Rafiki yangu mpendwa,

Jukumu lako kubwa na la kwanza kwenye maisha ni kuhakikisha kila siku unakuwa bora kuliko siku iliyopita.

kama kuna mtu mmoja unayepaswa kushindana naye kwenye maisha yako, basi ni wewe mwenyewe, kwa kuhakikisha kila siku mpya unakuwa bora kuliko siku iliyopita.

Na njia rahisi kabisa ya wewe kuwa bora zaidi kila siku ni kupitia usomaji wa vitabu. Kwa kusoma vitabu unajifunza vitu ambavyo mwandishi ametumia muda mwingi kuvitafiti au kupata uzoefu wake.

Kama hakuna kitu kipya unachojifunza na ukachukua hatua mpya baada ya kujifunza, huwezi kupiga hatua kwenye maisha yako, siku zote utaendelea kubaki pale ulipo sasa.

Ni kutokana na umuhimu huu mkubwa wa kujifunza, ndiyo maana nimechagua kukupa zawadi ya vitabu nane vya maendeleo binafsi na mafanikio kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla.

Kwa nini zawadi?

Rafiki, unaweza kuwa unajiuliza kwa nini nakupa zawadi hii.

Natoa zawadi hii kwa sababu naona watu wengi wamekwama sana kwenye kipindi tunachopitia sasa kama dunia.

Kutokana na mlipuko wa vizuri vya Corona unaoendelea duniani na hapa nchini kwetu, vitu vingi vimebadilika na hata mzunguko wa kazi na biashara umepungua sana.

Hivyo watu wamejikuta wana muda mwingi na hawana cha kufanya, hivyo wanatumia muda huo kujijaza hofu katika kufuatilia kila kinachoendelea.

Sasa napenda wewe rafiki yangu upate kitu cha kujaza muda mwingi unaopata sasa, ambacho pia hakitakupa hofu bali matumaini ya kuendelea na mapambano kwa ari kubwa pale hali hii itakapopita.

Sasa kwa kuwa hatujui hali hii itapita lini, hatupaswi kuendelea kupoteza muda zaidi, badala yake tuwekeze muda huu kwenye kujifunza na kuwa bora zaidi.

Zawadi ya vitabu nane.

Rafiki yangu mpendwa,

Zawadi ya vitabu nane ninayokwenda kukupa leo ni katika vitabu ambavyo nimeviandika, kwa lugha rahisi kabisa ya kiswahili ambayo kila mtu anaweza kuisoma na kuielewa.

Lakini pia vitabu hivi vipo kwenye mfumo wa nakala tete, hivyo unaweza kusomea kwenye simu, tablet au kompyuta. Huhitaji kubeba kitabu wala kuwa na bando kila wakati ndiyo usome, badala yake ukishakuwa na kitabu kwenye kifaa chako, unasoma muda wowote bila ya kikwazo chochote.

Unachohitaji ili kupata zawadi hii ya vitabu ni email (barua pepe ambapo utatumiwa vitabu hivi.)

Vitabu nane ninavyokwenda kukupa kama zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu 25 kwa nini unaendelea kuwa masikini.

Kitabu hiki kinakupa sababu 25 zinazokuzuia wewe kutoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri. Kuna mambo mengi umekuwa unafanya kwa mazoea, lakini ni kikwazo kikubwa kwako kupiga hatua. Soma kitabu hiki, yajue mambo hayo 25 na yabadili ili uweze kupiga hatua kwenye maisha yako.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 5 (5,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 3 (3,000/=). Kukipata tuma fedha tsh 3,000/= kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma email yako na jina la kitabu na utatumiwa. Chukua hatua sasa ili usikose zawadi hii, ni kwa muda tu.

vitabu vya elfu 5

  1. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA; Maandalizi na njia bora ya kunufaika na mabadiliko kwenye maisha, kazi na biashara.

Kuna kitu kimoja pekee ambacho huwa hakibadiliki kwenye maisha, kitu hicho ni mabadiliko. Yaani mabadiliko lazima yatokee, iwe unataka au hutaki. Mfano mzuri ni hali tunayopitia sasa, hii inaleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yetu. Sasa kwenye kila mabadiliko kuna makundi matatu ya watu, kundi moja wanafaniwa sana, kundi jingine wanakuwa kawaida na kundi jingine wanaachwa nyuma. Soma kitabu hiki uyajue kwa kina makundi haya na jinsi ya kuwa kwenye kundi linalofanikiwa sana.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 5 (5,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 3 (3,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu. Tuma fedha na ujumbe wenye email yako na jina la kitabu na utatumiwa.

  1. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, Jiajiri na utajirike kupitia mtandao wa intaneti.

Kama kuna kitu kimoja ambacho hali inayoendelea sasa inatufundisha, basi ni uwezo wa kufanyia kazi nyumbani na ukalipwa na wengine. Moja ya njia rahisi za kufanya hivyo ni kuwa na blogu ambayo inakuingizia kipato. Kitabu hiki kinakupa maarifa ya kukuwezesha kuanzisha blogu na kuitumia kuingiza kipato. Ukiwa na blog, unaweza kuiendesha ukiwa popote, hivyo hali kama hii inayoendelea sasa ya watu kuzuiliwa wasiwe na muingiliano sana, haikuathiri kwa kiasi kikubwa. Pata kitabu hiki na uanzishe blogu yako mara moja kwa muda mwingi ulionao sasa na baadaye uweze kuingiza kipato kupitia blogu hiyo.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 10 (10,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 7 (7,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

  1. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma.

Kila siku mpya unayoiona kwenye maisha yako, ni ukurasa mpya kwenye kitabu chako cha maisha. Ukurasa huo ni mtupu, wewe ndiye unayeamua uandike nini kwenye ukurasa huo. Kitabu hiki kinakupa hatua mbalimbali za kuchukua kwenye kila siku ya maisha yako, ili uweze kuwa na maisha bora. Kinakupa msingi mkuu wa mafanikio ambao ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Pata na usome kitabu hiki na kuishi msingi huo ili uwe na maisha bora.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 10 (10,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 7 (7,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

  1. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha na kuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa.

Katika zama hizi, ajira siyo salama kama kipindi cha nyua na pia mshahara umekuwa hautoshelezi kwa sababu ongezeko lake haliendani na ongezeko la gharama za maisha. Lakini wengi wamekuwa wanakwama, hawawezi kuacha ajira zao na kwenda kuanza biashara kwa sababu tayari wanazitegemea ajira hizo. Na hapa ndipo ninaposhauri mtu kuanza biashara akiwa bado ameajiriwa. Kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA kinakupa mwongozo wa jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako huku ukiendelea na ajira yako. Utajifunza jinsi ya kupata wazo bora, kupata mtaji, kupata muda na mengine muhimu. Soma kitabu hiki na uweze kuanza biashara mara moja.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 10 (10,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 7 (7,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

  1. MIMI NI MSHINDI; Ahadi yangu na nafsi yangu.

Hapo ulipo sasa na hatua uliyofikia, ni matokeo ya kile ambacho umekuwa unakijua na kukifikiria kwa siku za nyuma, ambavyo vimekusukuma kuchukua hatua hizi. Kama unataka kupata matokeo bora zaidi siku zijazo, unapaswa kuchukua hatua leo, kwenye kile unachojia, namna unavyofikiri na hatua unazochukua. Kitabu cha MIMI NI MSHINDI, kinakupa mbinu zote za ushindi na kisha unajipa ahadi ya ushindi, na ukichukua hatua kwenye yale unayojifunza, utapata ushindi mkubwa sana, hasa kwa nyakati tunazopitia sasa. Soma kitabu hiki.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 10 (10,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 7 (7,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

vitabu vya elfu 10

  1. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; dhibiti muda wako ili uweze kufanya zaidi.

Mambo mengi na muda ni mchache ni kauli ambayo imekuwa maarufu siku za karibuni. Kila mtu analalamika kwamba hana muda, ndiyo maana wengi hawasomi vitabu au kuchukua hatua za ziada kufanikiwa. Sasa mimi nakuambia hilo siyo sahihi, kila mtu, haijalishi yuko bize kiasi gani, anaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku. Soma kitabu hiki uone jinsi unavyoweza kuokoa muda mwingi kwenye siku yako.  Na kama unajiambia husomi vitabu kwa sababu huna muda, basi hiki ndiyo kitabu cha kuanza nacho.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 5 (5,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 3 (3,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

  1. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki biashara kubwa kwa kuanza na mtaji kidogo.

Moja ya mifumo rahisi na inayomwezesha kila mtu kuingia kwenye biashara ni mfumo wa mtandao (networking) mfumo huu unatumia wale unaowajua kusambaza bidhaa na huduma mbalimbali. Lakini mfumo huu wa biashara umepata sifa mbaya kwa sababu wengi hawaelezwi ukweli kuhusu aina hii ya biashara. Kwenye kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO, unajifunza kwa kina msingi wa biashara hii, jinsi ya kuifanya kwa mafanikio na jinsi ya kuepuka kutapeliwa na makampuni yasiyo sahihi. Soma kitabu hiki na uweze kufanya maamuzi sahihi kwenye biashara hii.

Bei ya kawaida ya kitabu hiki ni tsh elfu 5 (5,000/=) lakini kwa zawadi utakipata kwa tsh elfu 3 (3,000/=). Kukipata fuata maelekezo yaliyotolewa kwenye kitabu cha kwanza hapo juu.

Pata vyote kwa pamoja.

Rafiki, ukijumlisha bei halisi za vitabu hivyo nane unapata shilingi elfu sitini (60,000/=), ukijumlisha bei ya zawadi ya kitabu kimoja kimoja unapata tsh elfu 40 (40,000/=) lakini kama utavichukua vitabu hivyo nane kwa pamoja, kuna zawadi zaidi.

Kama utachukua vitabu vyote nane kwa pamoja, utapata kwa bei ya tsh elfu 30 (30,000/=) hapo unakuwa umeokoa elfu 30 nzima, yaani unavipata vyote kwa nusu ya bei.

Je unasubiri nini rafiki yangu? Chukua hatua sasa ili usikose zawadi hii, kwa sababu ni ya muda tu.

Kupata zawadi hizi, tuma fedha kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 (majina AMANI MAKIRITA) kisha nitumie ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye barua pepe yako pamoja na jina la kitabu, kama umechukua vyote andika zawadi ya vitabu vyote kisha nitakutumia vitabu hivyo kwenye email yako.

MUHIMU; vitabu hivyo vipo kwa mfumo wa softcopy pekee na vinatumwa kwa email tu. Chukua hatua sasa ili kupata zawadi hiyo ya vitabu na uweze kuvuka kipindi hiki ukiwa imara. Zawadi hii ni ya muda mchache, chukua hatua sasa ili usiikose.

Kama unahitaji vitabu vichache kati ya hivyo, unaweza kulipia vile unavyochagua kwa bei zake za zawadi zilizooneshwa hapo juu. Ukatuma fedha na majina ya vitabu unavyotaka kisha ukatumiwa.

NYONGEZA; KITABU CHA TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Rafiki yangu, kwa sababu nakupenda sana, naendelea kukupa zawadi ya maarifa ambayo yatakufanya uendelee kuwa bora sana.

Kitabu cha TANO ZA MAJUMA YA MWAKA, ni kitabu kikubwa ambacho kimesheheni maarifa mengi na bora sana. Kina siri 50 za mafanikio, kina uchambuzi wa vitabu 50 bora kabisa vya mafanikio, makala bora 50, maarifa ya kifedha na tafakari za kufikirisha 50.

KITABU; TANO ZA MAJUMA YA MWAKA

Hiki ni kitabu ambacho utakisoma kwa mwaka mzima, maana ni kikubwa na kina mtiririko mzuri wa usomaji.

Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy) na bei yake ya kawaida ni tsh elfu 50 (50,000/=), lakini nakupa zawadi ya kukipata kitabu hiki kwa tsh elfu 40 (40,000/=).

Kupata zawadi hii ya kitabu, wasiliana na 0678 977 007 au 0752 977 170 mwambie unahitaji zawadi ya kitabu cha TANO ZA MAJUMA YA MWAKA na utapewa utaratibu wa kukipata kwa kule ulipo. Kama upo Dar utalewa ulipo, kama upo mkano utatumiwa kwa basi, ambapo utaongeza nauli ya kutuma.

Rafiki, naamini zawadi hizi zitakusaidia sana katika kipindi hiki tunachopitia, ni kipindi ambacho unahitaji kuwa na msingi mzuri, la sivyo utakata tamaa na kupotea kabisa.

Chukua hatua sasa kupata zawadi kama maelekezo yalivyo hapo juu ili uvuke wakati huu ukiwa salama na imara kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz