“But there is no reason to live and no limit to our miseries if we let our fears predominate.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 13.12b

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi mpya na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KITU PEKEE CHA KUHOFIA…
Kitu pekee unachopaswa kuhofia kwenye maisha yako ni hofu yenyewe.
Kwa sababu hofu imekuwa inatunyima uhuru na amani, huku kitu tunachohofia kisitokee kabisa.
Hofu isipodhibitiwa, maisha hayawezi kuwa bora.

Hakuna sababu ya kuishi kama huwezi kudhibiti hofu.
Hakuna ukomo kwenye matatizo yako kama utaiachia hofu itawale itakavyo.
Hofu siyo kitu halisi, bali fikra ambazo wewe mwenyewe unakuwa umejijengea juu ya kitu.
Hivyo udhibiti wa hofu uko ndani yako kwa asilimia 100.
Ni wewe kuchukua hatua sasa.

Anza kupambana na hofu na kuiangusha kwenye maisha yako.
Utakuwa na ujasiri wa kujaribu mengi,
Utakuwa na utayari wa kupiga hatua zaidi,
Kama utaweza kuikabili hofu yoyote inayokuzuia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuhakikisha kila hofu uliyonayo unaivunja kabisa kwa kufanya kile ambacho unahofia kufanya.
#ChaKuhofiaNiHofu #DawaYaHofuNiKufanya #HofuNiUtumwaWaKujitakia

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1