Habari rafiki yangu mpendwa,

Jana tarehe 15/11/2020 tulikuwa na SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, hii ni semina pekee ya kukutana ana kwa ana inayofanyika mara moja kila mwaka.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru sana wale wote walioweza kuhudhuria semina hiyo.

Washiriki wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020

Ni imani yangu kwamba kila aliyeshiriki ameondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima ili aweze kupiga hatua zaidi.

Semina ilikuwa na mengi, makubwa na mazuri, tumepata mengi kutoka kwa kila mmoja wetu, tumeweza kuona jinsi kila mtu anapambana kwenye kile anachofanya na matokeo ambayo anayapata.

Sasa kazi imebaki kwa kila mmoja wetu, kwenda kuhakikisha anafanya makubwa ili tunapokutana tena kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kila mmoja aweze kuwa na hadithi ya tofauti ya kushirikisha wengine.

Imani yangu ni kila mmoja wetu anaweza kwenda kufanya makubwa sana kupitia yale aliyojifunza, hivyo tukachukue hatua ili tuweze kuleta mabadiliko kwenye maisha yetu.

Washiriki wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020

Baada ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, nitoe maelekezo machache muhimu ya kuzingatia kwenye safari hii ambayo tupo pamoja kuelekea kwenye mafanikio makubwa zaidi.

1. Hakuna nafasi mpya za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kwa wale ambao wameshakuwa wanachama ndiyo watapata nafasi ya kuendelea, kwa wale ambao hawajawa wanachama hakuna tena nafasi ya kujiunga.

2. Kwa walio wanachama, ukishatoka hutapata tena nafasi ya kurudi kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama sasa wewe ni mwanachama, pambana sana usitoke, na ili usitoke zingatia yale muhimu ninayoshirikisha hapa.

3. Kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, kuna sehemu nyingine nzuri ya kuendelea kujifunza ambayo nashauri sana uwepo, kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA ambapo kila wiki unapata chambuzi za vitabu, fungua kiungo na ujiunge; https://www.t.me/somavitabutanzania

4. Nakwenda kufanya kazi na watu wachache ambao wamejitoa kweli, ambao wameshaelewa hiki ambacho nimekuwa nashirikisha kwa muda mrefu, wanachukua hatua na matokeo yanaonekana, hata kama siyo makubwa. Kufanya kazi na watu wengi inachosha kupitiliza na wengi wao wanakuwa hawajajitoa kweli kweli.

Kocha Dr Makirita Amani akitoa somo kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020

5. Natoa muda zaidi kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA waliopo, nimetoa maelekezo ya email itakayotumika kutuma tathmini na taarifa mbalimbali. Unapokuwa na changamoto au unahitaji ushauri wa Kocha wakati wowote ule, tuma kwenye email niliyotoa na utapata majibu.

6. Masomo ya kila wiki kwenye KISIMA CHA MAARIFA yatalenga kutatua changamoto ambazo wanachama wamezitoa kwenye tathmini zao au ushauri walioomba kwa kocha. Kwa kuwa changamoto zinajirudia rudia, nitazitafutia suluhisho la kina kwa namna ambayo kila mtu anaweza kunufaika.

7. Kila mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA anapaswa kuwa kwenye Klabu ya mkoa aliopo au mkoa wa karibu, tunakwenda kujenga ukaribu zaidi kupitia klabu zetu.

8. Kila mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA afuate mwongozo niliotoa wa mwaka wa mafanikio 2020/2021 na achukue hatua zote zilizoelekezwa kwenye mwongozo ili tuweze kwenda pamoja kwa mwaka huu wa mafanikio na muongo mzima wa mafanikio tuliouchagua 2020 – 2030.

Mwalimu Hamisi Msumi akitoa somo la mahusiano kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020

9. SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 itafanyika kwa siku mbili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021 jijini Dodoma. Hivyo anza kujiandaa mapema kwa kutenga muda huo ili uweze kushiriki bila kukosa.

10. Karibuni sana wale ambao mmepata bahati ya kipekee ya kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, nafasi ambayo haipatikani tena. Maono makubwa ninayopambana nayo ni haya, tunapofika mwaka 2030 huku tukiwa na mabilionea wengi Tanzania, wale walio juu kabisa kwenye orodha waonekane kuwa na kitu kimoja wanachofanana, ambacho ni wote Kocha wao ni Dr. Makirita Amani, najua hilo linawezekana bila ya shaka yoyote, kwa sababu kwa watu niliochagua kubaki nao, wanaweza kabisa kufika huko, hivyo nitawapa kila kilicho ndani ya uwezo wangu kuhakikisha wanafika huko. Hivyo kama umepata nafasi hii, usiichezee, itumie vizuri, nitumie vizuri, nimejitoa kwa ajili yako kama upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kama haupo kwenye KISIMA usijisikie vibaya na kuona Kocha amekutenga, bado nakupenda mno, hivyo nitaendelea kukushirikisha makala nzuri kupitia mtandao wa AMKA MTANZANIA, nitaendelea kutoa vitabu vingi na vizuri ambavyo utaweza kuvisoma na nitaendelea kusoma na kukuchambulia vitabu, huku nikikupa hatua za kuchukua ili maisha yako yawe bora.

Lakini kwenye KISIMA CHA MAARIFA, wacha nifanye kazi na wachache waliobahatika ili niweze kuleta matokeo ya tofauti na ya kipekee.

Naamini umenielewa rafiki yangu, hivyo nikukaribishe sana tuendelee kuwa pamoja.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania