Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wanaotamani kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao hawataweza kuyapata.
Unaweza kushtuka kusikia hilo kutoka kwa Muuza Matumaini kama mimi, lakini huo ndiyo ukweli.
Ni wachache mno, mno, mno ambao wataweza kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao.
Na hilo ni jambo zuri kabisa.
Kwa sababu mafanikio ni magumu kuyapata na magumu zaidi kuyatunza baada ya kuyapata.

Mafanikio makubwa kwenye maisha yanataka mtu ajitoe kweli kweli kwenye lile eneo alilochagua kufanikiwa na kupuuza mengine yote ambayo hayana mchango kwa mafanikio yake.
Mafanikio makubwa yanahitaji mtu kutokujali kaisa wengine wanamfikiria au kumchukuliaje, badala yake apambane na kile alichochagua.
Siyo wote wanaweza hayo na hakuna ubaya wowote kwenye hilo.
Lengo la kukuandikia hapa rafiki yangu ni kutaka ujiambie ukweli kama ulivyo na siyo kujidanganya.
Najua unayataka mafanikio makubwa ndiyo maana unasoma hapa.
Swali ni je umejitoa kwa kiasi gani kuhakikisha unayapata mafanikio unayoyataka?
Upo tayari kutoa nini ili upate kile hasa unachotaka?
Kama kweli umejitoa ili kupata mafanikio makubwa,
Kama kweli umeamua hakuna kitakachokuwa na nguvu ya kukuzuia usifanikiwe,
Basi kuna hatua moja muhimu sana unayopaswa kuchukua.
Hatua hiyo ni kushiriki kwenye ubatizo wa uhakika wa mafanikio ambao utafanyika tarehe 16 na 17 Oktoba 2021 jijini Dodoma.
Katika ubatizo huo, unakwenda kupata vitu viwili muhimu sana na vya uhakika kwako kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Na uwezo wa wewe kushiriki kwenye ubatizo huo, ni kiashiria cha kwanza kama kweli umejitoa kwa mafanikio na hakuna kinachoweza kukuzuia.
Mhamasishaji Eric Thomas amewahi kusema hakuna mtu mvivu au asiye na juhudi, wengi hawajajua nini wanachotaka kweli.
Anatoa mfano, mchukue mtu yeyote, mpeleke kwenye kina kirefu cha maji na atapambana sana kujiokoa.
Na hapo anahitimisha kwa kusema ukiyataka mafanikio kama unavyotaka kupumua, hakuna cha kukuzuia.
Je wewe ni nini kinaweza kukuzuia usishiriki kwenye ubatizo mkuu wa mafanikio utakaofanyika kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021?
Kama kuna chochote kinachoweza kukuzuia, maana yake umekiri kwamba hujajitoa kweli kufanikiwa.
Na simaanishi hilo ni baya, ila ninachotaka kukutahadharisha ni usijidanganye tu.
Usijilishe upepo kwamba utafanikiwa tu wakati kuna vitu umeviruhusu viwe kikwazo kwako.
Mafanikio yanataka yawe kipaumbele cha kwanza kwako, la sivyo hayatakaa kwako.
Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, sehemu ambayo wale wote wenye kiu ya mafanikio makubwa na waliojitoa kweli kufanikiwa wanakutana na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
Kama bado hujajiwekea nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako, wasiliana sasa na 0717 396 253 upate nafasi yako mapema.
Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa, kwani siku zimebaki chache za kufika ukomo wa kulipa ada.
Na kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz