Rafiki yangu mpendwa,
Ninayo furaha kukufahamisha kwamba kitabu kipya kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU; Jiajiri na Ingiza Fedha Kwa Kutumia Simu Yako Ya Mkononi kipo tayari kwa ajili yako.
Hiki ni kitabu chenye maarifa na hatua za kuchukua ili uweze kujiajiri kwa kutumia simu yako.

Kitabu hiki nimekiandika kushirikisha uzoefu wangu wa jinsi ninavyofanya hatua kwa hatua mpaka kuweza kuuza huduma na bidhaa mbalimbali mtandaoni.
Kila nilichoshirikisha kwenye kitabu hicho, nimekufanya mwenyewe na kuyaona matokeo yake.
Hivyo nakusaidia wewe uache kubatisha badala yake ufanye yale ya uhakika.
Kitabu kitakusaidia uepuke makosa ambayo wengi wanayafanya na kushindwa kuingiza kipato kwa kutumia simu zao.
Kitabu nimekiandaa kwa mtiririko ambao ni rahisi kwa kila mtu kuufuata, kuelewa na kuchukua hatua.
Nimekiandika kwa dhana ya mtu kujenga makazi yako mtandaoni maana ndipo penye fursa zote kwenye zama hizi za taarifa.
Hatua ya kwanza ni kujenga msingi wa nyumba yako, unajua nyumba bila msingi haidumu. Na msingi ukiwa imara nyumba inakuwa imara.
Msingi utakaoujenga kwenye kitabu hiki ni wa UJASIRIAMAARIFA. Utajifunza kwa kina maana ya neno hilo na jinsi ya kujenga msingi huo.
Hatua ya pili ni kujenga nguzo ya ngumba yako, nguzo ndiyo inaisimamisha nyumba. Nguzo muhimu ya kuweza kuingiza fedha kwa simu yako ni kutoa thamani. Hapa utajifunz jinsi ya kutoa thamani ambayo watu wapo tayari kuilipia.
Hatua ya tatu ni kukamilisha nyumba yako ili uwe na makazi ya kudumu mtandaoni. Nyumba yako mtandaoni ni blog, hapo ndipo kila kitu kuhusu wewe na yale unayofanya kinapatikana.
Kwenye kitabu utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza blog na kuitumia kuingiza kipato.
Hatua ya nne ni kuwa na chumba maalumu kwenye nyumba yako ya mtandaoni, kwenye chumba hicho unawaalika wale makini kabisa. Hapa unajifunza mifumo ya kuwasiliana na watu moja kwa moja, kwa barua pepe au ujumbe mfupi wa simu.
Hatua ya tano ni vijiwe ambavyo unaenda kupiga soga na kukutana na watu wanaoweza kunufaika na thamani unayotoa. Hapa unajifunza jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kujenga hadhira.
Hatua ya sita ni kujenga jumuia ya watu wanaonufaika na kile unachofanya. Hapa unakuwa na makundi maalumu ambapo mashabiki wako wa kweli wanajiunga, unawapa thamani zaidi na wanakuwa tayari kulipia.
Hatua ya saba ni njia kumi za uhakika za kuingiza kipato kwa simu yako na mtandao wa intaneti. Hapa utajifunza kwa mifano kabisa ili uweze kuchukua hatua mara moja.
Hapa utajifunza pia kuweza kuandika kitabu kwa kutumia simu yako.
Hatua ya nane ni kutoka watu sifuri mpaka kupata mmoja, kisha kumi, mia mpaka kufika elfu na kuendelea. Hapo utajifunza jinsi ya kujenga mashabiki wa kweli na kuingiza kipato kizuri.
Hatua ya tisa ni mbinu za masoko na mauzo, uweze kuwafikia wengi na kuwashawishi kuja na kununua bidhaa na huduma unazouza.
Hatua ya kumi ni mipango mikubwa. Kujiajiri kwa simu yako siyo kitu cha kufanya tu kwa kujaribu, bali ni kitu cha kufanya kwa uhakika na kuweza kufanya makubwa. Hapa utajifunza jinsi ya kuwa na malengo makubwa, kuyafanyia kazi na kuyafikia.
Mwisho kabisa utakuwa tayari kuchukua hatua mara moja na hiyo simu unayotumia sasa iweze kuwa ofisi yako.
Rafiki, tayari unayo simu na mtandao wa intaneti ndiyo maana unaweza kusoma hapa. Nikusihi usome kitabu hiki ili uanze kutumia simu yako kwa manufaa.
Kujiajiri na kuingiza kipato kwa kutumia simu hakuhitaji uwe na mtaji wowote au maandalizi mengine. Ni kitu unachoweza kufanya kwa kuanzia hapo hapo ulipo sasa.
Iwe umeajiriwa, unafanya biashara, mwanafunzi au huna unachofanya, kitabu hiki kitakuwezesha kuingiza kipato kwa simu yako.
Kama umeajiriwa kitabu kitakusaidia kuanzisha biashara ya pembeni kwa kutumia simu yako.
Kama una biashara kitabu kitakusaidia kujenga wateja waaminifu na kukuza mauzo ya biashara unayofanya sasa.
Kama huna kazi au biashara kitabu kitakuwezesha kujenga biashara ya kipekee kwako, inayokupa uhuru wa kufanya kazi ukiwa popote.
Na kama ni mwanafunzi wa chuo, kitabu kinakufundisha jinsi ya kuanza kujiajiri kabla hata hujahitimu, ili unapohitimu husumbuki ukikosa kazi, unakuwa tayari una mfumo unaoingiza kipato.
Uzuri ni kwamba, kitabu kinakufundisha jinsi ya kitumia simu pekee, ambayo tayari unayo, hivyo huna sababu ya kusubiri.
Na ili kuonyesha mfano, nimeandika kitabu hiki chenye kurasa 175 kwa kitumia simu tu. Kila kitu kuanzia kuandika, kuhariri, kuweka picha na kutengeneza ganda la kitabu nimetumia simu ya mkononi.
Na nimekuonyesha kwa picha jinsi unavyoweza kufanya hivyo pia.
Rafiki, hiki siyo kitabu cha kukosa kama unataka kuongeza kipato chako zaidi.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 uweze kupata kitabu hiki.
Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.
Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.
Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf
Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz