Ndoa ni wito. Na siyo kila mtu ameitwa kuwa mwanandoa. Kama hujaitwa kuingia kwenye maisha ya ndoa usifosi baki hivyo kwani hata maandiko yanasema siyo kila mtu ameitwa kuwa mwanandoa.

Usiingie katika ndoa kwa sababu ni mazoea ya watu wengi kufanya hivyo.
Kabla hujaingia kwenye ndoa jitafakari kwanza, muumbe Mungu akusaidie kuisikia sauti ya wito wako.

Sasa tukirudi katika shabaha ya makala yetu ya leo ni kutaka kujua lengo namba moja la ndoa ni nini.

Na lengo namba moja la ndoa ni kufaidiana. Lengo la kwanza la ndoa ni kwa faida ya wale wawili wanaooana kimwili, kiroho, kimaadili na kimaisha.

Lazima wanandoa wanufaike na ndoa yao. Wakamilishane, wafarajiane, wasaidie na wafurahie ndoa yao wawili.

Tumeona faida namba moja ya ndoa ila siku hizi kuna ndoa ambazo hazionji faida hiyo. Na mimi rafiki yako nimefanya utafiti na kukuandikia kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa kitachokwenda kutibu ndoa ambazo zina njaa.

Je, ndoa yako ina njaa? Kama jibu lako ni ndiyo jipatie nakala yako itakayokwenda kutibu njaa ya ndoa yako.

Hatua ya kuchukua leo; usivumilie maisha ya ndoa badala yake furahia maisha ya ndoa.

Jifunze namna ya kufurahia maisha ya badala ya kuvumilia. Na mafunzo hayo yanaonekana kwenye kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa.

Bei ya kitabu hiki ni elfu 20 lakini nimeamua leo kukupa kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 15 ili usome na mwenza wako au kama huna ndoa basi utakua kwenye uchumba na muda mzuri wa kujifunza.

Wasiliana nasi kwa namba 0717101505//0767101504 kupata nakala yako. Yaani ukituma fedha tu unatumiwa kitabu chako.

Usikubali kupitwa na ofa hii nzuri ya leo ya siku ya muungano. Wahi, nakala ni chache. Kuwa wa kwanza kujipatia nakala yako.

Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali.

Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa
http://kessydeo.home.blog ,vitabu nakwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI. Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,
Mwl, Deogratius kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante sana