Rafiki yangu mpendwa,

Kama ambavyo umekuwa unapata taarifa ninazotuma, mwezi huu wa Oktoba 2020 nimetoa vitabu viwili vipya ambavyo ni UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA na ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kila ninapotoa vitabu, siku za awali huwa navitoa kama zawadi kwa wasomaji ambao wamekuwa na mimi kwa muda mrefu, maana hao nawathamini sana kwenye safari hii ya kushirikishana maarifa sahihi ya kutuwezesha kupiga hatua na kufanikiwa kwenye maisha.

Kwa vitabu hivyo viwili vipya nilivyotoa, vimekuwa vinapatikana kwa bei ya zawadi.

Nipende kukutaarifu wewe rafiki yangu kwamba leo tarehe 30/10/2020 ndiyo mwisho wa zawadi hiyo niliyokuwa nimekuandalia.

Kama bado hujachukua hatua ya kupata zawadi hii, nikusihi uchukue hatua hiyo sasa hivi ili usiikose zawadi. Kwani siku ya leo ikiisha, na zawadi inakuwa imekupita.

Ninakazana kuweka juhudi kubwa kwenye maarifa ninayokushirikisha wewe rafiki yangu ili uweze kupiga hatua. Na mirejesho ambayo mpaka sasa nimeipata kwa vitabu hivi viwili inanipa nguvu kubwa ya kuendelea.

Bei ya kawaida ya kila kitabu ni tsh elfu 20 lakini kwa bei ya zawadi inayoisha leo ni tsh elfu 15 kwa kila kimoja. Chukua hatua sasa rafiki, kwani yamebaki masaa machache sana.

Kama ndiyo unasikia kuhusu vitabu hivi vipya kwa mara ya kwanza, hapo chini kuna maelezo mafupi ya kila kitabu;

KITABU; UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Kila mtu amewahi kusikia au kuona miujiza ikitokea kwake au kwa wengine. Sehemu kubwa ya miujiza hiyo huwa inafanywa na watu wengine. Mfano ni pale mtu anapofanyiwa maombi na kisha akapona ugonjwa fulani au kupata matokeo fulani mazuri.

Kitu ambacho umekuwa huelezwi na wewe mwenyewe hujajua ni kwamba miujiza yoyote ile huwa inaanzia ndani ya mtu na siyo kutoka nje yake. Wale wa nje wanaoonekana kusababisha miujiza, huwa tu wanamsaidia mtu kufikia kwenye miujiza hiyo.

Ninachokueleza hapa rafiki yangu ni hiki, wewe hapo ulipo, una nguvu na uwezo mkubwa wa kutenda miujiza kwenye maisha yako.

Ndiyo, umesikia vizuri, wewe wewe, pamoja na yote yanayoendelea kwenye maisha yako, nguvu ya miujiza ipo ndani yako.

Lakini kwa bahati mbaya sana, hakuna ambaye amewahi kuchukua hatua kukujulisha kuhusu nguvu hii iliyopo ndani yako. Ndiyo maana huijui na hujaweza kuitumia.

Sasa umepata bahati ya kipekee sana ya kuweza kuijua nguvu ya kutenda miujiza iliyo ndani yako, na jinsi unavyoweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kinakupa nafasi ya kujua nguvu hiyo na jinsi unavyoweza kuitumia.

Una uwezo wa kuwa chochote unachotaka, kufanya na kupata chochote unachotaka, lakini hiyo ni kama tu utaweza kutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.

Hakuna ambaye amewahi kukupa siri hii unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki, ni siri inayokwenda kuyafungua maisha yako na hakuna chochote kitakachofichwa tena kwako.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa. Mwisho wa bei ya zawadi ni leo tarehe 30/10/2020, chukua hatua sasa ili usiikose.

ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Biashara fulani inalipa kweli, wewe ifanye tu na utapata mafanikio, huu ni moja ya ushauri ambao umewapoteza wengi kibiashara.

Wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kufuata mkumbo au ushauri wa bure kama huo na kuishia kupoteza mtaji na muda wao.

Biashara zimekuwa changamoto kwa wengi kwa sababu hakuna elimu sahihi inayotolewa kuhusu biashara.

Kwenye elimu ya msingi ambayo kila mtu anajifunza yale ya msingi kwenye maisha, biashara siyo moja ya misingi inayofundishwa.

Na hata wale wanaokwenda kusomea masomo ya biashara wanachojifunza ni vitu vinavyohusu biashara, mfano mlolongo wa thamani (chain of value), uhitaji na upatikanaji (demand and supply) na kutunza vitabu (book keeping).

Lakini kupata mafunzo kamili ya biashara, kuanzia kupata wazo sahihi, kugeuza wazo hilo kuwa biashara inayojiendesha kwa faida na kuweza kuiendesha biashara hiyo mpaka kufikia mafanikio, ni elimu ambayo hakuna inakopatikana.

Kwa kuona ombwe hili na changamoto ambazo wengi wanakutana nazo kwa kutokuijua misingi ya biashara, nimefanya utafiti wa kina na kutumia uzoefu wangu na wa watu wengine na kuweza kuja na kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Hii ni elimu ya msingi kweli kwa sababu ina yote muhimu ambayo mtu anapaswa kuyajua kuhusu biashara. Kuanzia kupata wazo, kusajili biashara, kutengeneza thamani, kupata wateja, kuwahudumia vizuri, kuajiri watu sahihi na hata kuikuza zaidi biashara yako.

Kwa zama tunazoishi sasa, ambapo nafasi za ajira ni chache kuliko wanaozihitaji, biashara ndiyo mkombozi. Lakini kwenda kuingia kwenye biashara kichwa kichwa bila ya kuijua misingi, ni kujipeleka kwenye anguko.

Pata leo nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, kama upo kwenye biashara utaweza kuiendesha biashara yako vizuri na kama ndiyo unapanga kuingia basi utajua yale muhimu ya kuzingatia ili ufanikiwe.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kama nilivyokueleza kwenye makala hii, nakwenda kukupa zawadi. Hivyo leo utakipata kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa. Mwisho wa bei ya zawadi ni leo tarehe 30/10/2020, chukua hatua sasa ili usiikose.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Nikukumbushe kwamba mwisho wa zawadi hii ni leo tarehe 30/10/2020, baada ya hapo vitabu vitakuwa vinapatikana kwa bei yake halisi. Chukua hatua leo hii ili usikose zawadi hizo nzuri kwako rafiki yangu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania