Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wanapokuwa kwenye ajira, huwa wanaona na kwa jinsi gani hawapo huru.

Mtu anaweza kuweka juhudi sana kwenye kazi na akazalisha matokeo makubwa, lakini bado kipato chake kinabaki vile vile.

Na inapokuja kwenye muda, ndiyo kabisa hana mamlaka juu ya muda wake.
Mwajiri anamiliki muda wake wote wa kazi na wakati mwingine hata muda wa ziada.

Baadhi hupata hasira kwa kukosa huko uhuru na kuamua kwenda kujiajiri.
Wanakwenda kujiajiri kwa lengo la kuwa huru, kwenye kipato na hata kwa muda.

Na siku za kwanza za kwenye kujiajiri zinakuwa za raha kama fungate.
Kwani mtu akiweka juhudi zaidi matokeo anayaona wazi, kipato chake kinaongezeka zaidi.
Na hapo anajiambia kumbe alikuwa anajichelewesha tu mwenyewe.

Basi anasukumwa kuweka juhudi zaidi, ili aendelee kuongeza kipato zaidi.
Na hapo ndipo fungate linaisha, raha ya mwanzo inakatika na uhalisia unakuja wazi.

Kadiri kile ambacho mtu anafanya kinakua, ndivyo anavyogundua kumbe hayuko huru kama alivyodhani.

Anaona kabisa fursa ya kufanya zaidi ili kipato kiongezeke, lakini kwa sababu kila kitu kinamtegemea, anakuwa hawezi kufanya kila kitu.
Na hapo yeye mwenyewe anakuwa kikwazo kwenye ukuaji wake.

Mbaya zaidi inakuja kwenye muda, japo mtu alidhani akijiajiri atakuwa huru na muda wake, kuutumia anavyotaka, anakuja kugundua hilo pia siyo kweli.

Muda wake unakuwa ndiyo kipato chake, akiacha kufanya tu kile anachofanya, fedha nazo zinaacha kuingia.

Na hapo ndipo mtu anajikuta kwenye utumwa mbaya mno kwenye maisha yake, akifanya kazi kama punda na asiweze hata kusafiri maana kila kitu kinamtegemea.

Huko ndiyo kujiajiri, mtego ambao wengi hunasa wakati wanatafuta uhuru.

Uhuru wa kweli kwenye maisha unapatikana kwa kumiliki biashara.
Biashara ni kitu kinachoweza kujiendesha chenyewe na kwa faida hata kama wewe mmiliki haupo moja kwa moja.

Biashara inakupa uhuru wa kifedha, kwani inakuwa na fursa za kukua hila ya ukomo.
Lakini pia inakupa uhuru wa muda kwa sababu haikutegemei wewe ndiyi iweze kwenda.

Kuna tofauti kubwa kati ya kujiajiri na kumiliki biashara ambayo wengi huwa hawaizingatii na hilo kuwa kikwazo kwao.

Unapojiajiri unaweza kuona kama uko huru, ni mpaka pale unapokuja kugundua huwezi kuwa na mapumziko maana kipato chako pia kitakauka.
Maana kile unachofanya kinakutegemea wewe kwa kila kitu, usipokuwepo mambo hayawezi kwenda.

Unapomiliki biashara unaweza kuondoka kwenye biashara hata kwa mwaka mzima, ukarudi na kukuta biashara imekua zaidi bila hata ya uwepo wako.
Kwa sababu biashara inakuwa na mfumo wa kuweza kujiendesha yenyewe bila ya kutegemea uwepo wako.

Rafiki, una bahati kubwa sana kwamba unayo fursa nzuri ya kujifunza jinsi ya kujenga biashara inayoweza kujiendesha yenyewe bila ya kukutegemea wewe moja kwa moja.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambapo utapata nafasi ya kujifunza kwa kina kuhusu kutengeneza mfumo wa biashara yako ili iweze kukupa ule uhuru ambao unautaka.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, kujenga mfumo wa biashara ni moja ya masomo makuu unayokwenda kujifunza.
Na hiyo ni sababu kubwa na muhimu kwako kuhakikisha hukosi semina hii bora na ya kipekee kwako.

Kwenye semina hii, utakwenda kujifunza hatua kwa hatua na kutengeneza mfumo wa biashara yako ambao utaenda kutekeleza tu.
Yaani unapotoka kwenye semina hii, unakuwa na ramani kamili ya kwenda kuendesha biashara yako ili isikutegemee wewe moja kwa moja.

Kujenga mfumo wa biashara ni jambo gumu na linalowasumbua wengi.
Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 utakwenda kujifunza kwa kina kuhusu hili na kuchukua hatua ili biashara yako iweze kunufaika.

Faida za kuendesha biashara kwa mfumo ni nyingi, ikiwepo kuiwezesha biashara kukua bila ukomo na hata kuweza kuiuza biashara kwa faida kubwa.

Rafiki, lengo lako ni kumiliki biashara na siyo tu kujiajiri.
Hakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kufanikisha hilo la kumiliki biashara yenye mafanikio makubwa, uwe na uhuru kamili wa maisha yako, kwa upande wa kipato na muda.

Siku zimebaki chache za kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya kipekee kwako.
Kama bado hujajihakikishia nafasi ya kushiriki, chukua hatua leo hii ili usikose fursa bii ya kipekee kabisa kwako.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz