Rafiki yangu mpendwa,
Kwa muda mrefu nimekuwa nakupa taarifa za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itafanyika Dodoma Oktoba 16 na 17.

Na kwa siku 30 sasa nimekuwa nakupa sababu kwa nini hupaswi kabisa kukosa semina hii. Kwa sababu ni tukio muhimu mno kwa kila mwenye kiu ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yake.

Leo napenda kukutaarifu kwamba imebaki siku moja tu ya kupata nafasi ya kushiriki kwenye semina hii.
Kesho tarehe 01/10/2021 ndiyo siku ya mwisho kabisa kupata mafasi hiyo.

Rafiki, kama sasa bado hujachukua hatua ya kukamilisha malipo ya ada ili ushiriki semina, fanya hivyo leo hii.
Usisubiri mpaka siku ya mwisho, kwani wengi wanaweza kupanga kukamilisha siku hiyo na pakawa na changamoto.

Ili kuepuka changamoto mbalimbali zisiwe kikwazo kwako kujihakikishia nafasi hiyo ya kushiriki semina, kamilisha malipo yako leo hii.

Rafiki, kwa mara ya mwisho nikukumbushe mambo 30 utakayokuwa umeamua kuyakosa kama hutachukua hatua ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.

1. Utakuwa umechagua kutokufanya uwekezaji bora kabisa kwako, ambao marejesho yake ni mara 10 ya kile ulichowekeza.

2. Utakosa nafasi ya kupata usimamizi wa karibu wa Kocha kwa kipindi cha mwaka mzima. Usimamizi huo una nguvu ya kukusukuma na kuhakikisha hukati tamaa.

3. Utakosa mtandao sahihi wa kimafanikio na kuendelea kuzungukwa na watu wasio na nyuma wala mbele kwenye eneo la mafanikio. Watu wengi wanaokuzunguka wanakurudisha nyuma.

4. Utakosa uwajibikaji katika kuyafanyia kazi  malengo na mipango yako. Kupanga ni rahisi, kutekeleza ni ngumu. Kama huja mfumo wa uwajibikaji, utaishia njiaji.

5. Utaendelea kutawanya nguvu zako kwenye mambo mengi yasiyo na tija kwako, kitu ambacho kitakuzuia usipate mafanikio makubwa. Kwa kushiriki semina utachagua machache muhimu utakayoyapa nguvu zako zote ili upate matokeo makubwa.

6. Utashindwa kuvunja laana ya ukuaji wa biashara, kwa biashara yako kukusumbua sana pale inapokua kwa sababu inakutegemea kwa kila kitu. Kwenye semina utajifunza jinsi ya kuvunja hilo.

7. Utakosa ubatizo wa uhakika wa mafanikio, kitu ambacho kitaifanya safari yako kuwa ngumu. Kwa kushiriki semina utapata ubatizo huo wa uhakika kitu kitakachokupa nguvu ya kupambana mpaka ufanikiwe.

8. Utakosa nafasi ya kuzijua na kuzitumia hatua sita za kupata chochote unachotaka. Hizo utajifunza kwa vitendo kwenye semina.

9. Utashindwa kubadili fikra zako kwa sababu hujayabadili mazingira yako. Kwa kusafiri kuja kwenye semina, utakuwa umeyabadili mazingira yako kitu kinachobadili fikra zako.

10. Utashindwa kujenga hamasa inayodumu kila siku kwenye maisha yako.  Utaendelea na ile hali ya kupata hamasa leo na kesho kuwa imeisha.

11. Utashindwa kujenga biashara inayodumu vizazi na vizazi kwa kuwa unakosa mfumo mzuri wa kuendesha biashara yako. Hilo utajifunza kwa vitendo kwenye semina.

12. Utakosa nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine, ambao wamepitia magumu kama yako, lakini wameweza kufanya makubwa. Kwa kuwasikia wengine wakitoa shuhuda zao, litakupa hamasa kwamba na wewe unaweza.

13. Utashindwa kutengeneza timu sahihi ya watu wanaokusukuma ili ufanikiwe zaidi. Kwa kuendelea kuzungukwa na wanaokuzunguka sasa, utaendelea kupata unachopata sasa.

14. Utamilikiwa na biashara yako badala ya wewe kuimiliki biashara. Kumilikiwa na biashara ni pale inapokutegemea kwa kila kitu, ambapo inakunyima uhuru kabisa. Kwenye semina utajifunza jinsi ya kuvunja hilo.

15. Utakosa vitu vitatu muhimu unavyohitaji sana ili ufanikiwe, COMMITMENT, DEDICATION NA ACCOUNTABILITY. Maarifa pekee hayatoshi ufanikiwe, unapaswa kuweka vitu hivyo vitatu ambavyo utajifunza kwa kina kwenye semina.

16. Utashindwa kupunguz yale yasiyo muhimu kwako, utaendelea kukusanya mengi ambayo hayatakusaidia. Kushiriki semina kutakufundisha mambo ya kuacha kufanya ili ufanye vizuri machache muhimu.

17. Utakosa kuambatana na mtu mwenye nia ya dhati wewe ufanikiwe kabla hata yeye hajafanikiwa. Wajibu wangu wa kwanza ni wewe ufanikiwe na hilo nakwenda kulifanyia kazi kwa kina kwenye semina na kwenye ufuatiliaji wa baada ya semina.

18. Utashindwa kujua tofauti ya kujiajiri na kumiliki biashara. Utadhani upo kwenye biashara kumbe umejiajiri tu, kitu kinachokuwa kikwazo kikubwa kwako kupata mafanikio makubwa. Kwenye semina utajua kwa undani.

19. Utazikosa hatua tano za kujenga biashara inayojiendesha kwa mfumo na kukupa wewe uhuru. Hatua hizo utajifunza kwenye semina pekee.

20. Utakosa mambo 12 ambayo nimejitoa kweli kuwapa wale wanaotaka mafanikio, maana ndiyo wameyaomba. Kwenye semina tutaanza kuyafanyia kazi.

21. Utashindwa kuweka mpango wako wa mafanikio unaoendana na wewe. Kwa sehemu kubwa mafanikio unayohangaikia sasa hayaendani na wewe, umeiga tu kwa wengine. Shiriki semina ili utengeneze mpango sahihi kwako.

22. Utakuwa umeshindwa kufanya uwekezaji muhimu sana ambao huwezi kuupoteza. Maarifa na mtandao utakaojenga kwenye semina ni uwekezaji ambao huwezi kuupoteza kwa namna yoyote ile.

23. Utashindwa kuzifanyia kazi tabia tano za biashara inayodumu kwa muda mrefu. Biashara nyingi hufa mapema kwa kukosekana kwa misingi mizuri mwanzoni, njoo ujifunze misingi hiyo kwenye semina.

24. Unakosa fursa ya kuuliza na kupata majibu ya maswali mbalimbali yanayokuwa yanakutatiza kwenye safari yako ya mafanikio. Kwenye semina utapata nafasi nzuri ya maswali yako yote kujibiwa.

25. Utakosa nafasi ya kukaa na kocha ana kwa ana na kupitia mpango unaoenda kufanyia kazi kwenye mwaka wako wa mafanikio. Njoo kwenye semina upate nafasi hiyo.

26. Unakosa fursa nzuri ya kuja na mwenza wako, ambapo mtatengeneza timu nzuri ya mafanikio. Mwenza wako ni mshirika muhimu wa mafanikio yako, anapaswa kuijua misingi sahihi.

27. Unakosa fursa ya kufanya mazoezi ya pamoja na wanamafanikio wengine. Mazoezi ni sehemu muhimu ya mafanikio. Kwenye semina tutakuwa na mazoezi ya pamoja.

28. Utakosa fursa ya kukutana na waandishi wa vitabu vipya zaidi ya sita vitakavyokuwepo kwenye semina.

29. Utakosa fursa ya chakula cha jioni kwa wanandoa, sehemu muhimu ya kuboresha mahusiano ili uweze kuweka nguvu zako kwenye mafanikio.

30. Unakosa msukumo wa kwenda kufanya makubwa kwenye safari yako ya mafanikio. Kushiriki kwenye semina hakutakuacha vile ulivyo sasa, bali kutakupa msukumo mkubwa mno wa kuweka juhudi kwenye kile unachotaka.

Rafiki, usikubali kukosa hayo na mengine mazuri ambayo unaweza kuyapata kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 pekee.
Imebaki siku moja tu, lakini usisubiri mpaka siku ya mwisho, chukua hatua leo hii ili ujihakikishie nafasi yako na usikose hayo mazuri.

Kama bado hujajipatia nafasi ya kushiriki semina, chukua hatua sasa. Maelezo muhimu yako hapo chini.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz