2933; Hatari ya saratani.
Rafiki yangu mpendwa,
Saratani huwa ni ukuaji wa eneo fulani la mwili usio na udhibiti wala ukomo.
Hatari kubwa ya saratani ni pale inapoachwa ikaendelea kukua.
Kadiri saratani inavyochelewa kuondolewa, ndivyo inavyokuwa na hatari kubwa.
Na ubaya wake ni inavyokua haibaki tu pale inapokuwa imeanzia, badala yake inasambaa kwenye maeneo mengine ya mwili.
Hivyo hata unapokuja kuitoa kwa kuchelewa, inakuwa haina maana kwa sababu inakuwa imeshasambaa sana.
Hivyo ndivyo ilivyo kwenye kila eneo la maisha yetu.
Kuna saratani ambazo huwa zinajitokeza na hatari yake inakuwa kubwa kadiri tunavyochelewa kufanya maamuzi.
Inaweza kuwa ni tabia binafsi, unaanza na tabia fulani ndogo ambayo siyo sahihi, lakini huichukulii hatua.
Kinachokuja kutokea ni tabia hiyo inakuwa imekomaa na kuzaa tabia nyingine ambazo ni mbaya pia.
Au inaweza kuwa ni watu unashirikiana nao kama wafanyakazi. Mmoja anaanza kwenda kinyume na taratibu ulizoweka, wewe unamvumilia. Kinachokuja kutokea ni tatizo linakuwa kubwa na wafanyakazi wengine wengi wanakuwa wameungana naye.
Jambo lolote kwenye maisha yako linaloanza kidogo, unapolipuuza linakua na kuleta madhara makubwa zaidi baadaye.
Hivyo unapaswa kuwa kama daktari wa upasuaji, unapoiona saratani inaanza, usiisubirishe, ikate haraka sana kabla haijashika mizizi na kusambaa.
Kila tatizo lolote kubwa ulilonalo sasa halikuanza na ukubwa ambao upo sasa. Lilianza kidogo kidogo, wewe ukalipuuza na likaendelea kukua na sasa unaliona ni hatari.
Chukua mfano wa madeni, hakuna anayeanza akiwa na madeni makubwa ghafla. Bali tabia mbaya ndogo ndogo za kifedha zinajenga madeni madogo madogo mpaka mtu anajikuta kwenye deni kubwa.
Kadhalika kuwa na watu ambao hawakusikilizi na kukuheshimu.
Haikuanza mara moja, bali ilianza kidogo kidogo na wewe ukapuuza ukiona ni kitu kidogo.
Hatimaye kimeshika mizizi na kusambaa. Maana watu huambiana na kuigana kwenye yote wanayofanya.
Weka mipango na taratibu za mambo yote unayofanya.
Kisha pale kitu chochote cha tofauti kinapojitokeza, chukua hatua mara moja na kumalizana nacho.
Usiwe mtu wa kushindwa kufanya maamuzi.
Kumbuka kadiri unavyochelewa kufanya maamuzi, ndivyo tatizo linazidi kukua na kusambaa.
Hiyo haimaanishi ukurupuke na kutatua kila tatizo mara tu unapoliona. Lazima ujihakikishie kwa haraka tatizo ni nini na chanzo chake ni nini. Maana unaweza kukimbilia kuondoa kansa isiyo sahihi. Ukaacha tatizo likiendelea kushika mizizi licha ya kudhani umeshaliondoa.
Uongozi ni kuweza kufanya maamuzi haraka na kuyasimamia mpaka yalete matokeo bora.
Simama humo kama kiongozi wa biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Usijiendee tu kwa kufuata mkumbo.
Jua kila unachojihusisha nacho na namna kinapaswa kuwa.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ili nijiepushe na saratani hii, nitaweka mipango na kisha kufanya kama nilivyopanga mpaka nipate matokeo.
LikeLike
Usiache tatizo mpaka Liwe kubwa.
Kuwa na mpango unaoufuta ili mambo yanapokuwa toafuti uchukuwe hatua haraka.
Simamia biashara yako na maisha yako mpaka upate matokeo mazuri.
LikeLike
Natakiwa kuwa makini na saratani kwani Kadiri ninavyoichelewesha kuiondoa itafikia pahala itashindikana kuondoka
LikeLike
Nisahihi kabisa Doctor/ kocha makirita huu ujumbe wa leo au somo la leo limenilenga leo mimi kwa sababu nina kijana mmoja ambaye ni Dereva anaye nisaidia kwendesha bajaji lakini tayari alikuwa ameisha anza kutengeneza madeni ambayo nilikuta tayari ameisha limbikiza kutokana na sababu zake nyingi ambazo hazikuwa na mashiko yoyote ya maana, kwa hivyo nilijaribu kuzungumza naye kwa mazungumzo ya kuchukulia mfano kutokana na utaratibu wa mwongozo tulio kubaliana kwa mujibu wa kisheria, na nikamweleza wazi kwamba kwenye mkataba wangu nayeye hatukubaliana kutoa sababu na visingizio, bali tulikubaliana kuweka kiasi fulani cha hela kila siku, bila kuacha, kwa hivyo alikuwa tayari ameisha anza kunipima akili ili aone kama nasomeka, nilivyo pambana naye, kwa namna yoyote, ameisha anza kurudi kwenye mstari ambapo anaendelea kulipa kidogo kidogo maana tayari alikuwa ameisha tengeneza deni la 160,000tsh, kwa sasahivi anaendelea kulipunguza ,kitu ambacho nilikiona mapema kutokana na somo la leo ulilo tushirikisha ,kwa kweli kutokana na somo la leo nitaendelea kulitumia katika kila sehemu ya maisha yangu maana linagusa kila eneo au sehemu yoyote ya maisha yetu ya kila siku.
LikeLike
Mbuyu ylianza kama mchicha. Matatizo makubwa yalianza kidogo na baadaye kuwa makubwa. Hii ndio NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
LikeLike
Hakika!
LikeLike
Asante kocha
Ni kweli kila kitu huwa kinaanza kwa udogo kabisa baadae kinakua kikubwa na kushndwa kabisa kukizuia au kukikwepa,ili niweze kufika nakotaka kwenye maisha yangu napaswa kuyaepuka maamuzi na mambo yasiyo sahihi yakiwa bado kwenye uchanga ili yasije nililetea madhara makubwa baadae ambayo sitaweza kuyadhibiti.
LikeLike
Asante kocha,ni somo la kutufanya kuchukua hatua mapema kuliko kupuuzia vidogo vidogo.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo hili. Hakika tunatakiwa kuthibiti chochote katika maisha yetu bado ikiwa katika hali ya udogo.
LikeLike
Ni kweli kabisa kocha kila tatizo tulilonalo leo halikuanza mara moja na kuwa kubwa,kuna namna tuliyapuuza na kuyavumilia matatizo haya.
LikeLike
Hakika kocha kesho yetu haifiki bila kuchukua hatua leo.
LikeLike
Ni kweli kabisa Kocha
LikeLike
Asante Sana kocha, kila kitu kinaanza kidogo kidogo na kujikuta kikiwa kikubwa.
LikeLike
2023🔥🔥
LikeLike