Rafiki yangu mpendwa,

Aliyekuwa mhamasishaji mashuhuri, Zig Zigler aliwahi kushirikisha kwenye mafundisho yake swali ambalo amekuwa anakutana nalo mara nyingi.

Alieleza kila anapokuwa anaongea na uongozi wa kampuni au taasisi anayokwenda kutoa mafunzo ya hamasa, swali huwa ni hamasa hiyo itadumu kwa muda gani?

Zigler alikuwa akiwajibu kwamba hamasa siyo kitu cha kudumu milele.
Lakini pia kula na kuoga siyo vitu vya kudumu milele.

Huogi mara moja na kusema utakuwa msafi milele.
Na wala huli chakula mara moja na kusema utakuwa umeshiba milele.
Vitu hivyo muhimu unavifanya kila siku ya maisha yako.

Rafiki, hamasa kutokudumu ni moja ya vikwazo ambavyo wengi wanakutana navyo wanaposhiriki mafunzo ya moja kwa moja.

Wakati wa mafunzo mtu anapata hamasa kubwa na kujiona anaweza kila kitu.
Anatoka akiwa na shauku ya kwenda kufanya makubwa sana kwenye maisha yake.

Lakini siku chache baadaye hamasa hiyo inapotea kabisa na anajikuta amerudi kwenye mazoea yake ya awali.
Kwa changamoto hii, wengi huona hakuna haja ya kuhudhuria mafunzo hayo kwa sababu hamasa wanayopata haidumu.

Rafiki,  kuna mafunzo ambayo hamasa yake ukiipata inadumu kwa mwaka mzima hila kuchuja.
Hiyo ni kwa sababu kuna hatua za kuchochea hamasa uliyoipata kila siku  kitu kinachoifanya hamasa hiyo kuwa ya milele.

Mafunzo hayo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Mafunzo haya yana sifa kuu tatu zinazoyafanya yawe na hamasa utakayodumu nayo kila siku.
1. Unaweka mpango kabisa utakaokwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima. Hushiriki tu kupata hamasa, bali unaweka mpango thabiti.
2. Kuna kauli unazojiambia na kuziandika kila siku. Kauli hizo zinaichochea hamasa uliyoipata na kukuwezesha kufanya makubwa.
3. Unapata usimamizi wa karibu wa Kocha. Mafunzo mengi yakishaisha ndiyo imetoka, ila SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA ni tofauti. Unaposhiriki, Kocha anakufuatilia kwa karibu kwa mwaka mzima. Hilo linakupa msukumo wa kufanya makubwa.

Rafiki, kwa kuyaona manufaa hayo makubwa ya SEMINA ZA KISIMA CHA MAARIFA kwa namna zinakupa hamasa ya kudumu, nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

Semina hii ya kukutana ana kwa ana itafanyika jijini Dodoma kwa siku mbili, tarehe 16 na 17 oktoba 2021.
Hizo ni ziku mbili za kujifunza, kuhamasika na kuweka mipango na mikakati utakayofanyia kazi kwa mwaka mzima.

Kwa kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 unakwenda kupata maarifa sahihi, hamasa na mtandao sahihi wa kukuwezesha kufanikiwa na kufanya makubwa zaidi.

Hii siyo semina ya wewe kukosa kwa namna ulivyo na kiu ya mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Maana kwenye semina hii unakwenda kukutana na watu sahihi kwa safari ya mafanikio uliyochagua.

Rafiki, nikukumbushe zimebaki siku 20 tu kupata nafasi ya kushiriki semina hii.
Kuna hatua kubwa mbili za kuchukua leo hii kama bado hujazichukua.
1. Kama hujathibitisha kushiriki semina fanya hivyo sasa hivi. Hilo litakuhakikishia nafasi ya kushiriki, maana hazipo nyingi. Wasiliana na 0717 396 253 kujiwekea nafasi ya kushiriki.
2. Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina fanya hivyo mapema. Unaweza kulipa kidogo kidogo kila siku au kulipa yote mara moja. Njia za kulipia zipo hapo chini.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, tujifunze na kuhamasika kwa pamoja na kwa mwaka mzima uende kufanya makubwa.

Kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz