#SheriaYaLeo (155/366); Dhibiti mwonekano wako.
Kwenye maisha watu wanakuhukumu na kukuchukulia kutokana na mwonekano wako.
Kwa kuwa watu hawana muda wa kuchunguza kwa ndani, wanachukulia mwonekano wako wa nje ndivyo ulivyo kwa ndani.
Ili watu wakuchukulie kwa namna sahihi kwako, unapaswa kutengeneza mwonekano wa nje ambao unawajengea picha hiyo.
Jiweke vile unavyotaka watu wakuchukulie na hilo litapunguza usumbufu wa watu kukuchukulia kwa namna isiyo sahihi kwako.
Usiseme huwezi kufanya hivyo kwa sababu utakuwa unaishi maisha ya maigizo.
Kwani maisha yote ni maigizo, kila mmoja akiigiza kwa namna yake ili kupata kile anachotaka.
Hivyo kama na wewe unataka kupata unachotaka, lazima uigize kwa namna hiyo ili kuwashawishi watu wakupe unachotaka.
Wakati mwingine unahitaji kutengeneza siri au mkanganyiko wa aina fulani ili watu wasiweze kukuelewa au kukutabiri.
Kadiri ambavyo watu hawakuelewi, ndivyo wanakufuatilia zaidi na hilo kukupa kile unachotaka kutoka kwao.
Usiwape watu mwonekano mmoja unaowafanya wakuzoee au waweze kukutabiri, kila wakati kuwa mbele zaidi kwa kuwa na mwonekano wa tofauti.
Sheria ya leo; Kamwe usiruhusu watu wajione wameshakuelewa na kukuzoea. Kila mara tengeneza mwonekano unaowafanya watu wakuchukulie vile unavyotaka wewe na siyo wanavyotaka wao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji