2292; Rahisi ni hatari…
Ukiona kila unachofanya ni rahisi kwako, hukutani na ugumu wala changamoto, ogopa sana, kwa sehemu kubwa uko eneo hatari na hutaweza kufanya makubwa.
Japo huwa tunapenda mambo yawe rahisi, lakini iko wazi, hakuna mafanilio yamewahi kutokana na kufanya vitu rahisi.
Tukirudi kwenye asili, ambayo ina kila funzo kwetu, iko wazi kabisa kwamba vitu vyote rahisi havina thamani.
Chukua mfano wa shamba, hata usipolilima au kuweka mbolea, magugu ya kila aina yatamea na kustawi sana. Lakini huwezi kutumia magugu hayo kwa manufaa.
Ukitaka upate mazao yenye manufaa kwenye shamba, lazima ulime, upande, upalizi na kuweka mbolea.
Kadhalika kuweka umakini wako kwenye kitu unachofanya ni vigumu lakini usumbufu ni rahisi, usumbufu haujawahi kuwa na thamani yoyote.
Wakati wengine wanakimbilia urahisi, wewe uepuke kama ukoma. Pale unayofanya yanapokuwa rahisi, jua kuna mahali unakosea.
Hili halimaanishi uyafanye mambo kuwa magumu zaidi ya yalivyo sasa, bali unapaswa kuhakikisha chochote unachofanya kinatoa thamani kubwa kwa wengine.
Rahisi pia imekuwa inatumika kuwatapeli na kuwahadaa watu. Watu wanaposikia kuna njia rahisi na ya uhakika ya kufikia mafanikio huwa wanaikimbilia na hapo ndipo hupoteza fedha, muda na nguvu zao.
Rahisi haijawahi kuwa salama kwa yeyote, iepuke sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Kocha.
Nikweli rahisi ni hatari nilete mfano kwangu mwenyewe kwasababu ya ugumu wa mauzo nilikimbiliaga biashara ya miamala ya uwakala wa Benki na kwasababu hiyo benki ilitengeneza brand nikaona hiyo ni rahisi kabisa kwa kweli ni rahisi lakini hakuna kikubwa ambacho nilifanya kwa kufanya biashara ya miamala
LikeLike
Tusikimbilie urahisi.
LikeLike