Rafiki yangu mpendwa,
Katika kipindi ambacho nimekuwa natoa huduma hii ya mafunzo, ushauri na ukocha, nimepata nafasi ya kufanya kazi na watu wengi.
Kitu kikubwa kabisa ambacho nimejifunza katika hilo ni hakuna kikwazo kikubwa kwenye safari ya mafanikio kama watu.
Watu wanaokuzunguka na unaotumia nao muda wako mwingi, wana athari kubwa mno kwenye mafanikio yako.

Nakumbuka mtu mmoja ambaye tulishauriana sana kuhusu uwekezaji na kukubaliana aanze kwa kuwekeza UTT na hatua zote tukapeana.
Lakini akawa hatekelezi. Tulipokuja kujadili tena ndiyo akaniambia alikuwa anaongea na wafanyakazi wenzake ambapo walimwambia huko ni kupoteza fedha.
Nilipomuuliza hao wafanyakazi wenzake wana uelewa kiasi gani kuhusu uwekezaji au wamewekeza wapi, hakuwa na majibu.
Mwingine tulishauriana kuhusu biashara gani aanze kwa mtaji aliokuwa nao. Tukaweka mikakati kabisa ya namna ya kupangilia mtaji huo ili hata akikutana na changamoto asipoteze kila kitu.
Cha kushangaza akaenda kufanya biashara nyingine tofauti kabisa, nilipomuuliza akasema aliona ndiyo inaweza kumlipa kwa haraka zaidi kuliko tuliyojadiliana awali.
Aliishia kupata hasara na tulipojadiliana tena kuhusu hilo nikagundua alitekwa na kelele za wengi kwamba hiyo ndiyo fursa inayolipa sana. Wengi ambao hata hawaifanyi, wanasikia tu na kusema.
Mwingine alikuwa na changamoto ya kuchelewa kuamka mapema asubuhi, kitu ambacho kilikuwa kinaathiri sana biashara yake.
Tukawa tunapeana mbinu mbalimbali za kukabiliana na hilo, lakini bado likawa linashindikana.
Katika kujadiliana zaidi nikagundua alikuwa kwenye mahusiano yenye changamoto, ambapo mara nyingi alikuwa akiongea na simu mpaka saa nane za usiku.
Mifano ni mingi mno, mno, lakini picha umeipata hapo.
Hata kwako pia, tukichunguza sasa, changamoto unazopitia sasa au ambazo umewahi kupitia huko nyuma, kwa sehemu kubwa zimeanza na wale wanaokuzunguka.
Baada ya kugundua hili, hata mfumo wangu wa ukocha umebadilika. Kabla hatujaanza kuhangaika na mambo magumu kwenye mafanikio ya mtu, tunaanza kwanza na wale wanaomzunguka.
Nimegundua hilo lina matokeo mazuri sana katika kumwezesha mtu kubadilika katika safari ya mafanikio.
Tatizo kubwa la jamii zetu ni kila mtu ni mshauri kwenye kila kitu.
Hakuna kitu ambacho watu hawana ushauri.
Na watu wanataka wakikupa ushauri uufuate, hata kama ni wa kijinga kabisa.
Wale wa karibu, huwa wana nguvu kubwa mno kwenye kutushawishi kukubaliana na ushauri wao.
Hili ni eneo kubwa tunalokwenda kufanyia kazi kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwenye semina hiyo unakwenda kupata njia tatu na za uhakika za kukabili hili.
Moja ni kukutana na watu sahihi ambao utashirikiana nao kwa karibu na wakusukume kufanikiwa zaidi.
Mbili ni utaweza kufanya usafi kwenye watu unaowapa kipaumbele kwenye maisha yako, kujua wapi ni sahihi na nani wa kumshirikisha mambo yako makubwa.
Tatu ni utajijengea ujasiri wa kuweza kusema hapana kwenye ushauri wowote wa kijinga ambao watu wanakupa, bila kuhofia au kujali wanakuchukuliaje.
Rafiki, watu wanaokuzunguka ni kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio yako.
Usikose kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili uweze kutengeneza watu sahihi kwa mafanikio yako.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz