“Without great solitude, no serious work is possible.” — Pablo Picasso

Bila ya utulivu, huwezi kufanya kazi ambayo ni bora.
Bila ya kuondokana na kelele na usumbufu mwingine wa akili yako, haiwezi kutulia na kuja na mawazo bora.
Wanasayansi, wanafalsafa, waandishi, wajasiriamali na watu wengine, huwa wanapata mawazo bora pale wanapokuwa kwenye utulivu mkubwa, katika hali ya upweke.

Lakini utulivu kwa sasa imekuwa ni anasa ambayo wachache sana wanaweza kuimudu.
Kelele na usumbufu vimekuwa ndiyo mazingira yetu ya kila wakati.
Na usumbufu mkuu umekuwa unatembea nao kila mahali, na hata ukilala uko nao pembeni, ukiamka unaanza nao.
Usumbufu huo ni simu janja yako.
Simu hiyo inakuwa usumbufu kwako kwa sababu kila mara inakukatisha kwenye kile unachofanya.
Pia inakuwa njia rahisi kwako kutoroka pale mambo yanapokuwa magumu.

Ni wakati wako sasa wa kudai uhuru wako kwenye maisha,
Uhuru wa kupata muda tulivu,
Muda ambao hakuna usumbufu wala kelele.
Kwenye kila siku yako tenga muda ambao utaweka akili yako yote kwenye jambo moja bila kuruhusu usumbufu wowote.
Kwa njia hiyo utaweza kuichochea akili yako ikupe mawazo bora zaidi.

Kama unajiambia huwezi kukaa mbali na simu yako kwa muda,
Basi jua umeshayapoteza maisha yako.
Haijalishi unafanya kazi au biashara ya aina gani,
Unapaswa kupata muda tulivu ambao utautumia kufanya yake makubwa na muhimu.
Tenga muda huo na kuutumia vizuri kila siku.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu hofu na kutishika, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/06/2014

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,