Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wanaosema wanamiliki biashara siyo wakweli.
Wengi wanakuwa wamemililiwa na biashara zao.

Wengi waliopo kwenye biashara hawadanganyi hivyo kwa makusudi, bali hawajui tofauti ya kumiliki biashara na kumilikiwa na biashara.

Unamiliki biashara pale ambapo biashara inaweza kujiendesha yenyewe hata kama wewe haupo kwenye biashara moja kwa moja.

Na unamilikiwa na biashara pale ambapo biashara inakutegemea wewe kwa kila kitu, kama haupo, biashara haiwezi kwenda kabisa.

Kama biashara haiwezi kwenda bila ya uwepo wako hiyo siyo biashara, bali ni aina nyingine ya ajira. Maana hupati ule uhuru kamili unaopaswa kuupata ukiwa kwenye biashara.

Uhuru kamili unaoweza kupatikana kupitia biashara ni pale ambapo biashara inaweza kujiendesha hata kama wewe mwanzilishi haupo kabisa.

Biashara kujiendesha yenyewe siyo kitu kinachotokea kama ajali, bali ni kitu ambacho kinatengenezwa.

Kitu hicho kinatengenezwa kupitia mfumo wa kuendesha biashara.
Hii ni njia ya kuigeuza biashara kuwa mashine inayoweza kujiendesha yenyewe.

Kujenga mfumo kwenye biashara ni kitu muhimu sana lakini hakuna mahali popote kimekuwa kinafundishwa.

Wengi wanaingia kwenye biashara bila ya kuwa na uelewa na hili la mfumo, kinachotokea ni wanajenga biashara ambayo ni gereza kwao.
Biashara ambayo kadiri inavyofanikiwa ndivyo inavyozidi kuwabana.

Rafiki, kama tayari umeingia kwenye biashara na inakutegemea kwa kila kitu. Au kama unapanga kuingia kwenye biashara itakayokupa uhuru wa kipato na muda. Kuna fursa nzuri kwako kujifunza jinsi ya kujenga mfumo wa biashara itakayoweza kujiendesha yenyewe.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, kujenga mfumo wa biashara ni moja ya masomo makuu unayokwenda kujifunza.
Na hiyo ni sababu kubwa na muhimu kwako kuhakikisha hukosi semina hii bora na ya kipekee kwako.

Kwenye semina hii, utakwenda kujifunza hatua kwa hatua na kutengeneza mfumo wa biashara yako ambao utaenda kutekeleza tu.
Yaani unapotoka kwenye semina hii, unakuwa na ramani kamili ya kwenda kuendesha biashara yako ili isikutegemee wewe moja kwa moja.

Kujenga mfumo wa biashara ni jambo gumu na linalowasumbua wengi.
Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 utakwenda kujifunza kwa kina kuhusu hili na kuchukua hatua ili biashara yako iweze kunufaika.

Faida za kuendesha biashara kwa mfumo ni nyingi, ikiwepo kuiwezesha biashara kukua bila ukomo na hata kuweza kuiuza biashara kwa faida kubwa.

Rafiki, lengo lako ni kumiliki biashara na siyo kumilikiwa na biashara.
Hakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kufanikisha hilo la kumiliki biashara yenye mafanikio makubwa, uwe na uhuru kamili wa maisha yako, kwa upande wa kipato na muda.

Siku zimebaki chache za kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya kipekee kwako.
Kama bado hujajihakikishia nafasi ya kushiriki, chukua hatua leo hii ili usikose fursa bii ya kipekee kabisa kwako.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz