Ni rahisi kujipima na kushindana na wengine, lakini unapoingia tu kwenye mashindano hayo, unakuwa umejipoteza.

Mtu sahihi wa kushindana naye ni wewe mwenyewe, kila siku kuhakikisha unakuwa bora kuliko ulivyokuwa jana yake.

Wewe ndiye unayejijua zaidi, wewe ndiye unajua unataka nini na ndani yako una nini.

Kama hujajua hayo, utahangaika na mashindano yasiyo na tija kwako.

Yeyote unayetaka kushindana naye hamfanani kwa chochote, hivyo hata kama utamshinda, wewe ndiye utakuwa umeshindwa kwa sababu umeacha yako na kuhangaika na ya wengine.

Ukurasa wa kusoma ni mashindano yatakufikisha wapi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/20/2212

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma