Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya manufaa makubwa unayokwenda kuyapata kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni kukutana na vitabu vipya pamoja na waandishi wa vitabu hivyo.
Kukutana na mwandishi wa kitabu ana kwa ana ni nafasi ya kipekee sana, kwani unaweza kumwuliza swali lolote kuhusu yale aliyoandika kwenye kitabu.
Mchakato wa kuandika kitabu siyo rahisi, hivyo mtu anapokamilisha kuandika kitabu, hawi mtu yule yule aliyekuwa kabla hajaandika.
Zoezi zima la uandishi linambadili sana mtu.
Unapokutana na mwandishi ana kwa ana, unapata nafasi ya kujifunza kupitia mabadiliko yaliyosababishwa na uandishi.
Mimi kama mwandishi na ambaye pia nimewakochi waandishi wengi kwenye kuandika vitabu, najua jinsi mchakato wa uandishi ulivyo mgumu na wenye kuleta mapinduzi kwa mtu anayeupitia.
Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambapo utakutana na vitabu hivi sita pamoja na waandishi wake.
1. MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.
Hiki ni kitabu kilichoandikwa na Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.
Vitabu vingi kuhusu mafanikio huwa vimeegemea upande wa hamasa zaidi. Hivyo watu wanapata maarifa na hamasa, lakini wanakosa mwongozo sahihi wa kufanyia kazi.
Hilo ndilo unalokwenda kupata kwenye kitabu hiki, ambacho ni zana muhimu mno kwenye safari yako ya mafanikio.
Hiki siyo kitabu cha wewe kukosa kama kweli unayataka mafanikio makubwa.

2. UHUSIANO WA MKRISTO NA MAFANIKIO.
Hiki ni kitabu ambacho kimeandikwa na Mwl Jofrey Sanga.
Kuna mapokeo potofu kwamba watu wa dini hawapaswi kufanikiwa na kuwa matajiri. Kwamba wakifanikiwa wataiacha imani yao na kwenda kwenye mambo ya dunia.
Kitabu hiki kinatuonyesha jinsi hilo lilivyo potofu na kutupa mafundisho sahihi ya jinsi mtu wa imani anaweza kuwa na mafanikio makubwa na bado akailinda imani yake.
Mistari mingi ya Biblia ambayo imekuwa inatafsiriwa kwa upotofu imetafsiriwa kwa usahihi kwenye kitabu hiki.
Kitu kikubwa utakachokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki ni kwamba Mungu anataka sana na ameweka uwezo kwa kila mtu wake kufanikiwa. Ni wewe ujue uwezo huo na kuutumia.
Nimepata nafasi ya kuandika dibaji ya kitabu hiki, ni kizuri na muhimu kwa maisha yako, hakikisha hukikosi.
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kwa namba 0758014675 kujua jinsi ya kukipata.

3. AMSHA UWEZO WAKO HALISI.
Kitabu hiki kimeandikwa na Alfred Mwanyika.
Kitabu kinatuonyesha jinsi tunavyotumia sehemu ndogo mno ya uwezo mkubwa ulio ndani yetu.
Haijalishi umefanya nini mpaka sasa, unachopaswa kujua umekuwa unatumia chini ya asilimia 10 ya uwezo wako mkubwa.
Kama ni shamba, una heka 10, ila umekuwa unalima moja pekee.
Mwandishi ametuonyesha jinsi ya kuamsha uwezo huo uliolala ndani yetu na kuweza kufanya makubwa.
Usikubali kufa na uwezo huo mkubwa ulio ndani yako, jifunze jinsi ya kuuamsha na kuutumia.
Nimepata nafasi ya kuandika dibaji ya kitabu hiki, siyo cha wewe kukosa.
Wasiliana na mwandishi kwa namba; 0752206899 kupata kitabu.

4. IJUE NJAA YA WANANDOA.
Kitabu hiki kimeandikwa na Mwl Deo Kessy.
Kwenye kitabu hiki mwandishi anatuonyesha jinsi changamoto kubwa za kwenye ndoa zinatokana na njaa ambayo kila mwanandoa anayo, lakini mwenzake hajui.
Hivyo pale wanandoa wanapojua njaa ambayo wenza wao wanayo na kuwashibisha, ndoa zinakuwa na utulivu na maelewano makubwa.
Hiki ni kitabu muhimu kwa kila aliyepo kwenye ndoa kukisoma, kwa sababu kuna mambo madogo madogo sana ambayo watu wamekuwa wanayapuuza, ila ndiyo yenye nguvu ya kujenga au kubomoa ndoa.
Nilipata pia nafasi ya kuandika dibaji kwenye kitabu hiki, ambapo mimi mwenyewe nimejifunza mengi, hivyo usikikose. Wasiliana na mwandishi kwa namba 0717101505.

5. UNAWEZA KUWA UNAYEMTAKA.
Kitabu hiki kimeandikwa na Felician Meza.
Kwenye kitabu hiki mwandishi ametushirikisha jinsi tunavyoweza kuyabadili maisha yetu, kutoka vile tulivyo sasa kwenda kuwa vile tunavyotaka. Tukitumia kauli ya vijana wa mjini, wanasema ni ‘kupindua meza’.
Je huridhishwi na aina ya maisha uliyonayo sasa? Je unatamani kuwa tofauti na ulivyo sasa? Hicho ni kitu kinachowezekana kabisa na kwenye kitabu hiki unapata njia za kuwezesha hilo.
Nimepata nafasi ya kukihariri kitabu hiki, kwa hakika hupaswi kukikosa. Wasiliana na mwandishi kwa namba 0786026109.

6. FUNGATE YA MILELE.
Kitabu hiki kimeandikwa na Mwl Hamis Msumi.
Tumezoea watu wanapooana kwenda kwenye fungate (honeymoon) kwa kipindi kifupi.
Hicho ni kipindi ambacho huwa hawakisahau, kwa sababu kinakuwa kipindi cha mapenzi na maelewano makubwa.
Lakini baada ya fungate kuisha, mambo huanza kubadilika na yale mapenzi na maelewano ya mwanzo yanapotea. Hilo linapelekea ndoa kuingia kwenye migogoro mikubwa na hata kupelekea kuvunjika.
Mwandishi ametuonyesha mambo hayapaswi kuwa hivyo, kwani fungate inaweza kuwa ya milele.
Mwandishi ametufundisha jinsi ya kuweza kujenga maelewano mazuri kwenye mahusiano ili yawe tulivu na tunayoyafurahia.
Usikose kitabu hiki, kitakusaidia kuboresha siyo tu mahusiano ya ndoa, bali mahusiano yako yote kwenye maisha.
Nilipata nafasi ya kumsimamia mwandishi kwa karibu wakati anaandika kitabu hiki, hatua kwa hatua na nikuambie tu kwamba hiki siyo kitabu cha wewe kukosa.
Wasiliana na mwandishi kwa namba 0784607524.

Rafiki, hivi ni vitabu 6 utakavyovipata kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 na kukutana na waandishi wake moja kwa moja.
Kutakuwa na vitabu vingine kutoka kwa waandishi wengine pia ambao nitaendelea kushirikisha.
Kwa kushiriki semina hii, unapata nafasi ya kukutana na waandishi hao wote kwa pamoja, nafasi ambayo ni nadra sana.
Njoo kwenye semina hii ukiwa na swali moja kubwa linalokusumbua sana kwenye kila eneo la maisha yako na utapata nafasi ya kuwauliza waandishi moja kwa moja na wakakupa ufafanuzi.
Na kama unataka kuandika kitabu chako pia, basi karibu kwenye semina, utapata mafunzo, hamasa na usimamizi wa karibu katika kukamilisha hilo.
Kwa vitabu nilivyoshirikisha hapo juu, utaona vingi nimeandika dibaji, kuvihariri na kusimamia kwa karibu kwenye uandishi wake, hivyo nina uhakika wa ubora wa maarifa yaliyo ndani ya vitabu hivyo.
Unaweza kuwa unapenda nikusimamie kwenye uandishi wa kitabu chako, au kukihariri au kuandika dibaji.
Unaweza kupata nafasi hiyo kwa kushiriki kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Karibu sana kwenye semina hii, zimebaki siku 3 pekee kupata nafasi, chukua hatua sasa, tuwasiliane kwa namba 0717 396 253.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz