2603; Mbona kila mtu anafanya?
Uzuri wa ukweli ni kwamba huwa haujali watu wanauchukuliaje.
Ukweli huwa hautumii nguvu kuwalazimisha watu wakubaliane nao.
Bali huwa unabaki kuwa ukweli.
Uongo huwa unatumia nguvu kubwa sana kuhakikisha kwamba unakubalika.
Unakimbilia kuwateka wengi ukijua wengi ni sehemu nzuri ya kujificha na kukubalika zaidi.
Ndiyo maana watu huwa ni rahisi sana kufanya kitu kwa sababu wanaona kila mtu anakifanya kitu hicho.
Upo mpaka usemi kwamba wengi wape na mwingine penye wengi hapaharibiki neno.
Kitu hakiwi sahihi kwa sababu wengi wanakifanya au wamekikubali.
Kitu huwa sahihi kama ni kweli.
Uongo hauwi ukweli kwa sababu wengi wanaukubali.
Na ukweli hauwi uongo kwa sababu wengi wanaukataa.
Huwa ni swala la muda tu kabla kila kitu hakijawa wazi hadharani.
Hatua ya kuchukua;
Usiangalie kundi kubwa la watu linafanya nini ndiyo na wewe ufanye.
Bali angalia ukweli ni upi na ufuate huo.
Kama siyo kweli, hata kama kila mtu anafanya, wewe usifanye.
Unaweza kuona kama unapitwa, lakini kuna ubaya gani kupitwa na wanaoenda kupotea?
Tafakari;
Kufuata mkumbo kumesababisha wengi kufanya maamuzi ambayo baadaye huja kuyajutia.
Kila unapojikuta upo upande wa wengi, ni wakati wa kujitathmini na kuona kama uko upande sahihi au la.
Usihadaiwe na wingi, wewe angalia ukweli.
Kocha.
Usidanganyike na wingi, wewe angalia ukweli. Asante Sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante sana kwa ukurasa huu
LikeLike
Karibu
LikeLike