#SheriaYaLeo (313/366); Uvumilivu mkuu.
Muda ni dhana ambayo sisi binadamu tumeitengeneza ili kuweza kuvumilia hali ya ulimwengu usio na ukomo.
Kwa kuwa tumetengeneza muda wenyewe, tuna nguvu ya kuweza kuuathiri, kucheza nao kwa namna fulani.
Tukiwa watoto, muda unaonekana mrefu na unaoenda taratibu.
Lakini tukiwa watu wazima, muda unaonekana mfupi na unaokimbia haraka.
Hivyo basi, muda unategemea sana mtazamo wetu, ambao tunaweza kuubadili.
Hili ni jambo la kwanza tunalopaswa kulielewa kwenye matumizi ya muda.
Kama hisia za ndani zinafanya muda uonekane unaenda haraka, tukiweza kudhibiti hisia zetu muda utakwenda taratibu.
Njia hii ya kukabiliana na vitu huwa inarefusha mtazamo wetu kwenye muda na kufungua fursa ambazo hofu na hasira zimezifunga, kitu kinachotupa uvumilivu ambao ndiyo hitaji muhimu kwenye muda.
Kamwe usionekane ukiharakisha, maana kuharakisha kunaonyesha huna udhibiti kwako mwenyewe na kwenye muda.
Mara zote unekana ukiwa na uvumilivu, kama vile unajua kila kitu kitakuja kwako kwa wakati wake.
Kuwa mpelelezi wa wakati sahihi, nusa hali ya muda na mwenendo utakaokupeleka kwenye madaraka makubwa.
Jifunze kusubiri pale ambapo muda bado na kushambulia kwa ukali pale muda unapokuwa sahihi.
Sheria ya leo; Jifunze uvumilivu. Subiri kwa siku moja kabla ya kuchukua hatua kwenye tatizo linalokukabili. Usionyeshe kukimbizwa na muda, bali onekana kuudhibiti muda.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji