“Nature does not hurry, yet everything is accomplished.” — Lao Tzu

Asili huwa haina haraka, lakini huwa inakamilisha kila kitu.
Asili huwa inafanya kila jambo kwa wakati wake na hivyo kukamilisha kila kitu.

Lakini sisi na haraka zetu tunaacha mengi ambayo hatujakamilisha.
Tuna mengi tunafanya na kuishia njiani.
Pamoja na mahangaiko yote, kufanya mambo mengi kwa pamoja, mengi hayakamiliki.

Dunia huwa inalizunguka jua kila siku, haina haraka hata siku moja.
Mzunguko huo ndiyo unatupa usiku na mchana pamoja na majira mbalimbali ya mwaka.

Tujifunze kutoka kwenye asili, kwa kujua nini tunachotaka na kisha kuchukua hatua ya kukifanya kwa ukamilifu.
Badala ya kuharakisha na kufanya mengi kwa pamoja, tunapaswa kuchagua machache na kuyafanya mwa kina.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wema wako usikuponze, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/13/2174

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.