Rafiki yangu mpendwa,
Nilitoa zawadi ya watu kuja na wenza wao kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Wengi wamechukua nafasi hiyo na tayari wameweka nafasi ya kuja na wenza wao.

Hilo linatupa fursa nyingine nzuri ambayo tunakwenda kuifanyia kazi wakati wa semina.
Fursa hiyo ni kuwa na chakula cha pamoja kwa wanandoa (Couple’s Dinner).
Tukio hilo litafanyika jioni ya siku ya jumapili tarehe 17/10/2021 baada ya kumalizika kwa semina yetu ya siku mbili.

Huu utakuwa wakati mzuri wa wanandoa kukaa pamoja na kujenga timu imara ya mafanikio. Kwani kama ambavyo nimekuwa nashirikisha, mwenza wako ana nguvu kubwa ya kujenga au kubomoa mafanikio yako.

Kwa mafanikio makubwa tunayoyapigania, wenza wetu wanapaswa kuwa upande wetu mara zote, hata pale dunia nzima inapokuwa inatupinga.
Lakini hilo haliwezi kutokea tu, bali linajengwa.
Na katika chakula hiki cha pamoja, tunapata nafasi ya kufanyia kazi hilo.

Kwenye tukio hilo tutapata pia mafunzo ya kina ya mahusiano kutoka kwa waandishi ambao wametafiti na kubobea kwenye eneo la mahusiano, hasa ya ndoa.

Mwl Hamisi Msumi atatufundisha kwa kina jinsi ya kuwa na FUNGATE YA MILELE. Hili litatuwezesha kuwa na utulivu mkubwa kwenye mahusiano na nguvu zetu zote kupeleka kwenye kupambania mafanikio.

Mwl Deo Kessy atatuonyesha njaa ya wanandoa na jinsi ya kuishibisha ili ndoa zetu ziweze kwenda vizuri na zisiwe kikwazo kwa mafanikio yetu.

Na Mwanasayansi Felician Meza atatuonyesha kwa nini ndoa siyo ndoano, ili tuache kutumia ndoa kama kikwazo bali ziwe chachu na sababu ya sisi kufanikiwa.

Kama mahusiano ya ndoa hayajakaa vizuri, nguvu na muda wako mwingi utapotelea kwenye kuhangaika na changamoto hizo za mahusiano, nguvu ambazo hutaweza kuzitumia kwenye kupambania mafanikio.

Hivyo eneo la mahusiano ya ndoa linapaswa kwenda vizuri ili mtu uweze kuweka nguvu, muda na umakini wako wote kwenye mafanikio.
Mwenza wako anapaswa kuelewa ugumu wa hii safari na kuweza kukuelewa pale unapokuwa hupatikani kwa urahisi.

Njoo na mwenza wako kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ili muweze kujenga timu imara ambayo haiwezi kuangushwa na chochote.
Kama nyinyi wawili mtaelewana na kushirikiana kwa uaminifu mkubwa kwenye hii safari ya mafanikio, hakuna chochote kinachoweza kuwaangusha.

Zawadi ya kuja na mwenza kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA bado ipo, wasiliana na mimi sasa kwa namba 0717 396 253 ili upate nafasi hiyo.

Rafiki, hili ni tukio la kipekee na linalofanyika mara moja tu kwa mwaka. Katika kipindi hicho unaweza kujenga mengi kwa wakati mmoja, kuanzia maarifa ya mafanikio, hamasa ya kufanikiwa na kuboresha mahusiano yako pia.

Huenda hamjawahi kwenda mbali na mwenza wako kwa muda mrefu, mmekuwa kwenye mazingira hayo hayo ambayo mmeshayazoea sana. Kushiriki semina hii na mwenza wako ni moja ya njia za nyinyi wawili kubadili mazingira yenu na kupata wakati wa kuwa pamoja, peke yenu.
Mnaweza kukaa bila ya usumbufu unaowazunguka kila siku na kuweka mipango mikubwa kwenu.

Hii siyo fursa ya kukosa, wahi leo nafasi yakushiriki semina wewe na mwenza wako, ili muweze kujenga timu sahihi ya mafanikio.

Kama bado hujachukua hatua za kupata nafasi ya kushiriki semina, chukua sasa maana zimebaki siku mbili tu. Maelezo kamili ya semina yako hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz