Kila kitu kina ugumu ndani yake,
Hata kama kwa nje vitu vinaonekana rahisi kiasi gani, jua kwa ndani mambo siyo rahisi kihivyo.
Hata kama watu wanakushawishi kwamba mambo ni rahisi, usiingie kirahisi kwenye ushawishi wao.
Jambo lolote lenye manufaa na maslahi mapana kwa wengi, lina ugumu ndani yake.
Jambo lolote ambalo unaona wengine wamefanya na kufanikiwa, jua kuna magumu mengi wamepitia mpaka kufika pale.
Tusitegemee kwetu itakuwa rahisi, na pale tunapokutana na urahisi unaotushawishi tutafika kule tunataka kufika, tunapaswa kuwa na wasiwasi.
Hili linakwenda kwa watu pia, watu siyo rahisi kama wanavyoonekana kwa nje. Watu wana changamoto zao, na utazijua baada ya kuanza kujihusisha nao. Unaweza kumwona mtu ni mzuri sana anapokuomba kazi, lakini unapompa kazi ndiyo unagundua kwamba siyo mzuri kama ulivyoshawishika awali.
Kwa kujikumbusha kwamba mambo siyo rahisi, unajiweka kwenye nafasi ya kuwa na maandalizi bora na kuwa tayari kuyapokea magumu hayo yanapokuja, kwa sababu yatakuja, ni swala la muda tu.
Na kama unachotaka wewe ni urahisi, basi usikazane kupiga hatua yoyote kwenye maisha yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Hakika Coarch!
Mambo sio rahisi kihivyo….
Mambo yite yanaugumu ndani yake
LikeLike
Karibu Ernest.
LikeLike