“When you start to lose your temper, remember: there’s nothing manly about rage.” – Marcus Aurelius

Kuna wakati mambo yanatokea, mambo ambayo hukutegemea yatokee na hukuwa umejiandaa nayo.
Kama mambo hayo yanakuangusha au kukukwamisha, unapatwa na hasira.
Ni wakati wa hasira ndiyo unaweza kufanya vitu utakavyovijutia sana kwenye maisha yako.

Hivyo mara zote jichunge unapokuwa na hasira,
Jizuie usifanye maamuzi yoyote na wala usichukue hatua yoyote.
Hakikisha pia hakuna mwingine anayejua kama una hasira.

Wengi wamekuwa wanachukulia hasira kama kitu cha kujisifia,
Wanasema wazi kabisa kwamba wana hasira au kuwaambia watu wasiwakasirishe kwa sababu watafanya vitu vibaya.
Wewe usiwe hivyo,
Jua hakuna sifa au ufahari wowote kwenye hasira.
Badala yake chukulia hasira ni kitu cha aibu, ni udhaifu kwenye fikra na mategemeo yako na hivyo imalize ndani yako bila ya kuleta madhara yoyote nje.

Kila unapopatwa na hasira, kwanza tambua uko kwenye hasira.
Baada ya hapo hakikisha inajidhibiti ili usifanye maamuzi au kuchukua hatua yoyote.
Na mwisho, hakikisha hakuna anayejua wakati gani una hasira au huna.
Ukiweza kufanya haya, hasira haitakuwa tatizo kubwa kwako,
Bali itakuwa ni njia ya kujikumbusha wapi unateleza.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu jinsi ya kutumia maumivu kama mtaji, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/07/2046