Rafiki yangu mpendwa,
Tunaendelea na sababu 30 kwa nini hupaswi kabisa kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 itakayofanyika tarehe 16 na 17 oktoba 2021 jijini Dodoma.

Kama unasoma hapa, hii ni semina yako na hupaswi kuruhusu sababu yoyote ile ikuzuie kushiriki.
Kwa sababu husomi hapa kujifurahisha, bali unasoma hapa kwa sababu una kiu ya mafanikio makubwa.

Kuna mambo mengi ungeweza kuwa unayasoma sasa, mengi mno, lakini umechagua kuachana na hayo mengine yote na kusoma makala hii. Hicho ni kiashiria tosha kwamba unataka makubwa na bora zaidi.
Na ambacho ninaweza kukuhakikishia ni hayo yanapatikana kabisa, ila siyo rahisi kama wengi wanavyodhani.

Katika kipindi ambacho nimekuwa natoa huduma za mafunzo, ushauri na ukocha, nimekuwa naona picha moja ikijirudia sana.
Mtu anakutana na kazi zangu, anazisoma na kuzielewa, anapata hamasa kubwa ya mafanikio, anajiwekea malengo makubwa kabisa na kuona mafanikio ni yake.

Yote hayo ni mazuri kabisa, lakini tatizo kubwa linakuja pale mtu anapoanza kufanyia kazi malengo makubwa aliyojiwekea.
Anakutana na changamoto na vikwazo mbalimbali, kitu ambacho ni kawaida kwenye safari ya mafanikio.

Lakini mtu huyo kwa kuwa alikuwa hajajiandaa kwa vikwazo na changamoto, anashindwa kuendelea, anakimbilia kufanya kitu kingine ambacho kwa nje kinaonekana ni rahisi kuliko kile anachofanya sasa.

Anaenda kwenye kitu kingine, akiwa na hamasa kubwa kwamba anakwenda kufanya makubwa. Huko nako mambo yanajirudia, mtu anakutana na vikwazo na changamoto ambazo hakutegemea.
Anaacha tena na kwenda kuanza kitu kingine.

Hivyo ndivyo wengi huyaendesha maisha yao, kwa kutamani kupata mafanikio makubwa, lakini kutokuwa tayari kuweka juhudi kwenye kitu kwa muda mrefu mpaka waone matokeo mazuri.

Je wewe ni mmoja wa watu ambao umekuwa unakutana na ugumu kwenye kila kitu unachoanza?
Je mpaka sasa umeshajaribu vitu mbalimbali lakini hakuna hata kimoja ambacho umepiga hatua kubwa?
Je unataka kuweka juhudi zako kwenye kitu ulichochagua bila ya kusumbuliwa na fursa mpya zinazoibuka kila siku?

Kama majibu ni ndiyo, basi usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwani kwenye semina hii utaweka mpango wako wa mwaka wa mafanikio 2021/2022 na Kocha atakusimamia kwa karibu katika utekelezaji wa mpango huo kwa mwaka mzima.

Kocha hatakupa mwanya wa kuhangaika na mambo yaliyo nje ya mipango uliyojiwekea.
Kwa kufanyia kazi mpango wowote ulionao kwa mwaka mzima, lazima utapata matokeo ya tofauti na ambayo umekuwa unapata huko nyuma.

Na hata pale utakapokutana na magumu na changamoto, mtashauriana vizuri na kocha namna ya kuvuka magumu hayo  na kuendelea na mipango yako.

Magumu na changamoto ni njia ya asili ya kuwaengua wale ambao hawajajitoa kweli kufanikiwa.
Hivyo kipimo cha kwanza cha kama umejitoa kweli kufanikiwa, ni kuwa tayari kuvuka kila aina ya magumu na changamoto.

Kwa usimamizi wa karibu wa kocha, utaweza kuvuka kila aina ya magumu na changamoto utakazokutana nazo.
Kocha atakusimamia kuiishi kauli ya mafanikio inayosema nitapata ninachotaka au nitakufa nikiwa nakipambania.

Je wewe hutaki kupata mafanikio makubwa kwenye kile ulichochagua?
Nani asiyependa kupiga hatua zaidi ya pale alipo sasa?
Ushiriki wa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni hatua ya kwanza kwako kuhakikisha unapata kile unachotaka.

Na kuonyesha kweli kwamba hutaruhusu chochote kikuzuie kufanikiwa, usiruhusu chochote kikuzuie kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kama kuna ambacho kinaweza kukuzuia kushiriki semina, maana yake umekubali kuna vingi vinaweza kukuzuia kufanikiwa.

Kataa hilo sasa kwa kuhakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, chukua hatua sasa ili uitangazie dunia na asili kwamba utafanikiwa na hakuna kinachoweza kukuzuia.

Kama bado hujathibitisha kushiriki semina, tuma ujumbe sasa kwenda namba 0717 396 253.
Kama umeshathibitisha, kamilisha malipo ya ada yako mapema.

Kama ndiyo kwanza unapata taarifa hizi za semina, maelezo zaidi yako hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz