Rafiki yangu mpendwa,

Kuna changamoto moja kubwa nimekuwa naiona kwa watu wanaopata huduma za ukocha kutoka kwangu.

Wakati wanapokuwa kwenye huduma ya ukocha, wanapata msukumo mkubwa sana wa kuchukua hatua kila siku na wanapata matokeo mazuri sana.

Lakini wanapotoka kwenye huduma hizi za ukocha, ule msukumo unapungua taratibu mpaka kufika mahali kwamba hawawezi tena kuchukua hatua.

Sote tunajua ya kwamba mafanikio hayaji kama ajali au muujiza, bali ni matokeo ya kufanya kila siku kile ambacho umepanga kufanya ili ufanikiwe.

Swali ni je unawezaje kupata msukumo usioisha ambao utakusukuma kila siku?

Kama unavyonijua mimi rafiki yako, kila wakati naangalia ni kwa namna gani bora naweza kutumia uwezo, ujuzi na uzoefu wangu kukusaidia wewe kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwa sababu naamini wewe ukifanikiwa basi na mimi lazima nitafanikiwa.

Baada ya kuona changamoto hii kwa wengi, nimekuandalia programu mpya inayoitwa DAILY COACHING PROGRAMU.

Hii ni programu mpya ya ukocha ambayo inakupa msukumo wa kuchukua hatua kila siku ili kufikia mafanikio makubwa. Programu hii hairuhusu sababu yoyote ile, bali matokeo.

Karibu upate maelezo kamili kuhusu programu hii na hatua za kuchukua ili kujiunga na uanze kunufaika mara moja.

TO DO LIST.jpg

DAILY COACHING PROGAMU; Kufanya Kila Siku Ndiyo Njia Pekee Ya Kufanikiwa.

Programu mpya ya kujijengea nidhamu ya kufanya kitu kila siku bila kuacha.

Unajiunga na kundi maalumu la wasap na kueleza ni kitu gani utakuwa unafanya kila siku na ushahidi utakaotuma kama umefanya kitu hicho kama ulivyopanga.

MSINGI MKUU.

Msingi mkuu wa programu hii ni kufanya kila siku kile ambacho umepanga kufanya, bila kuacha, hakuna sababu yoyote ile itakayopokelewa kwa nini hujafanya.

Kama upo kwenye eneo ambalo halina mtandao kabisa, utawasiliana na kocha kwa mawasiliano ya kawaida kuonesha kwamba umefanya.

Ukishindwa siku moja utapaswa kulipa faini.

Ukishindwa siku mbili mfululizo utapaswa kulipa faini ya siku mbili.

Ukishindwa siku tatu mfululizo unaondolewa kwenye programu.

Ukishaondolewa, utaweza kujiunga tena kwa kulipa ada ya adhabu na kisha kuendelea kulipa ada ya kawaida.

GHARAMA ZA PROGRAMU HII.

Gharama za kushiriki programu hii ni ada ya tsh elfu moja (1,000/=) ambayo utapaswa kuilipa kila siku.

Huwezi kulipa kwa wiki, mwezi au mwaka, bali utalipa kila siku kama unavyofanya ulichoahidi kila siku.

Faini ya kushindwa siku moja ni tsh elfu 5 (5,000/=), faini ya kushindwa siku mbili ni tsh elfu 10 (10,000/=)

Ukiondolewa, ili kujiunga tena utapaswa kulipa faini ya tsh elfu 30 (30,000/=)

Lengo ni wewe uheshimu kile ulichopanga, ukifanye na uoneshe ushahidi kwamba umefanya, hivyo faini inakusukuma usiruhusu sababu.

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA KILA SIKU KWA MSUKUMO WA PROGRAMU HII.

Kuna mambo mengi unayoweza kufanya kila siku kwa msukumo wa programu hii, baadhi ni;

 1. Kuamka mapema kila siku.
 2. Kuandika.
 3. Kusoma vitabu.
 4. Kufanya mazoezi.
 5. Kufuatilia namba za biashara yako.
 6. Kutekeleza mipango mbalimbali ya biashara yako, kama masoko kwa kutembelea au kuwasiliana na wateja, mauzo na kadhalika.
 7. Kupata muda wa kuwa peke yako, kutafakari na kutahajudi.
 8. Kupata muda wa kuwa na wale wa muhimu kwako, mwenza, familia n.k
 9. Kufanya maandalizi ya mambo ya baadaye, mfano masomo n.k
 10. Kuweka akiba na kuwekeza.
 11. Kuziishi TABIA ZA KITAJIRI tulizojifunza.
 12. Kujenga tabia mpya au kuvunja tabia ya zamani.
 13. Kushirikisha TO DO LIST yako asubuhi na kutoa mrejesho wa utekelezaji jioni.
 14. Mpango mwingine unaoweza kuwa umejiwekea mwenyewe.

MANUFAA YA ZIADA UTAKAYOYAPATA KWA KUWA KWENYE PROGRAMU HII.

 1. Utapata nukuu za kuianza siku kwa hamasa na msukumo mkubwa (HAMASA YA LEO) kila siku saa kumi alfajiri.
 2. Utapata nafasi ya kuomba ushauri wa namna bora ya kutekeleza mipango yako ya kila siku.

KUJIUNGA NA DAILY COACHING PROGRAM.

Fuata hatua hizi kujiunga na programu ya DAILY COACHING.

 1. Fungua kiungo hiki kisha jiunge na kundi la wasap. Kiungo; https://chat.whatsapp.com/GcL2GpPBAAb7BTdJIxSuZs
 2. Ukishajiunga tuma utambulisho wako na kile unachokwenda kufanyia kazi kila siku na ushahidi utakaotoa.

Mfano; Majina yangu ni Emanuel John, kila siku nitakuwa naandika na nitatuma hapa ushahidi wa makala au picha (screenshot) ya maneno niliyoandika kwa siku.

Mfano; Majina yangu ni Issa Juma, kila siku nitakuwa naamka saa kumi alfajiri na nitapost hapa muda ambao nimeamka na kuripoti kile nilichofanya kwa muda niliowahi kuamka ili nisirudi kulala.

 1. Baada ya kujiunga, siku inayofuata unaanza kutuma ushahidi wa kile unachofanyia kazi kila siku.
 2. Ada unalipa kila siku kwenda namba 0717 396 253 au 0755 953 887 majina Amani Makirita.

Karibu sana ujiunge na programu hii ya DAILY COACHING na kila siku upate msukumo wa kuchukua hatua ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Fungua sasa https://chat.whatsapp.com/GcL2GpPBAAb7BTdJIxSuZs na jiunge kisha ahidi nini utafanya kila siku na anza kutekeleza.

Mafanikio makubwa ni matokeo ya hatua ndogo ndogo ambazo mtu anachukua kila siku bila kuacha. Karibu kwenye programu hii itakayokuwezesha kuchukua hatua hizo kila siku.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania