Rafiki yangu mpendwa,
Unapoianza safari ya mafanikio, huwa unachukua kila fursa inayokuja mbele yako.
Huwa unafanya mambo mengi ili kufika kwenye mafanikio makubwa unayoyataka.

Hii ni sawa kabisa mwanzoni kwa sababu bado unakuwa hujajua kipi kinaweza kufanya kazi na kukufikisha unakotaka kufika.

Lakini kadiri unavyokwenda na hali hiyo ya kukubali na kufanya mengi, mambo mawili makubwa yanajitokeza.

La kwanza ni kuwa na mambo mengi ya kufanya kuliko muda ambao unao. Hapa unakuwa umeelemewa na kuvurugwa kweli kweli, maana muda ni mfupi na mambo ni mengi.

La pili ni machache kati ya mengi unayofanya yanakupa matokeo mazuri na makubwa. Kama unafanya mambo 10, unagundua mawili yanakupa matokeo makubwa kuliko mengine nane ukiyachanganya pamoja.

Ni katika hatua hiyo ndiyo unapaswa kubadilika, kuondoka kwenye kujumlisha na kwenda kwenye kutoa.

Mabadiliko hayo yanahusisha kupunguza mambo ambayo mtu unayafanya, ili kuweka nguvu zako zote kwenye mambo machache yenye tija zaidi.

Hapo ndipo penye ugumu ambao umekuwa kikwazo kwa wengi kupata mafanikio makubwa zaidi.

Kufanya mambo mengi kunampa mtu mafanikio ya wastani.
Lakini kufanya mambo machache kwa kina, kunampa mafanikio makubwa zaidi.

Ishu ni utayari wa mtu kuacha kinachomlipa sasa kwa ajili ya kufanya zaidi kile kitakachomlipa baadaye.

Nani yupo tayari kumwacha mteja anayemlipa kwa sasa ili aweke nguvu zake kwa wateja wachache wanaolipa vizuri?

Hapo ndipo penye kitendawili cha mafanikio, ili upate zaidi lazima kwanza uwe tayari kupoteza.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 unakwenda kujifunza hili kwa kina na kuliishi kwa mwaka mzima wa mafanikio 2021/2022.
Kwani utachagua biashara moja tu ambayo ndiyo utafuatiliwa nayo kwa ukaribu kabisa.
Biashara hiyo ndiyo utakayoweka kila kitu ili iweze kuwa na mafanikio makubwa kabisa.

Ni kanuni ya asili kwamba nguvu zikikusanywa eneo moja zinaleta matokeo makubwa kuliko zikitawanywa.
Na unaweza kupima hilo kwa zoezi dogo, mwanga wa jua hauna ukali sana ukiwa umetawanyika.
Ila ukiukusanya sehemu moja kwa kutumia lensi, unakuwa na nguvu ya kuunguza na hata kuwasha moto.

Je ni eneo gani kwenye maisha yako ambalo unataka kuliwashia moto ili ufanye makubwa zaidi?
Je ni biashara ipi kati ya unazofanya unataka kuiwekea juhudi kubwa ili iwe na tija zaidi?
Je ni wateja wapi kati ya wengi unaowahudumia ambao unajua ukiweka juhudi kubwa kwao utapata matokeo mazuri?

Umeshapiga sana hatua za kujumlisha, kukimbizana na kila aina ya fursa.
Sasa ni wakati wa kupiga hatua za kutoa, kubaki na fursa chache ambazo zina manufaa makubwa.

Zoezi hilo ni gumu sana kulifanya peke yako, kwa sababu hutakuwa tayari kuacha kitu kinachokupa matokeo mazuri, hata kama ni madogo.

Na hii ndiyo sababu ya msingi kwako kuhakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, ambapo utapata mwongozo na usimamizi wa kuachana na mengi na kuhangaika na machache muhimu.

Hii siyo semina ya wewe kukosa kama umejitoa kweli kufanikiwa, maana safari ya mafanikio haijawahi kuwa rahisi.
Njoo twende pamoja kwenye safari hii ili tuweze kufanya makubwa zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz