#SheriaYaLeo (281/366); Tofauti ya hisia na mantiki.

Watu wengi hutumia maneno hisia na mantiki bila kuelewa maana yake halisi.
Watu huona wale wasiokubaliana nao kama wanatumia hisia badala ya mantiki.

Tunachopaswa kujua ni kwamba sisi binadamu wote ni viumbe wa kihisia.
Huwa tunaathiriwa na hisia mbalimbali ambazo zinachochea fikra zinazotufanya tujisikie vizuri.

Watu wa mantiki huwa wanalielewa hilo na hivyo kuhakikisha wanazitenganisha fikra na hisia zao kabla hawajafanya maamuzi.
Hilo linawawezesha kufanya maamuzi ya mantiki.

Watu wa hisia huwa hawawezi kutenganisha fikra na hisia zao, huwa wanakimbilia kufanya maamuzi kulingana na msukumo wanaokuwa nao, ambao mara nyingi unatokana na hisia.
Hilo ndiyo linapelekea wafanye maamuzi ya hisia.

Tofauti kuu ya watu wa hisia na mantiki ni kwenye kujitambua.
Watu wa mantiki wanatambua jinsi hisia zinavyoathiri fikra zao na kuhakikisha wanazitenganisha kabla ya kufanya maamuzi.
Wati wa hisia hawatambui jinsi hisia zinavyoathiru fikra zao, hivyo wanakimbilia tu kufanya maamuzi kutokana na msukumo wanaokuwa nao ndani yao.

Sheria ya leo; Unajipimaje kwenye tofauti hiyo ya mantiki na hisia? Je unatambua fikra zako zinaathiriwa na hisia na kujaribu kuzitenganisha kabla ya kufanya maamuzi? Au umekuwa unakimbilia tu kufanya maamuzi kutokana na msukumo wa kihisia unaokuwa nao?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji