Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wamekuwa wanapambana kujenga biashara, lakini zimekuwa hazidumy kwa muda mrefu.
Nguvu zote wanazokuwa wameweka zinakuwa zimepotea.

Kwanza kuna wale wanaokimbizana na kila biashara mpya inayokuja kwa kuona ni fursa ambayo hawapaswi kuikosa.
Hawa huhangaika na biashara mbalimbali na mwishowe hakuna hatua wanazopiga.

Halafu kuna wale wanaokazana kujenga biashara ambazo wanaziendesha vizuri kipindi ambacho wao wenyewe wapo kwenye biashara.
Ila inapotokea kwamba hawawezi kuwa tena kwenye biashara, zinakufa.

Wanakuwa wameweka juhudi kubwa kujenga biashara zao, lakini zinawategemea wao kwa kila kitu.
Wanapokuwa hawapo, biashara zinakufa.

SAMSUNG CAMERA PICTURES

Hapa nakwenda kukushirikisha hatua za msingi za kuchukua ili kuweza kujenga biashara iyakayodumu kwa muda mrefu, vizazi na hata vizazi, iwe mwanzilishi upo au haupo.

1. Maono.
Biashara lazima iwe na maono makubwa ili iweze kukua na kudumu.
Msukumo wa kuingia kwenye biashara haupaswi kuwa tu tamaa ya faida ambayo mtu anaona anaweza kupata.
Bali kunapaswa kuwepo kwa maono makubwa ya mabadiliko ambayo biashara hiyo inakwenda kuleta.
Angalia makampuni yote makubwa na ambayo yamekuwepo kwa zaidi ya miaka 50, yana maono makubwa ambayo ndiyo yanafanyiwa kazi.
Kila kizazi kinachoingia kuendesha biashara, kinasimama kwenye yale maono.

Unapaswa kuweka maono makubwa ya biashara yako ambayo yatakuwa ndiyo mwongozo mkuu wa biashara hiyo wakati wote.

2. Thamani.
Biashara inapaswa kuwa na thamani ambayo inaitoa.
Wengi hukimbilia kwenye biashara kwa tamaa ya faida, kwa kuona inalipa.
Ambacho hawaangalii ni thamani gani wanayokwenda kuitoa kwenye biashara hiyo.
Kwa sababu hiyo, wengi wamekuwa wanahangaika na biashara ambazo kwa nje zinaonekana kuingiza faida kubwa na ya haraka, lakini ndani hazina thamani yoyote.
Nyingine zinakuwa ni biashara za msimu au kipindi kifupi, mtu anaingia na kufanya uwekezaji na kuja kujikuta amechelewa.

Unapaswa kuingia kwenye biashara ambayo kuna thamani unaitoa na thamani ambayo ni ya kudumu, haipitwi na wakati na wala siyo ya msimu.

3. Uhitaji.
Pamoja na kuwa na thamani unayotoa, kunapaswa kuwepo na uhitaji pia.
Lazima kuwe na watu ambao wana matatizo au mahitaji ambayo thamani unayotoa inatatua.
Na matatizo au mahitaji yao yawe makubwa kiasi kwamba hawawezi kuendelea kuyavumilia.
Lakini pia wanapaswa kuweza kumudu gharama za thamani unayowapatia.
Kwa kifupi unapaswa kuhakikisha soko la thamani unayotoa lipo.

Tengenza biashara ambayo inaleta majibu ya changamoto au mahitaji ambayo tayari watu wanayo.

4. Ukuaji.
Biashara inapaswa kuwa na fursa za ukuaji ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Ukuaji unaweza kuwa kulifikia soko kubwa zaidi au kuuza zaidi kwenye soko ambalo lipo.
Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kuanza na soko dogo, lakini linapaswa kukua ili biashara iweze kumudu kuwepo na idumu kwa muda mrefu.
Biashara haipaswi kuwa na kikwazo chochote kile kwenye ukuaji.
Na katika ukuaji wa biashara, gharama zinapaswa kuwa zinapungua ili faida zaidi iweze kutengenezwa.

Jenga biashara ambayo haina ukomo wowote kwenye ukuaji na kisha tumia kila fursa kuweza kuikuza zaidi.

5. Usimamizi.
Bila ya usimamizi mzuri, biashara haiwezi kukua. Na hata ikitokea imekua basi itaanguka vibaya sana.
Lazima kuwepo mfumo mzuri wa usimamizi na uendeshaji wa biashara, ili biashara iweze kujiendesha yenyewe hata kama mwanzilishi hayupo.
Yeyote anayepewa jukumu lolote kwenye biashara, anajua kabisa nini anapaswa kufanya na anapimwaje kwenye utekelezaji wake.
Mambo yote ya usimamizi wa biashara yanapaswa kutengenezewa mfumo ambao unakuwa sehemu ya biashara.

Jenga biashara yenye mfumo wa uendeshaji ili iweze kujiendesha bila hata ya uwepo wako.

6. Sifa (Brand).
Biashara nyingi kubwa ambazo tunaziamini leo kuna sifa fulani zimejenga ambayo tuna uhakika nayo.
Tunapoenda kwenye biashara hizo, hatuna wasiwasi juu ya sifa hiyo.
Mtu anaponunua simu ya iphone, hana mashaka juu ya ubora na usalama. Hiyo ndiyo sifa yake kuu.
Biashara zinazoshindwa hazina sifa yoyote ambayo inazitofautisha. Hazina kitu chochote ambacho inakisimamia na wateja kuiamini kwenye kitu hicho.

Wewe unapaswa kuchagua sifa ambazo biashara yako inapaswa kuwa nazo na kuzilinda kwa gharama yoyote ile. Eneo la sifa linapaswa kuwa la msimamo mkali, bora uingie gharama au hasara ila ulinde sifa ya biashara yako.

Rafiki, hizo ni hatua sita muhimu sana za kufuata ili kujenga biashara itakayodumu kwa muda mrefu na kufanikiwa sana.

Nikukaribishe kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambapo tunakwenda kuijenga misingi hii kwa kina na kuifanyia kazi kwa kipindi cha muongo mzima wa 2020 – 2030.

Katika semina hii utajifunza kwa hatua na kufanyia kazi haya ili biashara yako iweze kunufaika kwa kiwango kikubwa.

Hii ni semina yako rafiki yangu, semina ambayo hupaswi kuikosa kama kweli umedhamiria kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz