Rafiki yangu mpendwa,
Kwa zaidi ya miezi mitatu nimekuwa nakupa taarifa kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 itakayofanyika Dodoma.
Nimekueleza manufaa yote unayokwenda kuyapata kwa kushiriki semina hii, ambayo ni mengi na muhimu sana kwenye safari yako ya mafanikio.
Pia nimekuwa majibu ya maswali mbalimbali uliyokuwa unauliza kuhusu tukio hilo la kipekee mno kwenye safari ya mafanikio.
Napenda kuchukua nafasi hii kukutaarifu kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kabisa kupata nafasi ya kushiriki semina hiyo muhimu.
Leo tarehe 01/10/2021 ndiyo siku ya mwisho kukamilisha malipo ya ada ya kushiriki kwenye semina ili uweze kupata nafasi ya kushiriki.

Nikukumbushe kwamba semina hii ni muhimu sana kwako kwenye safari ya mafanikio.
Na kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha, nakwenda kuweka muda wangu mwingi zaidi kufanya kazi na mtu mmoja mmoja mpaka kweli aweze kuleta matokeo ya tofauti kwenye maisha yake.
Hii siyo tu semina ya kushiriki na kutoka ukiwa umefurahia kujifunza na kupata hamasa. Bali hii ni semina ambayo kwa kushiriki, lazima ulete matokeo ya tofauti kwenye maisha yako.
Maisha yako hayatabaki kama yalivyo sasa baada ya kushiriki semina.
Hivyo usiikose kama unataka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.
Wito wangu wa mwisho kwako rafiki yangu ni chukua hii nafasi, usiruhusu chochote kiwe kizuizi kwako kushiriki semina hii. Kwani ukiruhusu chochote kikuzuie, unakuwa umeiambia dunia kwamba upo tayari kuzuiwa na chochote ili usifanikiwe.
Na ukishaiambia dunia hivyo, itakuletea kila aina ya kikwazo ili kuhakikisha hufanikiwi.
Ionyeshe dunia leo kwamba hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa kwa kuhakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021. Chukua hatua leo ya kukamilisha ada yako ili ujihakikishie nafasi yako.
Rafiki, nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina, tuweze kukaa pamoja, kujifunza, kuhamasika na baada ya hapo kwa mwaka mzima tufanye kazi kwa karibu ili uweze kuleta mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako.
Karibu sana rafiki yangu, hutajutia kwa kushiriki semina hii na pia hutajisamehe kwa kuikosa, maana utakuwa umechagua kukosa mambo mazuri na yenye manufaa kwako.
Usikubali kuwa na majuto, una nafasi sasa ya kuchukua hatua ili ushiriki semina hii.
Kumbuka nafasi hiyo ni leo tu, hivyo chukua hatua sasa hivi.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz