Ndiyo mchango wako katika kuifanya dunia kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi.

Kwa kukifanya vizuri na kwa ubora wa hali ya juu, kwa kuongeza thamani kubwa kwa wengine, unakuwa umetoa mchango mkubwa sana.

Hata kwa misaada, utasaidia wengi kwa kufanya kazi au biashara yako vizuri, kutengeneza kipato kikubwa na kukitoa kwa wenye uhitaji, kuliko kwenda wewe moja kwa moja kuwasaidia.

Wengi hupoteza juhudi zao wakidhani wanasaidia kumbe wanajaribu kabisa. Msaada wowote unaojaribu kutoa nje ya kazi au biashara yako hauwezi kuzaa matunda mazuri kama ukifanya kupitia kazi au biashara yako.

Fanya kile unachofanya vizuri, kwa viwango vya juu, kwa namna ambayo maisha ya wengine yanakuwa bora zaidi na utakuwa umetoa mchango na msaada mkubwa hapa duniani.

Ukurasa wa kusoma ni mchango wako kupitia kazi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/04/2316

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma