
Unaweza kuona una ushauri mzuri sana kwa wengine, lakini tambua siyo wote watakaoona uzuri wa ushauri huo kama unavyouona wewe.
Na hata kama watauona huo uzuri, bado siyo wote watakaofanyia kazi ushauri wako. Na kama unawashauri bila ya wao kuomba, ndiyo kabisa hawatajihangaisha na ushauri wako.
Watu huwa hawathamini ushauri wanaoupata kirahisi kabla hawajaumia. Hivyo kama mtu hajaja kwako kukuomba umshauri, okoa muda wako kwa kutokuhangaika kumshauri, maana hatofanyia kazi.
Ukurasa wa kusoma ni kama hawajakuomba usijisumbue; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/05/2348
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma