Unapaswa kuijua thamani yako na kisha kuiheshimu na kuisimamia, bils kujali wengine wanafanya nini au kukucgukuliaje.

Hupaswi kuyumbishwa na maoni ya wengine kuhusu wewe, ijue thamani yako na kuisimamia.

Kama ambavyo dhahabu itabaki kuwa dhahabu, hata kama itawekwa kwenye tope au kudharauliwa na wengine.

Na kama ambavyo noti ya elfu kumi itabaki ba thamani hiyo hata kama mtu ameitupa chini na kuikanyaga kanyaga, hakikisha na wewe unabaki na thamani yako bila ya kujali unapitia nini.

Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha ni kuwa wewe, kusimamia thamani yako bila kuyumbishwa na chochote.

Ukurasa wa kusoma ni mazoea yanavyokupoteza, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/05/2256

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma