Uimara wa kitu huwa unapimwa kwa kukipitisha kitu hicho kwenye mazingira magumu kabisa.

Mazingira ambayo kitu kisichokuwa imara hakiwezi kuyastahimili.

Hivyo pia ndivyo uimara wa watu unavyopimwa, kwa kuwapitisha kwenye mazingira magumu.

Unapopitia magumu yoyote, jua hicho ni kipimo cha uimara wako.

Unapoamua kufanikiwa, uimara wako utapimwa kwa viwango vya juu kuliko wengine, hivyo lazima uwe tayari kusimama imara.

Asili haipendi kutoa mafanikio makubwa kwa watu wasio imara, hivyo inaweka vipimo vigumu kwa wote wanaotaka mafanikio.

Kuwa tayari kuvuka kila aina ya ugumu ili uyafikia mafanikio makubwa unayoyataka.

Ukurasa wa kusoma ni watu watabaki kuwa watu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/03/2285

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma