Rafiki yangu mpendwa,
Tupo kwenye mfululizo wa sababu 30 kwa nini hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Sababu ya kwanza ni kuongeza kipato chako kwa angalau milioni 2.
Sababu ya pili ni kupata usimamizi wa karibu wa Kocha kwa mwaka mzima.
Na sababu ya tatu, ambayo ni muhimu nno kwa mafanikio yako ni kujenga mtandao sahihi.

Jim Rhon amewahi kusema wewe ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka na unaotumia nao muda wako mwingi.

Vile ulivyo na mafanikio uliyonayo, hayawezi kuwazidi watu wako watano wa karibu.

Na hapa kuna siri kubwa kuhusu mafanikio ambayo imekuwa haiongelewi sana.

Watu wanashauriwa kujifunza sana ili kufanikiwa.
Wanashauri kuweka juhudi kubwa kwenye kazi ili kufanya makubwa.
Yote hayo ni muhimu, lakini yatakuwa kazi bure kama mtu hatazungukwa na watu sahihi.

Ndiyo rafiki, unaweza kuhangaika kweli kweli, lakini bado usifanikiwe, na sababu inakuwa wazi, umezungukwa na watu ambao hawajafanikiwa na wala hawana mpango wa kufanikiwa.

Binadamu huwa tuna tabia kama ya kaa.
Ukimweka kaa mmoja kwenye chupa ambayo hujaifunika, haitachukua muda atatoka kwenye chupa hiyo na kuwa huru.
Ila ukiweka kaa wawili kwenye chupa ambayo haijafunikwa, hata mmoja hataweza kutoka.
Kwa sababu kila mmoja anapojaribu kutoka, mwingine anamrudisha.

Hilo ndiyo linalotokea kwenye mapambano ya mafanikio.
Kama umezungukwa na watu ambao hawajafanikiwa na hawapo kwenye mapambano ya kufanikiwa, hawatakuacha ufanikiwe.

Maana kila utakapojaribu kufanikiwa, watakuwa wa kwanza kukutudisha nyuma ili usiwaache wenyewe.
Badala wapambane waende na wewe juu, wanakurudisha chini ili muwe pamoja.

Wanafanya hivyo kwa kukukatisha tamaa, kukushauri vibaya na hata kukuwekea vikwazo mbalimbali.

Rafiki, huenda unajiambia hilo siyo tatizo kwangu, naweza kuwa na ambao hawajafanikiwa lakini nisiruhusu wawe kikwazo kwangu.
Na hapo nakuambia tu unajidanganya. Unaweza kutamani sana kuwazuia wasiwe kikwazo kwako, lakini hutaweza kutekeleza hilo.
Wanapokuwa pamoja wana nguvu kubwa kuliko wewe.

Hivyo unawahitaji watu sahihi ili ufanikiwe, watu ambao tayari wameshafanikiwa au wanapambana kufanikiwa.
Watu hao watakushirikisha uzoefu wao na hata kukupa hamasa ya wewe kufanikiwa zaidi.
Watu hao watataka kukuona ukifanikiwa na hawawi kikwazo kwako.

Changamoto ni unawapata wapi watu wa aina hiyo? Maana kwenye jamii zetu ni nadra sana kuwapata.
Na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa wewe kuhudhuria SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Semina hiyo inawakusanya wale wote wenye kiu ya mafanikio kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na wengine nje ya Tanzania. Wanakuja pamoja kujifinza, kushirikishana uzoefu na kuhamasishana kwenda kufanya makubwa zaidi.

Hakuna sehemu nyingine unaweza kukutana na watu wengi wa aina hiyo kwa pamoja.
Watu ambao wamekuwa tayari kuacha shughuli zao na kusafiri kuhudhuria tukio hilo, ni watu ambao wana thamani kubwa mno kwenye safari ya mafanikio.

Kupata tu nafasi ya kuwa kwenye chumba kimoja na watu hao, tayari kunakubadili mno mtazamo wako.
Kama kuna vitu ulidhani haviwezekani, wewe mwenyewe unaanza kuona vikiwezekana, kwa kuzungukwa tu na watu sahihi.

Unahitaji mtandao sahihi ili kufanikiwa.
Unawahitaji watu sahihi wa kuambatana nao kwenye safari yako ya mafanikio.
Ni vigumu kuwapata watu hao kwenye mazingira uliyopo.

Hivyo sehemu pekee na ya uhakika kwako kuwapata watu sahihi kwa safari yako ya mafanikio ni kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, hivyo basi, hilo siyo tukio la wewe kukosa.

Fanya kila namna kuhakikisha unahudhuria tukio hili la kipekee sana, kwani halitakuacha vile ulivyo sasa.
Litaamsha kitu cha tofauti ndani yako na mtandao mpya utakaoujenga utakusaidia sana kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Kama bado hujathibitisha kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 fanya hivyo leo hii ili ujihakikishie nafasi ya kushiriki. Wasiliana na 0717 396 253 kujiwekea nafasi yako.
Na kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina endelea kukamilisha kwa sababu siku zimebaki chache.

Kama ndiyo unasikia kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 kwa mara ya kwanza basi taarifa zaidi ziko hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz