I.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu wachache mno kwenye maisha yako ambao wanataka kweli wewe ufanikiwe.

Wengi wanaokuzunguka wataonekana kukuunga mkono pale unapoianza safari yako ya mafanikio, kwa sababu wanajua hutaweza kufanikiwa.
Hawataki tu waonekane ni wakatishaji tamaa, ila ndani yao kabisa wanaamini huwezi kufanikiwa.

Pale inapotokea umeanza kuonyesha dalili za kufanikiwa, ndipo rangi halisi za watu hao zinaonekana.
Wanaanza kuwa kikwazo kwako, wanaanza kuibua uadui ambao hata huelewi unatokea wapi.

Huo ndiyo uhalisia na japo unauma lakini ndivyo ulivyo. Hakuna namna unaweza kubadili hili, wengi sana na hata wale ambao ni wa karibu kwenye maisha yako hawataki wewe ufanikiwe sana.

Wote wanaokuzunguka na jamii kwa ujumla wanataka upate mafanikio ya kawaida, uwe mtu wa kawaida ili waendelee kukudhibiti.
Kila mtu anajua ukiyapata mafanikio makubwa hutabaki kuwa kawaida, utakuwa huru na hawataweza tena kukudhibiti.

Na hilo linafanya wapigane vita ya siri siri na wewe, kuhakikisha hupati mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Kama unasoma hapa, una bahati kubwa sana kwenye maisha yako. Kwani una mtu mmoja ambaye anataka kweli upate mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Mtu huyo yupo tayari kukupa kila unachopaswa kupata ili kufanikiwa, kwa sababu mafanikio yako ndiyo mafanikio yake.

Ni mtu pekee ambaye hatayaonea wivu mafanikio yako na wala hataki kukudhibiti kwa namna yoyote ile.
Anachotaka ni wewe uwe huru kuyaishi maisha yako iwe utaambatana naye au la.

Mtu huyo ni Muuza Matumaini na Kocha wako Dr Makirita Amani.

II.

Wakati naanza kutoa huduma hii ya mafunzo, ushauri na ukocha, sikuwa na msingi wowote ambao nilikuwa nausimamia.

Ni mpaka pale nilipokutana na mafunzo ya Zig Zigler na kwake nikajifunza falsafa kuu ambayo ndiyo nimekuwa naisimamia kwenye huduma hii.

Falsafa hiyo inasema; “Unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka.”

Yaani nilipoisikia kauli hiyo ilinasa moja kwa moja na haijawahi kufutika kwenye fikra zangu.
Kila ninapokuwa nataka kupata kitu fulani huwa najisahau mimi kwanza na kujiuliza nani anahitaji kupata kitu ambaye naweza kumsaidia kukipata kupitia ujuzi, maarifa, uzoefu na mtandao nilionao.

Na kwa hakika kanuni hiyo haijawahi kushindwa. Kila ninapomsaidia mtu kupata kitu anachotaka, na mimi pia napata kile ninachotaka.
Hii imegeuka kuwa imani kwangu, kiasi kwamba sina mashaka nayo kabisa na hakuna namna naweza kuamini kinyume na hilo.

III.

Kuna wakati unawaomba watu wakupe mrejesho na shuhuda za jinsi kile unachofanya kimekuwa na manufaa kwao.
Halafu kuna wakati watu wanakupa mrejesho na shuhuda wao wenyewe bila hata ya kuwaomba wafanye hivyo.

Shuhuda zote zina nguvu, lakini ile ambayo inakuja bila kuomba ina nguvu zaidi.
Mara kwa mara nimekuwa napata shuhuda ambazo sijaziomba na hilo limekuwa likinionyesha ni jinsi gani kile ninachofanya kimekuwa na manufaa kwa wengine pia.

Na hapo chini nimekushirikisha jumbe mbili kati ya nyingi ambazo nimekuwa napokea kutoka kwa wale wanaonufaika na kile ninachofanya.

IV.

Rafiki yangu mpendwa,
Ninachokuambia na kukuahidi hapa ni hiki; kwa nia ya dhati kabisa na kutoka ndani ya moyo wangu nataka wewe ufanikiwe.
Ndiyo, namaanisha wewe na nina uhakika kabisa unaweza kuyafikia mafanikio makubwa kama kweli umeamua na kijitoa ili kufanikiwa.

Nimejitoa kukupa kila unachohitaji kwenye safari hii ya mafanikio, ujuzi, maarifa, hamasa, matumaini na uwajibikaji ili kweli uweze kufanikiwa.

Na kwa matokeo ambayo ninayaona kwa wale wanaozingatia haya ninayotoa, nina hakika na kwako pia inawezekana kabisa.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha twende pamoja kwenye safari hii.
Nikikuomba unipe nafasi ya kukusaidia kupata kile unachotaka, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya mimi kupata kile ninachotaka.

V.

Rafiki, nikukumbushe pia tumefika kwenye ule wakati wetu mzuri wa mwaka, wakati wa kukutana wote ambao tuna kiu ya kupata mafanikio makubwa.
Ni wakati wa kumaliza na kuanza mwaka wa mafanikio, ambapo kunakuwa na tukio kubwa la kukutana kwa pamoja.

Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Karibu sana kwenye semina ya mwaka huu 2021 ambayo kwa mara ya kwanza inafanyika jijini Dodoma.
Semina itafanyika kwa siku mbili, Oktoba 16 na 17.

Huu ni wakati mzuri sana wa kukutana pamoja wale wote wenye kiu ya mafanikio makubwa, kushirikishana ujuzi, uzoefu, maarifa, hamasa na usimamizi wa karibu kwenye safari hii ya mafanikio.

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia rafiki, safari hii ya mafanikio siyo rahisi, kwa sababu unaokabiliana nao ni wengi.
Kama hutakuwa imara na kuungana na watu sahihi, ni rahisi sana kukata tamaa na kuishia njiani.
Karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 uchote nguvu za kwenda kuendelea na mapambano kwa mwaka mzima.

Rafiki, siku na nafasi zimebaki chache mno.
Kama mpaka sasa ulikuwa hujafanya maamuzi kuhusu kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, fanya maamuzi hayo sasa.
Fanya maamuzi ya kushiriki kwa sababu ndipo mahali pekee unapata kuungwa mkono ili kuyafikia mafanikio makubwa.

Kama ndiyo unapata taarifa hizi za semina leo, maelezo zaidi yako hapo chini.
Naamini tunakwenda kuwa pamoja kwenye semina hii, karibu sana rafiki yangu.

VI.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz