2802; Wape wanachotaka.
Naweza kusema kwenye haya maisha kama hujafanikiwa, chanzo kikubwa ni ubinafsi.
Kwenye maisha unashindwa pale unapojiangalia wewe mwenyewe zaidi ya unavyowaangalia wengine.
Pale unapoweka maslahi yako mbele na kupuuza ya wengine.
Utakazana sana kupata unachotaka, lakini hutakipata.
Kwa sababu kanuni za asili haziendi hivyo.
Huwezi kuziambia kuni nipe moto na zikakupa.
Utapiga kelele sana, utafanya maombi ya kila aina, lakini kuni hizo hazitakupa moto.
Ila kama utazipa kuni hizo moto kidogo, basi zenyewe zitakujibu kwa kukupa moto mwingi zaidi.
Unaona hapo, unatoa kwanza ndiyo unapata.
Ndivyo asili inavyofanya kazi kwenye kila eneo.
Usidhani wewe ni mjanja sana ambaye umekuja na njia ya tofauti ya kukuwezesha kupata bila kutoa.
Unaweza umatumia baadhi ya mbinu kupata bila kutoa, lakini mwisho wa siku utaishia kupoteza chochote ulichopata bila kutoa.
Moja ya falsafa yetu tunayoiishi kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni tunaweza kupata chochote tunachotaka kama tutawapa wengi zaidi kile tunachotaka.
Unawapa kwanza wengine kisha ndiyo unapata kile unachotaka.
Uzuri ni kwamba watu wana vitu vingi wanavyotaka, hivyo ukiacha tu kuwa mbinafsi, lazima utafanikiwa.
Hatua ya kuchukua;
Leo jiulize ni nini ambacho watu wanakitaka sana ambacho unawapatia? Kadiri kitu kinavyokuwa adimu na kuhitajika na wengi, ndivyo thamani yake katika kukupa mafanikio inakuwa kubwa.
Tafakari;
Hakuna anayejali sana wewe unataka nini, lakini kila mtu anajali kile anachotaka yeye. Unaweza kuwa na uhitaji mkubwa wa fedha kwa sababu una gharama muhimu unapaswa kulipia. Utalia hata machozi ya damu kuwaomba watu wakupe fedha hizo lakini hawatajali. Siyo kwa sababu hawana, ila kwa sababu matatizo yako hayana umuhimu kwao kama matatizo yao wenyewe.
Lakini ukijua wanachohitaji sana watu hao na ukawapatia, wanakuwa tayari kukupa fesha unazotaka.
#LetsBuildBusinessea
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed
Asante sana kocha , nitawapa wanavyotaka hili na Mimi animate ninavyotaka
LikeLike