Kinachofanya wewe uwe na ndoa bora au ya hovyo ni kitu kimoja tu na hicho ndiyo kinapelekea wewe kuona ndoa yako ni bora au ya hovyo. Na kitu hicho siyo kitu kingine bali ni mitazamo uliyonayo juu ya ndoa yako.

Je una mtazamo gani kwenye ndoa yako? hakuna ndoa mbaya wala nzuri bali mitazamo yetu ndiyo inatafsiri ndoa zetu ni za namna gani. Ukiwa na mtazamo chanya basi utaweza kuiona ndoa yako ni nzuri vivyo hivyo kwa yule mwenye mtazamo hasi naye ataona mambo ni magumu.

Katika makala yetu ya leo tunakwenda kujifunza maamuzi muhimu wanayotakiwa kufanya wanandoa. Maamuzi hayo muhimu ni wanandoa kuamua ni ndoa ya namna gani wanayotaka kuwa nayo au ni maisha ya namna gani wanayotaka kuishi.

Hakuna mtu atakayeweza kuwaamulia ndoa yenu iweje bali nyie wenyewe mnatakiwa kufanya maamuzi ni ndoa ya aina gani mnataka. Usipoweza kufanya maamuzi ya kuamua hakuna kitu chochote kitakachoweza kubadilika.

Maamuzi ya wanandoa ndiyo yanaweza kuleta ndoa wanayotaka lakini kama wanandoa hawajatulia na kuamua wataendelea kuishi maisha ya ajabu ambayo wameyachagua.

Wanandoa wanayo nafasi ya kufanya maamuzi ya kuamua ndoa wanayotaka wao wenyewe.  Watu wengi hufikiri kwamba katika ndoa  watakutana na mazuri pekee, hapana hata kiapo cha ndoa kinasema kuwa mtavumiliana  katika shida na raha hivyo hakuna sehemu ambayo ni rahisi na salama kila sehemu inahitaji ulipie gharama zake.

SOMA; Saikolojia Ya Kuchepuka; Sababu Halisi Za Watu Kuchepuka Kwenye Mahusiano Na Hatua Za Kuchukua Pale Mwenzako Anapochepuka.

Maisha mazuri au mabaya yanatokana na maamuzi yetu wenyewe, unapofanya maamuzi ndiyo unakuwa unakata shauri, unaamua sasa wewe utakua mtu wa namna  gani na hivyo kuamua kujitoa sadaka kadiri ya maamuzi ambayo mtu ameamua kuyachagua.

Hatua ya kuchukua leo; kila mwanandoa ni mlinzi wa ndoa yake, hivyo kila mmoja anaalikwa kufanya maamuzi sahihi ya kulinda ndoa yake.

Kwahiyo, wanandoa ndiyo wenyewe ndiyo wenye nguvu ya kuamua ni ndoa  au maisha ya ndoa ya namna gani wanataka kuishi. Hivyo kama wewe ni mwandoa fanya maauzi sasa je maamuzi uliyofanya juu ya ndoa yako unayafurahia? Kama kuna maamuzi uliyofanya hayakupi kile unachotaka kaeni chini na amueni maisha mnayotaka kuishi kwani nyie ndiyo waamuzi wa mwisho.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl. Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com //kessydeoblog@gmail.com

Asante sana