Rafiki yangu mpendwa,
Maisha ni mfululizo wa changamoto mbalimbali.
Hakuna siku utaamka uwe huna changamoto kabisa.
Ukitatua changamoto moja, unakuwa umefungua changamoto nyingine kubwa zaidi.

Hivyo badala ya kutamani maisha yasiwe na changamoto, kuwa imara ili uweze kukabiliana na kila changamoto unayokutana nayo.

Na njia ya uhakika ya kuwa imara kukabiliana na changamoto yoyote unayokutana nayo kwenye maisha yako ni kuwa na maarifa sahihi.

Hapa nimekuandalia maarifa sahihi ya kukabiliana na changamoto kubwa tano ambazo zinawakabili wengi.

Moja; fedha, madeni, uwekezaji.
Eneo la fedha ndiyo ambalo kila mtu kuna changamoto anakuwa anapitia.
Kubwa kwa wengi ni kipato kutokutosheleza, wengi wana kipato ambacho hakitoshelezi mahitaji ya maisha yao.
Nyingine ni madeni yanayotokana na watu kukopa ili kukidhi mahitaji ambayo uhaba wa kipato umeshindwa kukidhi.
Na nyingine ni uwekezaji, wengi hawana uwekezaji sahihi utakaoweza kuwafikisha kwenye uhuru wa kifedha.

Maarifa sahihi.
Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kina maarifa sahihi ya kukuwezesha kukabiliana na changamoto zote za kifedha unazopitia sasa na utakazokuja kupitia huko mbeleni.
Kinakupa maarifa ya jinsi ya kuongeza kipato chako, kuondoka kwenye madeni na kuifanya fedha ikufanyie kazi ili uweze kuwa huru.

Mbili; mshahara hautoshi.
Mshahara haujawahi kutosha na wala hautakujakuwahi kutosha.
Huwa kuna utani kwamba mwajiri huwa anamlipa mfanyakazi mshahara kidogo kwa kiasi kwamba hataacha kazi.
Msingi wa utani huo ni kwamba hutaweza kupata kiasi cha fedha unachoona unastahili kupata kwa kutumia mshahara.
Anayeamua mshahara wako ni mtu mwingine, kwa vigezo anavyojua yeye.
Na hata pale mshahara unapoongezeka, bado huwa hautoshelezi.
Hivyo huwezi kutegemea mshahara pekee kama unataka kuwa na kipato cha uhakika.

Maarifa sahihi;
Kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA kina majibu kwako ya namna ya kuongeza kipato chako bila ya ukomo.
Utaweza kufanya hivyo kwa kuanzisha biashara ukiwa bado upo kwenye ajira.
Kitabu hiki kinakuongoza kuanzia kupata wazo, kuanzisha na kukuza biashara yako.
Kitabu kinakupa mbinu za kuweza kuendesha biashara na ajira kwa wakati mmoja bila ya kuingiliana.

Tatu; kuanzisha na kukuza biashara.
Kila utafiti ambao huwa nafanya kwa wasomaji wa maarifa ninayoshirikisha biashara huwa ni kitu ambacho kinawasumbua wengi.
Wengi wanataka kuanza biashara ila wanakutana na vikwazo mbalimbali.
Na wapo walioanza biashara ila wanakutana na changamoto zinazozuia biashara zao zisikue na hata wakati mwingine kupelekea biashara hizo kufa.

Maarifa sahihi;
Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kinakupa maarifa sahihi ya jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio makubwa.
Kitabu kinaanza na wewe kwenye kupata wazo sahihi kwako, kusajili biashara, kupata mtaji, kushawishi wateja na kuendesha biashara kwa misingi sahihi ili iweze kufanikiwa.
Huu ni mwongozo sahihi kwa kila aliye kwenye biashara au anayepanga kuingia kwenye biashara.

Nne; umekata tamaa na maisha.
Watu wengi wamekata tamaa na maisha na kujiona hawawezi kupata mafanikio makubwa.
Hilo linatokana na uongo ambao watu hao wanakuwa wamelishwa na jamii tangu wakiwa wadogo.
Hadithi ambayo mtu amekuwa anaambiwa tangu akiwa mtoto, ndiyo anaiamini na kuiishi, kitu ambacho siyo sahihi na kinakuwa kikwazo.

Maarifa sahihi;
Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kinakuonyesha nguvu kubwa kabisa iliyo ndani yako na jinsi ya kuweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Haijalishi uko wapi kwa sasa, jua kabisa unaweza kufanya makubwa zaidi.
Usikubali yeyote akukatisha tamaa kwa kukuambia huwezi au haiwezekani.
Kifanye kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kuwa mwongozo wako ili uendelee na mapambano na ufanye makubwa.

Tano; simu yako imekugeuza kuwa mtumwa.
Kwa zama tunazoishi sasa, simu zetu za mkononi ambazo ni simu janja, zimetuzidi ujanja.
Simu hizi zimechukua sehemu kubwa ya maisha yetu kitu ambacho kimekuwa siyo kizuri.
Tunalala nazo na kuamka nazo. Tunatembea nazo kila mahali.
Na hilo limekuwa na athari kubwa kwenye utulivu wetu kwa ujumla.
Ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kushika udhibiti wa maisha yako na kuacha kuwa mtumwa wa simu yako au teknolojia nyingine mpya.

Maarifa sahihi;
Kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI kinakupa maarifa sahihi ya kuweza kuondoka kwenye mtego huo wa simu janja. Kitabu kinakupa mbinu za kuweza kuitumia simu na teknolojia kwa manufaa na siyo kutumika na teknolojia kwa manufaa ya wengine.
Kwa namna teknolojia inavyokwenda kwa kasi na kupata nguvu ya kuteka watu, kitabu hicho kinapaswa kuwa nguzo yako la sivyo utashindwa kufanya makubwa.

Rafiki, pata vitabu hivyo vitano nilivyokushirikisha hapa na uvitumie kama mwongozo wa kukabiliana na changamoto hizo tano kubwa zinazokukabili na kuwa hatari kwako kupata mafanikio makubwa.

Vitabu hivyo vimechapwa (hardcopy) na unaweza kutumiwa popote pale ulipo ndani ya Afrika Mashariki.
Kama upo Dar es salaam utaletewa mpaka ulipo bila ya gharama ya ziada.
Kupata vitabu, wasiliana sasa na 0752 977 170.

Hakuna changamoto inayokusumbua sasa ambayo haina majibu, wekeza kwenye maarifa sahihi na utaweza kuzivuka changamoto mbalimbali na kufanya makubwa.

Rafiki yako anayekupenda sana.
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani
www.somavitabu.co.tz