji ambao utakuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako. Najua kama mtu una nia ya kweli ya kupiga hatua, basi utatafuta kila njia ya kuweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na kupata maarifa haya sahihi.

Nitaendelea kukupa mafunzo mengi na bora kabisa bure kupitia AMKA MTANZANIA na mfumo wetu wa email, lakini pale utakapohitaji zaidi, utapaswa kwanza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na hapo ndipo mengine yataendelea.

Kwa wale ambao hawajapata taarifa za semina, nitaweka maelezo hapo chini;

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto kubwa ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia, hasa ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, unapaswa kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, kwa sababu najua utaondoka na mengi ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Usipange kukosa semina hii.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge